Utafutaji wa kiwanja umenifanya nielewe mwanadamu ni hatari sana

Na kwanini nitumie pesa kupata haki yangu?
Ukisema hati ni haki yako sio kweli, Hati inabidi ifanyiwe mchakato mpaka kukamilika

Imagine umenunua eneo ambalo halijapimwa ,afu unataka hati, Hapo lazima umpate surveyor akalipime kwanza ,waje watu wa mipango mji kujiridhisha kama eneo lipo sehemu sahihi kwa makazi, Bado uende ukachukue form za mipaka ambazo majirani wako wanatakiwa waziisign, kuna issue ya kuweka beacons ,baada hapo upewe form zingine za kujaza details zako ziende wizarani , upewe control number za kulipia makadirio ya Kodi ya eneo husika ,

Haya yote hata ukisema uyafanye mwenyewe lazima hela ikutoke tuu,

Kiwanja kimoja kinaweza kikakugharimu hata 500k mpaka kufanikisha hati miliki kama utafutailia wewe mwenyewe
 
Sasa utakua mjinga kiasi gan ukubali kununua hicho kiwanja kabla ya kuanza process za ku transfer
Kumbuka hati Inaweza kutumika hata kuombea mkopo, kwa mantiki hiyo ,kama mtu anajielewa hawezi kubali kununua kiwanja chenye hati kabla ya kwenda wizarani kuanza process za transfer
Mmh nakushangaa utaanza je process ya transfer kabla ya kulipia hicho kiwanja, unafikiri mchakato wa transfer ni siku mbili au wiki ata miezi sita inaisha transifer bado.......
 
Ukisema hati ni haki yako sio kweli, Hati inabidi ifanyiwe mchakato mpaka kukamilika

Imagine umenunua eneo ambalo halijapimwa ,afu unataka hati, Hapo lazima umpate surveyor akalipime kwanza ,waje watu wa mipango mji kujiridhisha kama eneo lipo sehemu sahihi kwa makazi, Bado uende ukachukue form za mipaka ambazo majirani wako wanatakiwa waziisign, kuna issue ya kuweka beacons ,baada hapo upewe form zingine za kujaza details zako ziende wizarani , upewe control number za kulipia makadirio ya Kodi ya eneo husika ,

Haya yote hata ukisema uyafanye mwenyewe lazima hela ikutoke tuu,

Kiwanja kimoja kinaweza kikakugharimu hata 500k mpaka kufanikisha hati miliki kama utafutailia wewe mwenyewe
Ikugharimu 500k tu wewe unatania kama sehemu haina mchoro wa wizara huo mchoro tu ni zaidi ya 3m upelekwe wizarani kufanyiwa approval ambao sio chini ya miezi sita kwasbb na yenyewe ina process zake pia, mchoro ulirudi ndo uanze ku- process hati yako umlipe saviour sio chini ya 300k ulipia na kodi za TRA na za almashauri ili upate hiyo hati sio mchozo.
 
Pesa, Ardhi na Mapenzi.

Hivi ni vitu vilivyo mwaga damu sana, vilivyo karibisha ushetani, vilvyo vunja utu na vilivyo tengeneza uhasama mkubwa sana.

Lakini bado ni vitu vyenye thamani kuliko vitu vyote.

Unapotafuta kiwanja, inabidi uwekeze zaidi katika umakini na upelelezi.

Kuna sehemu nilipata kiwanja, jamaa akawa tayari kuniuzia, lakini kumbe nyuma ya pazia kile kiwanja ni urithi wa watoto wa kaka yake yani baada ya kaka yao kufariki na barua zipo. Yeye akawa amepewa cha nyuma yake ila yeye anang'ang'ania pote.

Kuna sehemu nilipata kiwanja, jamaa akawa ananihakikishia kabisa kuwa hakuna tabu na hadi majirani zake (kabila moja) pale wakawa wanachochea. Lakini kwa bahati nzuri kuna afisa ardhi anaishi pembeni na anamjua mshikaji wangu niliekuwa nae, akatuita pembeni na kuniambia kuwa hapo pana mgogoro jamaa anaekuuzia alinunua kiwanja cha mtu mwingine kwa hio ni kama anataka arushie mtu janga asepe.

