chamtemamoto
JF-Expert Member
- Jul 30, 2013
- 796
- 215
16)(a) MIMBA YA ISA ILIKUWA NI YA SIKU MOJA Quran Suratul Maryam,19:21-22 (Malaika) akasema: Nikama hivyo (unavyosema; lakini) Mola wako amesema Haya ni sahali Kwangu, na ili Tumfanye muujiza kwa wanaasamu na rehema itokayo Kwetu (ndiyo Tumefanya hivi); Na hili ni jambo lililokwisha kuhukumiwa. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali b) MIMBA YA YESU SIKU ZILITIMIA. Luka 2:6-7 ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ngombe kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni NB: Mwezi wa sita uliotajwa katika Luka 1:26 ni mwezi wenye kuelezea umri wa mimba ya Yohana ndani ya tumbo la Elizabethi. Luka 1: 36 Tena tazama jamaa yako Elizabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa NB: Hori iliyotajwa hapa,ina maana ya chombo cha kulishia wanyama kinachokuwa ndani ya zizi. Kwa Kiyunani (Kigiriki) ambayo ndiyo lugha iliyotumika kuandikia Agano Jipya ,chombo hicho kinaitwa Fatne kwa Kiingereza kinaitwa a manger 17)ISA (A.S) ATAKAPORUDI ATAKUJA KUVUNJA MISALABA NA KUUA NGURUWE Mkweli Mwaminifu, Juzuu 3-4, uk.20, Hadithi na. 753 Haisimami saa ya (kiyama) mpaka akuteremkieni nabii Isa (a.s) mwana wa Maryamu atahukumu (kwa sheria ya Kiislamu) (na) muadilifu, basi atavunja misalaba (ya Wakristo Makanisani) na ataua nguruwe, na ataondosha fedheha au (aibu), na mali itazidi kuwa nyingi sana mpaka hataikubali (ataikataa) mtu (kwa kuogopa kiyama) .Soma pia katika Sahihi Bukhar, vol. 3, Hadithi na 425,. Al-Luluwar-Marjan, juzuu ya 1,Hadithi na 95 uk.51. The Noble Quran uk.757 b)YESU KRISTO ATAKAPORUDI ATAWATUMA MALAIKA ZAKE KUWAKUSANYA WATAKATIFU Luka 24:30-31 ndipo itakapoonekana ishara ya mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi, naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu. ONYO LA YESU KRISTO WA NAZARETH Math 24:24 kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini hata walio wateule. (Angalia pia Marko 13:22) Yoh 8:24 Kwa hiyo naliwambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye mtakufa katika dhambi zenu. WEWE MTEULE JE UTADANGANYWA NA KUDANGANYIKA KUWA KWELI ISA A.S NDIYE YESU KRISTO? UKIAMINI HIVYO UTAKUWA UMEDANGANYIKA NA UTAKOSA WOKOVU WA MWENYEZI MUNGU!!!!!!!!!! YESU KRISTO, YEYE NI IMMANUEL, MSHAURI WA AJABU, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, MFALME WA AMANI!!!! (ISAYA 9:6, MATH 1:23)