Utafiti: Ndoa nyingi zimeshakufa ingawa watu bado wanaishi kama mke na Mume

Okay sasa kama ni hivyo kwanini mnatumia nguvu kubwa kuipinga haki sawa ambayo lengo lake ni kumfanya mwanamke awe financially independent from mwanaume
Kwa hiyo mtakubali kuwe na haki sawa hadi kwenye kuihudumia familia?

Yaani mume na mke wachangie 50/50?
 
Kwa hiyo mtakubali kuwe na haki sawa hadi kwenye kuihudumia familia?

Yaani mume na mke wachangie 50/50?
Hilo mbona wanawake hawana shida nimegundua wanaume ndio mna shida, haki sawa haihusu majukumu ya kiuchumi tu, bali inahusu hata majukumu ya nyumbani nayo inabidi mfanye wote 50 50

Na pia haki sawa haina cha mwanaume kumtawala mwanamke, wala mwanamke kumtii mwanaume inatakiwa kila mmoja ajitawale mwenyewe, na kila mmoja amheshimu na amsikilize mwenzake

Sasa wanaume wengi mkiambiwa hivyo hamtaki yani kwa kifupi ninyi hamtaki haki sawa ila mnataka majukumu sawa tena ikibidi mwanamke ndio afanye zaidi, huko kuendelea kung'ang'ania kwenu mfumo dume ndiko kunafanya wanawake nao washindwe kuwasaidia kuhudumia familia, na waendelee kutaka muwahudumie hata kama wana uwezo wa kuwasaidia
 
Kweli wanawake hamjielewi mnataka nini

Iko hivi ni jukumu la mume kumtunza mke wake hiyo ni haki yenu

Huu mfumo wa haki sawa ukitaka kujua sio mpango wa Mungu ndio maana hata nyinyi unawachanganya kuutetea

Hauwezi kubishana na Muumba hata siku moja. Feminists wanawachanganya sana
 
Nyinyi si ndio huwa mnasema pesa za mwanaume za wote za mwanamke za mwanamke leo tena imekuwa hilo halina shida?
Ndio wanawake huwa wanasema hivyo kwa sababu ya mfumo dume, ila huko kwa wenzetu ambao hawana mfumo dume huwezi kusikia mwanamke akisema hivyo, hata ninyi huku siku mkiachana na mfumo dume basi wanawake wataacha kusema hivyo na wataanza kuwajibika kama ninyi tu
Kwa hiyo mnataka kupingana na Mungu aliyemweka mume kuwa kichwa cha familia?
Si unaona sasa kwahiyo kwenye kuhudumia familia 50 50 mnakubali kirahisi tu na hamuoni kama mnampinga mungu, ila kwenye masuala ya kichwa cha familia ndio mnakumbuka kwamba kuna kumpinga mungu au hujui kwamba mwanaume kuhudumia mke na watoto nao ni mpango wa mungu, kwanza kwanini huwa unamtaja mungu kana kwamba wewe ni mtakatifu yani kwanini wanaume mnataka wanawake wafuate maandiko yote ila ninyi mnachagua yale yanayowanufaisha tu ndio mnayafuata
Hakuna aliyechanganywa wala aliyejichanganya mbona kila kitu kiko wazi hapo, ni vile tu wanaume hamtaki kuukubali ukweli, ila mnajifanya kusingizia kwamba watu wamejichanganya tu hapo

Hiyo mifumo kila mmoja una sheria zake wewe hujalazimishwa kuchagua mfumo fulani uko huru kuchagua mfumo wowote, ila hakikisha unapochagua huo mfumo ukubaliane na sheria zake zote siyo unachagua zile zinazokunufaisha wewe tu, halafu ukae ukijua hii dunia siyo kila mtu anaamini imani unayoamini wewe

Halafu sasa hivi unasema kwamba mke kuhudumiwa na mumewe ni haki yake, ilihali mwanzo umesema wanawake wana njaa sana ndio maana wanaogopa kuachika, yani umeisema kana kwamba mume kumhudumia mke wake ni favour sasa kati ya mimi na wewe nani kajichanganya hapo
 
Hakuna aliyechanganywa wala aliyejichanganya mbona kila kitu kiko wazi hapo
Umekumbuka ulisema haki sawa inamaanisna kwenye ndoa kila mtu ajiamulie mwenyewe hakuna mambo ya mke kumtii mume. Unafikiri hapo ndoa itakuwaje?

Tena ukasema haki sawa yaani 50/50 ikiwezekana hata kwenye kuhudumia familia wakati ni haki yenu kuhudumiwa mkiolewa
 
Wenye akili hawaoi.
Hao ni waoga, kila siku wanaimba oooh mwanamke kiumbe dhaifu kama dhaifu kwanini wasioe?? hawana uhakika na akili za kumuhandle mwanamke, wakiwaza ndoa wanawaza kuchapwa hizo haziwezi kuwa akili
 
Uyo ndugu yetu humu ndani tumejitahidi kumuelewesha kwa muda mrefu sana lakini tumeshindwa, nimefarijika sana kuona kajibiwa hivi na mwanamke.
 
Mkuu ndoa haina haki sawa, ndoa ni mpango wa Mungu mwenyewe, mambo ya haki sawa yaache kazini kwako ukiingia ndani mume ndio mwenye sauti, na huo mpango wa Mungu uko hivi:

Mwanzo 3:16
[16]Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
 
Sasa hiyo inakuwaje sababu hebu nifafanulie mkuu
Jadda , pale mwanzo ulisema. Wanaume wanapaswa kuchagua mama wa nyumbani zidi ya wanawake wanao fanya kazi au wafanyabiashara. Kwa kua hao wanaofanya kazi,hawawezi kutimiza majukumu ya nyumbani.
Hivyo nikauliza kuwa kwa maana hiyo mwanamke akiwa mfanyakazi ni tiketi ya ndoa kuvunjika?
 
Hii comment itatibu ndoa nyingi, nimepata elimu kubwa
 
Mtume Paul,alishasema ukiona huwezi kuoa ni bora usioe ,1 Wakorintho 1:8
"8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo"...
 
Hao ni waoga, kila siku wanaimba oooh mwanamke kiumbe dhaifu kama dhaifu kwanini wasioe?? hawana uhakika na akili za kumuhandle mwanamke, wakiwaza ndoa wanawaza kuchapwa hizo haziwezi kuwa akili
Wewe unawaza kuchapwa na mambo ya kumuhandle mwanamke lakini wenye akili hata muda wa kujishughulisha na wanawake hawana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…