Kuna sehemu tena, jamaa ana burgain bei na mimi bei kumbe kiwanja sio chake, ni cha mdogo wake, baadae baada ya kumchimba eti ndio ananiambia sio chake. Kwa hio ina maana bei aliotaka kupatana na mimi ilikuwa kaeka commission yake juu.

KUWENI MAKINI.
Chadema acheni Utapeli
 
Bei zimepunguzwa
 
Kuna hivi vinavyotangazwa kila kukicha kwenye maredio vinapatikana mlandizi, bagamoyo, sijui kigamboni na inasemwa ni bei ya chini sana, je uhalali wake upo vipi???

Mwenye taarifa au uzoefu na hili atujuze.
Mlandizi njia ya kutokea bagamoyo ile wengi walinunua kama mashamba. Baadae mkoa wa pwani wakasema yale maeneo sio mashamba bali ni maeneo ya mji kimkakati hivo yakapimwa kwa viwanja. Ukipata mtu sahihi kule ni fursa sio muda kunajaa mana bandari ya bwagamoyo ikianza tu, kazi kwisha....watu wazito kadhaa ikiwemo maaskofu wana maekari kule sio poa kabisaa
 
Mimi mimeshakuwa dalali kwa miaka mingi najua A to Z kuhusu utapeli wa viwanja kuna mtu apo juu nimemsikia anasema kiwanja kizuri ni kile chenye hati nakupa hii chukua ...ishu ya utapeli wa viwanja mgao unaenda adi wizarani yani utapigwa na hati yako mkononi unayo na cha kufanya huna..
Hajawai kukutana na double allocations za hati.

Kiwanja kimoja kina hati tatu zenye wamiliki tofauti na zote zimetolewa na manispaa ama wizara ya ardhi

Double allocation zinatokea kwasababu ya Rushwa tu kwa maofisa wa Ardhi/Manispaa/Halmashauri husika ,mara nyingi inatokea kwamba kiwanja kishauzwa au kashapewa mtu mwingine ,akija mtu mwenye nguvu anakitaka basi watu wa ardhi/manispaa/halmashauri wanampa huyo mtu mwingine wakitegemea akija kulalamika wanampatia sehemu nyingine mmiliki wa awali.

Hapa mmiliki wa awali hawezi kutapeliwa labda akubali na yeye kuhongwa ili apelekwe sehemu nyingine ila akikaza fuvu hawezi kuondolewa.

Mara nyingi viwanja vya kupimwa matapeli wakija wanayaondoa mawe halafu wanauza kama skwata wakishirikiana na watu wa serikali za mitaa ila hivi wanaomizwa ni hao wateja na si mmiliki.
 
Mimi mimeshakuwa dalali kwa miaka mingi najua A to Z kuhusu utapeli wa viwanja kuna mtu apo juu nimemsikia anasema kiwanja kizuri ni kile chenye hati nakupa hii chukua ...ishu ya utapeli wa viwanja mgao unaenda adi wizarani yani utapigwa na hati yako mkononi unayo na cha kufanya huna..
Je nini kifanyike, ili mnunuzi awe salama?
 
Mmh nakushangaa utaanza je process ya transfer kabla ya kulipia hicho kiwanja, unafikiri mchakato wa transfer ni siku mbili au wiki ata miezi sita inaisha transifer bado.......
Point yangu ni kwamba kama una akili timamu lazima uende wizarani kujiridhisha kuwa hati ni safi haina makando kando
Hati kuchukulia six months ni uzembe wako tuu ukijiongeza haiwez chukua muda wote huo
 
Ikugharimu 500k tu wewe unatania kama sehemu haina mchoro wa wizara huo mchoro tu ni zaidi ya 3m upelekwe wizarani kufanyiwa approval ambao sio chini ya miezi sita kwasbb na yenyewe ina process zake pia, mchoro ulirudi ndo uanze ku- process hati yako umlipe saviour sio chini ya 300k ulipia na kodi za TRA na za almashauri ili upate hiyo hati sio mchozo.
Kumbe unaelewa mziki wa kuipata hati , sasa iweke mtu mwneye hati miliki atapeliwe kiwanja?
 
