Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Katika utafiti uliofanyika ndani ya viunga vya Mwanza ambao ulihusisha kuzifanyia uchunguzi dawa za asili za Nguvu za kiume zinazouzwa na watu binafsi, makampuni au watu wa mitishamba na jadi. Dawa hizi za asili zilikutwa na mchanganyiko wa Sildenafil na Tadalafil, Dawa ambazo ni za hospitalini zinazotumika kutibu shida ya kushindwa kusimamisha uume.
Majina ya kampuni ya dawa hizo, yalifichwa kwa taratibu za kimaadili, ila inaonesha ni kiasi gani hawa watu wa dawa za asili uchukuwa dawa za hospitalini na kuzichanganya na mitishamba kisha kudai ni tiba asilia.