UTAFITI: Watanzania Mungu wetu ni mmoja, tena mwenye nguvu na wa kweli, ila wenyewe hatujui tu

UTAFITI: Watanzania Mungu wetu ni mmoja, tena mwenye nguvu na wa kweli, ila wenyewe hatujui tu

Ni jambo la ajabu kuukataa utaifa wako, Mungu hakukosea kukuumba wewe Mtanganyika. Msingi wa huu muungano ni utaifa wa Tanganyika na Zanzibar ambayo ndiyo mataifa yaliyopata uhuru. Tanzania haijawahi kutawaliwa na mkoloni, wala haijawahi kupata uhuru. Tunapotaka kuukataa huu ukweli ndiyo matatizo huanza. Tanzania ni chombo cha kisiasa kilichotengenezwa kuyanganisha haya madola mawili, ya Tanganyika na Zanzibar.

Tanganyika ndiyo imebeba kumbukumbu za mababu zetu, siyo Tanzania. Tanganyika ndiyo ina makovu ya ukoloni, utumwa na ushahidi wa mapambano yetu dhidi ya watawala wa kigeni. Hii historia ndiyo inatuunganisha watanganyika wote. Historia ya Mkutano wa Berlin 1884-1885 ni ya Tanganyika, siyo Tanzania wala Zanzibar. Historia ya vita vya maji-maji ni ya Tanganyika, siyo Tanzania wala Zanzibar.

Wakati Tanganyika inagawanywa na wakolini kule Berlin, Zanzibari lilikuwa ni taifa tayari ambalo linatawaliwa na Sultan. Mbaya zaidi nalo lilitaka kushirikishwa kwenye ule mkutano likidai kwamba baadhi ya maeneo ya Tanganyika kama Arusha, Kilimanjaro, Mkondokwa na Usagara ni yake. Ushahidi upo unaonyesha Sultan wa Zanzibar akiandika barua kwa mfalme wa Ujerumani kwamba kwanini yeye hukushirikishwa kwenye mkutano wa Berlin.

Hivi unadhani ni jambo sahihi kusema kwamba siku ya uhuru wa Tanganyika ndiyo siku ya uhuru wa Tanzania, ilhali Zanzibari hajapitia mambo yale ambayo sisi watanganyika tumepitia, ??

Kutaka kulazimisha kwamba uhuru wa Tanganyika ndiyo uhuru wa Tanzania ni kukosa hekima na kuzitukana kumbukumbu za mababu zetu kwasababu za kisiasa. Zanzibar hawataki huu muungano kwasababu wamekuwa na utaifa wao kwa zaidi ya miaka 200. Sisi utaifa wetu umeanza mwaka 1961, bahati mbaya ukabakwa na wajamaa kwasababu wanazozijua wenyewe.
Uishi milele mkuu! Umeniyafakarisha kiasi cha kutokwa machozi ya furaha yaliyochanganyikana na uchungu
 
Back
Top Bottom