Utafiti: Ndoa nyingi zimeshakufa ingawa watu bado wanaishi kama mke na Mume

Utafiti: Ndoa nyingi zimeshakufa ingawa watu bado wanaishi kama mke na Mume

Okay sasa kama ni hivyo kwanini mnatumia nguvu kubwa kuipinga haki sawa ambayo lengo lake ni kumfanya mwanamke awe financially independent from mwanaume
Kwa hiyo mtakubali kuwe na haki sawa hadi kwenye kuihudumia familia?

Yaani mume na mke wachangie 50/50?
 
Kwa hiyo mtakubali kuwe na haki sawa hadi kwenye kuihudumia familia?

Yaani mume na mke wachangie 50/50?
Hilo mbona wanawake hawana shida nimegundua wanaume ndio mna shida, haki sawa haihusu majukumu ya kiuchumi tu, bali inahusu hata majukumu ya nyumbani nayo inabidi mfanye wote 50 50

Na pia haki sawa haina cha mwanaume kumtawala mwanamke, wala mwanamke kumtii mwanaume inatakiwa kila mmoja ajitawale mwenyewe, na kila mmoja amheshimu na amsikilize mwenzake

Sasa wanaume wengi mkiambiwa hivyo hamtaki yani kwa kifupi ninyi hamtaki haki sawa ila mnataka majukumu sawa tena ikibidi mwanamke ndio afanye zaidi, huko kuendelea kung'ang'ania kwenu mfumo dume ndiko kunafanya wanawake nao washindwe kuwasaidia kuhudumia familia, na waendelee kutaka muwahudumie hata kama wana uwezo wa kuwasaidia
 
Kweli wanawake hamjielewi mnataka nini

Iko hivi ni jukumu la mume kumtunza mke wake hiyo ni haki yenu

Huu mfumo wa haki sawa ukitaka kujua sio mpango wa Mungu ndio maana hata nyinyi unawachanganya kuutetea

Hauwezi kubishana na Muumba hata siku moja. Feminists wanawachanganya sana
 
Nyinyi si ndio huwa mnasema pesa za mwanaume za wote za mwanamke za mwanamke leo tena imekuwa hilo halina shida?
Ndio wanawake huwa wanasema hivyo kwa sababu ya mfumo dume, ila huko kwa wenzetu ambao hawana mfumo dume huwezi kusikia mwanamke akisema hivyo, hata ninyi huku siku mkiachana na mfumo dume basi wanawake wataacha kusema hivyo na wataanza kuwajibika kama ninyi tu
Kwa hiyo mnataka kupingana na Mungu aliyemweka mume kuwa kichwa cha familia?
Si unaona sasa kwahiyo kwenye kuhudumia familia 50 50 mnakubali kirahisi tu na hamuoni kama mnampinga mungu, ila kwenye masuala ya kichwa cha familia ndio mnakumbuka kwamba kuna kumpinga mungu au hujui kwamba mwanaume kuhudumia mke na watoto nao ni mpango wa mungu, kwanza kwanini huwa unamtaja mungu kana kwamba wewe ni mtakatifu yani kwanini wanaume mnataka wanawake wafuate maandiko yote ila ninyi mnachagua yale yanayowanufaisha tu ndio mnayafuata
Kweli wanawake hamjielewi mnataka nini

Iko hivi ni jukumu la mume kumtunza mke wake hiyo ni haki yenu

Huu mfumo wa haki sawa ukitaka kujua sio mpango wa Mungu ndio maana hata nyinyi unawachanganya kuutetea

Hauwezi kubishana na Muumba hata siku moja. Feminists wanawachanganya sana
Hakuna aliyechanganywa wala aliyejichanganya mbona kila kitu kiko wazi hapo, ni vile tu wanaume hamtaki kuukubali ukweli, ila mnajifanya kusingizia kwamba watu wamejichanganya tu hapo

Hiyo mifumo kila mmoja una sheria zake wewe hujalazimishwa kuchagua mfumo fulani uko huru kuchagua mfumo wowote, ila hakikisha unapochagua huo mfumo ukubaliane na sheria zake zote siyo unachagua zile zinazokunufaisha wewe tu, halafu ukae ukijua hii dunia siyo kila mtu anaamini imani unayoamini wewe

Halafu sasa hivi unasema kwamba mke kuhudumiwa na mumewe ni haki yake, ilihali mwanzo umesema wanawake wana njaa sana ndio maana wanaogopa kuachika, yani umeisema kana kwamba mume kumhudumia mke wake ni favour sasa kati ya mimi na wewe nani kajichanganya hapo
 
Hakuna aliyechanganywa wala aliyejichanganya mbona kila kitu kiko wazi hapo
Umekumbuka ulisema haki sawa inamaanisna kwenye ndoa kila mtu ajiamulie mwenyewe hakuna mambo ya mke kumtii mume. Unafikiri hapo ndoa itakuwaje?

