Utafiti: Ndoa nyingi zimeshakufa ingawa watu bado wanaishi kama mke na Mume

Utafiti: Ndoa nyingi zimeshakufa ingawa watu bado wanaishi kama mke na Mume

Juzi tulikua tunajadili Yule mwanamke alomng'ata mmewe mpaka kuelekea logo chake.Basi katika stori mi na mr.nikmwambia lakini si sheria inasema kuvumilia katika shida na Raha.Mr.ananiambia inabidi sa hivi hicho kipengele kinadilishwe au waspesfy kabisa ni shida zipi.


Kiukweli ndoa nyingi zipo ICU ndani japo nje zinaonekana hai.
Ni kweli, huu mtaa ninaoishi hakuna ndoa hata moja iko salama mpaka najiuliza why watu wanajiita wanandoa na mipete ili hali ndoa zilishajifia.
 
Hatuhudumii mademu
Lakini hao hao mademu mnataka wawaheshimu na wakiwa kwenu wafanye majukumu yote kama wake wa ndoa
Sio mimi aliyeanzisha ndoa ndio anataka hivyo
Sawa sasa siyo kila mtu anamuamini huyo unayemuamini wewe, kikubwa we deal na wanawake wenye mtazamo kama wako tu, wenye mitazamo tofauti waachie wengine wanaofanana na wanaoelewana
Kwenye familia ni sawa
Sasa basi ndio mhudumie wake zenu bila kutaka wawasaidie majukumu yenu
 
Sema Ndoa yako ndiyo iliyo kushinda, Ndoa nyingi kivipi wewe umefanya tafiti wapi, leta data hapa zinazo onyesha juu ya unacho kisema. Wewe sema ndoa yako imekushinda tujue cha kukusaidia au kukushauri.

Changamoto za hapa na pale hazikosekani shida ni kuendekeza mfumo dume, mwanaume una taka kuwa juu kwa msemo wa Mwanaume akosei na Mwanamke hataki kujishusha kumsikiliza mume nini anasema maana amesha ambiwa Mwanamke bila hata mwanaume anaweza, sasa hapa ndoa itawezekana vipi.

Mzee kama una endekeza mfumo dume kwenye ndoa yako karne hii ya 21 utakula za Uso kwenye kila ndoa unayo ingia we Kilaza.

Na kama utajitetea hupo kwenye ndoa jibu kwanini haupo kwenye ndoa, watu tupo kwenye ndoa na maisha yanaenda japo kabla ya kuingia kwenye ndoa nilisha kutana na watu wengi kama wewe wanaosema ndoa mbaya mara ndoa ndoano.

Watu wapo busy kuogopesha watu kuingia kwenye ndoa ila wao wapo kwenye ndoa na kutoka hawataki.

Kama mliokotana barabarani mkuu pambana sana.

Ndoa ni tamu zaidi ya sanaaa kama hamku okotana.

Hope ume nielewa mzee.
Hujaeleweka, andika hizo faida za ndoa unazosema.
 
wanaume wangapi kila siku wanalalamika kwamba wanawake ni wavivu hawataki kutafuta pesa wanasubiri kuhudumiwa kama walemavu
Mke mwema anayetajwa kwenye maandiko METHALI 31 hakutajwa ni mvivuna mbinafsi

METHALI 31:14
14. Huleta chakula chake kutoka mbali.

METHALI 31:27
27. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.




Mungu anataka mke awe wa aina hii ndiyo maana hasa ya msaidizi
 
kila mtu anaamini unachoamini wewe na siyo kila mtu anayaona mambo kama unavyoamini wewe, wewe kama unaona ndoa lazima iwe na kiongozi ni sawa ila tu tafuta mwanamke ambaye atakuwa na mtazamo kama huo wako
Sio mtazamo wangu

1 Wakorintho 11:3

Neno: Bibilia Takatifu

3 Lakini napenda muelewe kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, kama vile mume alivyo kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo
 
Mwanamke atoke kazini saa 12 aingie jikoni kupika bado muda wa kulala akate viuno hii ni ngumu
Mimi nilishaachanaga na hiz habar zenu. Nilishaachaga kuongea ongea so ni yeye tu, akijisikia kupika sawa, asipojisikia sawa. Akijisikia kufua sawa asipojisikia okay, akijisikia kuamka saa 5 asbh weekend sawa au akiishia kulala siku nzuma ni yeye tu, akijisikua kutoka out ni yeye, yan nilishaachaga kuzozana vitu vya kijinga wakat naweza kuji take care mwenyewe binafsi, so yf mimi yupo tu kama mpangaji mwenzangu home. She is free to wharever she wants, tunaweza kaa the whole weekend kimya tuuu bila kuzungumza kila mtu na biznez zake. Nitasafir kwenda mkoa kikaz (napenda kusafir usiku) ,nitafika nakokwenda na kurudi home no contact no nothing.

Kitu cha msingi sana kwa mwanaume, saana, just make u have money most of time if not always ili uweze kwenda popote na kufanya chochote muda wowote. Vinginevyo, mwanamje anaweza akakuua kwa msongo wa mawazo.
 
