Utafiti: Ukatili wa kiuchumi kwa Wanaume umeongezeka, kunyimwa haki ya kuwa na mtoto pia ni Ukatili

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374

Msaidizi wa Mratibu wa Dawati la Jinsi na Watoto wa Jeshi la Polisi Tanzania, ACP Faidha Suleiman
akiwa katika moja ya majukumu yake ya kutoa elimu kwa wananchi.


Licha ya kuzoeleka matukio ya wanaume kuhusika kuwafanyia ukatili wanawake mara nyingi, utafiti umebaini kibao imegeuka na kuna ukatili mwingi wanaofanyiwa wanaume.

Ukatili upo wa aina nyingi, baadhi ni kunyimwa haki ya kuwa na mtoto baada ya kutengana na wazazi wenza, wanawake wakiamini wao ndio wenye haki ya kila kitu kwa mtoto, pia kuna ukatili wa kiuchumi ambao huu umekuwa ukiwaumiza wanaume wengi kisaikolojia.

Msaidizi wa Mratibu wa Dawati la Jinsi na Watoto wa Jeshi la Polisi Tanzania, ACP Faidha Suleiman anasema: “Ukatili wa kiuchumi ndio mkubwa, wanaume wanaombwa sana hela au wanakosa mamlaka ya matumizi ya fedha wanazotafuta wao, wenza wanawabana na kuwaumiza kiuchumi, tunapata kesi nyingi za aina hiyo kwa kuwa wanaume wenyewe wanazungumza kwa sasa.”

Anaongeza: “Baadhi ya ukatili upo wa kupigwa, kuchukuliwa fedha, kadi za bank, pia kuna ukatili ulioshamiri hivi karibuni wa wanaume kunyang’anywa watoto, wanawake wengi wamekuwa hawawapi watoto haki za kuwa na baba zao.

“Matukio haya mara nyingi yanatokea Mijini kuliko Vijijini, zamani wanaume walikuwa hawasemi lakini miaka ya hivi karibuni imekuwa kawaida wao kuzungumza.

“Moja ya sababu kubwa ya kuongezeka kwa ukatili kwa wanaume ni maendeleo ya utandawazi, wanawake wanajifunza mambo mengi kupitia mitandao mbalimbali.

“Jamii inapaswa kuwa huru na kufunguka, utafiti tulioupata unaonesha matukio haya yanatokea sehemu mbalimbali nchini.”
 
Cc Esmadomokaya vs Petit mbebapochi wa wema
 
Ukatili wa kiuchumi upo,
Hata hizi harakati za kumkomboa mwanamke zinachangia.

Mfano:
1. Kuna ile sheria ya MKE kukopa pesa ya familia, afu Deni anaandikiwa mume.
Kuna baadhi ya Wanawake wanaitumia kwa manufaa yao binafsi.

2. Sheria ya matunzo kwa mtoto,
Wanaume wanaombwa pesa nyingi za matunzo, ambayo kiuhalisia hayafiki kwa mtoto husika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli, una hoja.
 
wanawake wanang'ang'ania kukaa na watoto ili uwape hela ya matunzo
 
Yote hayo yanachagizwa na umaskini wa fikra.

Pelekeni shule watoto wakaelimike.
 
Sasa kama mwanamke kaamua kunikomoa amekimbia na watoto, sawa tu akimbie akalee mwenyewe huko anakopakimbilia, ugomvi wa kugombania watoto sitaki
 
sema hao jamaa sijui wanatathmini kitu gani kwa afande,maana dah.
 
Hii hali wala haipo kihivyoooo
Sema tu munailazimisha, sasa ngojeni ikolee ndio mutajua utamu wake
 
Depal wewe endelea tu kuniomba hela mimi hata sitakupelea kwenye dawati la jinsia...

Hahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…