Hajawai kukutana na double allocations za hati.
Kiwanja kimoja kina hati tatu zenye wamiliki tofauti na zote zimetolewa na manispaa ama wizara ya ardhi
Hayo mnayoyasema inawezekana ikawa ni kweli ,Lakini sijawahi kuskia mtu akilalamika ametapeliwa kiwanja na ana Hati miliki ya wizara ya hicho kiwanja
Kwa Dunia ya Leo kama hao watu wengekuepo wangesha share experience yao
Kuhusu utoaji wa Hati miliki ya wizara , Mansipaa na halimashauri zinazingatia vitu vingi
Kuna zile cordinate point za beacons ambazo zinazunguka kiwanja ,zile ndo zinatambulisha mipaka halisi ya kiwanja
Ukiachana na hilo kuna hili la kuweka jina la mmliki kwenye ramani ya mipango mji
Kuna swala la Nida
Haya yote yafanyike alafu Bado kiwanja kimoja kitolewe hati tatu kwa wakati mmoja?
Basi tutakua na serikali ya hovyo sana
Me nna amini hilo haliwezi kutokea
Niwape mfano rahisi ,hili sakata linaloendeles kule bagamoyo makurunge baina ya serikali ya Zanzibar na watu walionunua kule , Serikali ya Zanzibar hawakua na Hati miliki ndo maana waliouziwa pale waliweza kufanikisha mpaka mchakato wa Hati miliki kutoka wizarani
Msichukulie mambo kirahisi hvyo
Kama kuna mtu ambaye ameshawai kutapeliwa kiwanja akiwa na Hati miliki ya wizarani aje hapa atupe hicho kisa chake