John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Msaidizi wa Mratibu wa Dawati la Jinsi na Watoto wa Jeshi la Polisi Tanzania, ACP Faidha Suleiman
akiwa katika moja ya majukumu yake ya kutoa elimu kwa wananchi.
Licha ya kuzoeleka matukio ya wanaume kuhusika kuwafanyia ukatili wanawake mara nyingi, utafiti umebaini kibao imegeuka na kuna ukatili mwingi wanaofanyiwa wanaume.
Ukatili upo wa aina nyingi, baadhi ni kunyimwa haki ya kuwa na mtoto baada ya kutengana na wazazi wenza, wanawake wakiamini wao ndio wenye haki ya kila kitu kwa mtoto, pia kuna ukatili wa kiuchumi ambao huu umekuwa ukiwaumiza wanaume wengi kisaikolojia.
Msaidizi wa Mratibu wa Dawati la Jinsi na Watoto wa Jeshi la Polisi Tanzania, ACP Faidha Suleiman anasema: “Ukatili wa kiuchumi ndio mkubwa, wanaume wanaombwa sana hela au wanakosa mamlaka ya matumizi ya fedha wanazotafuta wao, wenza wanawabana na kuwaumiza kiuchumi, tunapata kesi nyingi za aina hiyo kwa kuwa wanaume wenyewe wanazungumza kwa sasa.”
Anaongeza: “Baadhi ya ukatili upo wa kupigwa, kuchukuliwa fedha, kadi za bank, pia kuna ukatili ulioshamiri hivi karibuni wa wanaume kunyang’anywa watoto, wanawake wengi wamekuwa hawawapi watoto haki za kuwa na baba zao.
“Matukio haya mara nyingi yanatokea Mijini kuliko Vijijini, zamani wanaume walikuwa hawasemi lakini miaka ya hivi karibuni imekuwa kawaida wao kuzungumza.
“Moja ya sababu kubwa ya kuongezeka kwa ukatili kwa wanaume ni maendeleo ya utandawazi, wanawake wanajifunza mambo mengi kupitia mitandao mbalimbali.
“Jamii inapaswa kuwa huru na kufunguka, utafiti tulioupata unaonesha matukio haya yanatokea sehemu mbalimbali nchini.”