Ni kweli, huu mtaa ninaoishi hakuna ndoa hata moja iko salama mpaka najiuliza why watu wanajiita wanandoa na mipete ili hali ndoa zilishajifia.
Mi sijawah kuvaa pete ya ndoa my whole life licha kuoa over 10 years sasa.

Yf alivaa vaa kama 3 years hiv naye akapoteza sijui akazigawa hata i dont know na sikuwah kumuuliza, ilanpete yangu mimi tulivyofunga tu ndoa nikamkabidhi kwamba have it, cant wear it
 
Ndoa ni muhimu lakini sio lazima.Mimi kwa uzoefu wangu wa miaka 20plus nimejifunza mengi sana.Mojawapo ni kuwa furaha yako hupati kwa mwenzako kama nilivyokuwa nafikiria ,pia tunaingia kwenye ndoa na matarajio makubwa kutoka kwa kila mmoja wetu.Sasa kikubwa kwenye ndoa ni kupata mtu unae endana nae angalao kwa asilimia 40% kitabia na pia kila mmoja aweze kuchukua mapungufu ya mwenzake kama yakwake na kuyafanyia kazi na kuyakubali na sio kumbadilisha.Mfano ,mimi nilimkuta mume wangu ni mywaji (sisemi mlevi) ila mimi sinywi so nilichofanya ni kuakikisha nampa muda wake wa kunywa kama ndio kitu kinampa furaha uwezi amini after 15yrs ameacha mwenyewe na hataki hata kusikia kwa kuwa ameona haimpi faida wala kwa umri wake sio kitu kinampa furaha nay more.Shida ni pale sasa unataka kumbadilisha fika uliolewa unajua kabisa ulimkuta anakunywa ,unafoka,unanuna why !unless aanze mkiwa ndani ya ndoa that is something else huu ni mfano mmoja tu.Kikingine lazima muweke issue za finances /kifedha wazi ,haijalishi nani anapata zaidi au hapati,try to communicate kwa habari ya budget,spending nk including investment au namna ya kuongeza kipato.Ukiona mwenzako anatumia kipato let say anamchepuko huwa nawaambia ladies be calm ,deal na furaha yako my dear you can not compete with man chini ya jua.Jipende,jidhamini ,glow my dear ,kama ulikuwa unaenda maili moja kutafuta fedha move to next miles jifanye hata ujui kinachoendelea (yaani ignore).Kingine ile mwanzo tu hamjaoana ,muwe na moment together tafuta karatasi kila mtu aandike anachokipenda kwa mwenzake ,anachokichukia na nini anataka afanyie,review after one year and hii iwe sehemu ya maisha yenu kila mwaka mshirikishe Mungu (sio mchungaji ,shehe.mashoga au nabii) wewe na Mungu wako.Trust me ,ndoa ni PARADISO nina enjoy
Umeua vibaya sana,congrats
 
Mke mwema anayetajwa kwenye maandiko METHALI 31 hakutajwa ni mvivuna mbinafsi

METHALI 31:14
14. Huleta chakula chake kutoka mbali.

METHALI 31:27
27. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.




Mungu anataka mke awe wa aina hii ndiyo maana hasa ya msaidizi

Sio mtazamo wangu

1 Wakorintho 11:3​

Neno: Bibilia Takatifu​

3 Lakini napenda muelewe kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, kama vile mume alivyo kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo
Hapana hayo siyo maagizo ya mungu bali yalikuwa mawazo ya mfalme suleiman kama ambavyo watu wanasema kwamba mwanaume kuoa mke mmoja siyo maagizo ya mungu bali yalikuwa mawazo ya mtume paulo, kingine ambacho narudia kusisitiza ni kwamba siyo kila mtu ana dini kama yako hivyo usipenda kujadili mada za jumla kwa kutumia vitabu vya dini yako, duniani dini kubwa zenye wafuasi wengi ziko zaidi ya 10 na kila moja ina miungu yake na maandiko yake achilia mbali zile dini ndogo zenye wafuasi wachache ambazo ni zaidi ya 5000
 
Hapana hayo siyo maagizo ya mungu bali yalikuwa mawazo ya mfalme suleiman kama ambavyo watu wanasema kwamba mwanaume kuoa mke mmoja siyo maagizo ya mungu bali yalikuwa mawazo ya mtume paulo, kingine ambacho narudia kusisitiza ni kwamba siyo kila mtu ana dini kama yako hivyo usipenda kujadili mada za jumla kwa kutumia vitabu vya dini yako, duniani dini kubwa zenye wafuasi wengi ziko zaidi ya 10 na kila moja ina miungu yake na maandiko yake achilia mbali zile dini ndogo zenye wafuasi wachache ambazo ni zaidi ya 5000
Hili ni tatizo la wabongo wangi, wanadhani kila mtu ni mkristo au muislam. Dunia yenye watu bilioni saba na ushee dini hizo mbili hazifiki hata nusu ya watu duniani .
 
Back
Top Bottom