Tena ukasema haki sawa yaani 50/50 ikiwezekana hata kwenye kuhudumia familia wakati ni haki yenu kuhudumiwa mkiolewa
 
Wenye akili hawaoi.
Hao ni waoga, kila siku wanaimba oooh mwanamke kiumbe dhaifu kama dhaifu kwanini wasioe?? hawana uhakika na akili za kumuhandle mwanamke, wakiwaza ndoa wanawaza kuchapwa hizo haziwezi kuwa akili
 
MKwa uzoefu wangu,mwanamke wa ndoa kufanya kazi za nyumbani ni kujipanga.My experience nilikuwa na dada wa kazi wakati watoto wangu ni wadogo .Walivyoenda form 1 boarding wote ,niliondoa dada na principle yangu kuanzia wakiwa primary wakiwa holiday dada anaenda likizo na wenyewe wanajipanga na kila siku tunapanga majukumu ya nyumbani pamoja(from Baba yao mpaka watoto) .Mimi nafanya kazi ,tena niko busy sana na ni bosi mkubwa tu kwa level ya director na bado naweza kupika naosha vyombo nafanya usafi(utakuta mwanamke analipa kwenda "gym" akiamua kazi za nyumbani akafanya ndio gym yake) .Watoto wako university na sina dada wa kazi for almost 5 yrs now nina kijana anakuja twice a week kwa ajili ya huko nje tu.Niko Likizo ndio maana nina muda hata wa kuelimisha wamama wenzangu (sisemi kila kitu kita work kwa kila mtu) ila malezi na exposure ni muhimu sana.Kwa kuwa ungekuwa ulaya una luxury ya kuwa na mdada wa kazi unajipanga my dear.
Uyo ndugu yetu humu ndani tumejitahidi kumuelewesha kwa muda mrefu sana lakini tumeshindwa, nimefarijika sana kuona kajibiwa hivi na mwanamke.
 
Hilo mbona wanawake hawana shida nimegundua wanaume ndio mna shida, haki sawa haihusu majukumu ya kiuchumi tu, bali inahusu hata majukumu ya nyumbani nayo inabidi mfanye wote 50 50

Na pia haki sawa haina cha mwanaume kumtawala mwanamke, wala mwanamke kumtii mwanaume inatakiwa kila mmoja ajitawale mwenyewe, na kila mmoja amheshimu na amsikilize mwenzake

Sasa wanaume wengi mkiambiwa hivyo hamtaki yani kwa kifupi ninyi hamtaki haki sawa ila mnataka majukumu sawa tena ikibidi mwanamke ndio afanye zaidi, huko kuendelea kung'ang'ania kwenu mfumo dume ndiko kunafanya wanawake nao washindwe kuwasaidia kuhudumia familia, na waendelee kutaka muwahudumie hata kama wana uwezo wa kuwasaidia
Mkuu ndoa haina haki sawa, ndoa ni mpango wa Mungu mwenyewe, mambo ya haki sawa yaache kazini kwako ukiingia ndani mume ndio mwenye sauti, na huo mpango wa Mungu uko hivi:

Mwanzo 3:16
[16]Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
 
Sasa hiyo inakuwaje sababu hebu nifafanulie mkuu
Jadda , pale mwanzo ulisema. Wanaume wanapaswa kuchagua mama wa nyumbani zidi ya wanawake wanao fanya kazi au wafanyabiashara. Kwa kua hao wanaofanya kazi,hawawezi kutimiza majukumu ya nyumbani.
Hivyo nikauliza kuwa kwa maana hiyo mwanamke akiwa mfanyakazi ni tiketi ya ndoa kuvunjika?
 
Ndoa ni muhimu lakini sio lazima.Mimi kwa uzoefu wangu wa miaka 20plus nimejifunza mengi sana.Mojawapo ni kuwa furaha yako hupati kwa mwenzako kama nilivyokuwa nafikiria ,pia tunaingia kwenye ndoa na matarajio makubwa kutoka kwa kila mmoja wetu.Sasa kikubwa kwenye ndoa ni kupata mtu unae endana nae angalao kwa asilimia 40% kitabia na pia kila mmoja aweze kuchukua mapungufu ya mwenzake kama yakwake na kuyafanyia kazi na kuyakubali na sio kumbadilisha.Mfano ,mimi nilimkuta mume wangu ni mywaji (sisemi mlevi) ila mimi sinywi so nilichofanya ni kuakikisha nampa muda wake wa kunywa kama ndio kitu kinampa furaha uwezi amini after 15yrs ameacha mwenyewe na hataki hata kusikia kwa kuwa ameona haimpi faida wala kwa umri wake sio kitu kinampa furaha nay more.Shida ni pale sasa unataka kumbadilisha fika uliolewa unajua kabisa ulimkuta anakunywa ,unafoka,unanuna why !unless aanze mkiwa ndani ya ndoa that is something else huu ni mfano mmoja tu.Kikingine lazima muweke issue za finances /kifedha wazi ,haijalishi nani anapata zaidi au hapati,try to communicate kwa habari ya budget,spending nk including investment au namna ya kuongeza kipato.Ukiona mwenzako anatumia kipato let say anamchepuko huwa nawaambia ladies be calm ,deal na furaha yako my dear you can not compete with man chini ya jua.Jipende,jidhamini ,glow my dear ,kama ulikuwa unaenda maili moja kutafuta fedha move to next miles jifanye hata ujui kinachoendelea (yaani ignore).Kingine ile mwanzo tu hamjaoana ,muwe na moment together tafuta karatasi kila mtu aandike anachokipenda kwa mwenzake ,anachokichukia na nini anataka afanyie,review after one year and hii iwe sehemu ya maisha yenu kila mwaka mshirikishe Mungu (sio mchungaji ,shehe.mashoga au nabii) wewe na Mungu wako.Trust me ,ndoa ni PARADISO nina enjoy
Hii comment itatibu ndoa nyingi, nimepata elimu kubwa
 
Mtume Paul,alishasema ukiona huwezi kuoa ni bora usioe ,1 Wakorintho 1:8
"8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo"...
 
Hao ni waoga, kila siku wanaimba oooh mwanamke kiumbe dhaifu kama dhaifu kwanini wasioe?? hawana uhakika na akili za kumuhandle mwanamke, wakiwaza ndoa wanawaza kuchapwa hizo haziwezi kuwa akili
Wewe unawaza kuchapwa na mambo ya kumuhandle mwanamke lakini wenye akili hata muda wa kujishughulisha na wanawake hawana.
 
Back
Top Bottom