Double allocation zinatokea kwasababu ya Rushwa tu kwa maofisa wa Ardhi/Manispaa/Halmashauri husika ,mara nyingi inatokea kwamba kiwanja kishauzwa au kashapewa mtu mwingine ,akija mtu mwenye nguvu anakitaka basi watu wa ardhi/manispaa/halmashauri wanampa huyo mtu mwingine wakitegemea akija kulalamika wanampatia sehemu nyingine mmiliki wa awali.

Hapa mmiliki wa awali hawezi kutapeliwa labda akubali na yeye kuhongwa ili apelekwe sehemu nyingine ila akikaza fuvu hawezi kuondolewa.

Mara nyingi viwanja vya kupimwa matapeli wakija wanayaondoa mawe halafu wanauza kama skwata wakishirikiana na watu wa serikali za mitaa ila hivi wanaomizwa ni hao wateja na si mmiliki.
We ndo umeongea jambo la msingi
 
Pesa, Ardhi na Mapenzi.

Hivi ni vitu vilivyo mwaga damu sana, vilivyo karibisha ushetani, vilvyo vunja utu na vilivyo tengeneza uhasama mkubwa sana.

Lakini bado ni vitu vyenye thamani kuliko vitu vyote.

Unapotafuta kiwanja, inabidi uwekeze zaidi katika umakini na upelelezi.

Kuna sehemu nilipata kiwanja, jamaa akawa tayari kuniuzia, lakini kumbe nyuma ya pazia kile kiwanja ni urithi wa watoto wa kaka yake yani baada ya kaka yao kufariki na barua zipo. Yeye akawa amepewa cha nyuma yake ila yeye anang'ang'ania pote.

Kuna sehemu nilipata kiwanja, jamaa akawa ananihakikishia kabisa kuwa hakuna tabu na hadi majirani zake (kabila moja) pale wakawa wanachochea. Lakini kwa bahati nzuri kuna afisa ardhi anaishi pembeni na anamjua mshikaji wangu niliekuwa nae, akatuita pembeni na kuniambia kuwa hapo pana mgogoro jamaa anaekuuzia alinunua kiwanja cha mtu mwingine kwa hio ni kama anataka arushie mtu janga asepe.

Kuna sehemu tena, jamaa ana burgain bei na mimi bei kumbe kiwanja sio chake, ni cha mdogo wake, baadae baada ya kumchimba eti ndio ananiambia sio chake. Kwa hio ina maana bei aliotaka kupatana na mimi ilikuwa kaeka commission yake juu.

KUWENI MAKINI.
Acheni ubahili na ujuaji.

Tafuta Wakili, mlipe akufanyie "conveyancing".

Ukishamlipa wakili atahakikisha unanua kiwanja/nyumba ambayo iko salama kwa kuanza kukufanyia 'official search' (upekuzi wa usalama wa ardhi hiyo kwenye masijala ya ardhi katika eneo husika), mpaka kukuandikia mkataba wa mauziano (au kuhakiki mkataba wa mauziano utakaoletewa).

Wengi wenu kwa ubahili au ujuaji, mnajikuta mnanunua ardhi/nyumba ambazo sio mali halali za wauzaji, au ardhi/nyumba ambazo zimekopewa benki n.k

Nikupe mfano, marafiki wawili waliosoma pamoja walitaka kununua nyumba za ghorofa karibu karibu. Nyumba zikapatikana. Mmoja akatafuta wakili akamlipa amfanyie "conveyancing" from stage A to Z, akamlipa 2M.

Wa pili akaona ile 2M ni pesa nyingi, akaenda kununua hivyohivyo. Baada ya kusaini mkataba na kuhamia, akagundua kwamba ule mkataba wa mauziano alioletewa ulikuwa na "exclusion clause", this is a clause limiting liability to the drawer (drafter of the contract).

Baada ya kuhamiwa akaletewa bili ya maji na umeme jumla 3.2M. Alipomfata muuzaji ili alipe akakataa, akasema haikuwa sehemu ya makubaliano. Kwenda kwa Mwanasheria akaambiwa hivyohivyo, kwasababu mkataba uliandikwa "nyumba inauzwa kama ilivyo". Lakini angemlipa Wakili basi angeongeza clause kwamba "madeni yote yanayohusu nyumba hiyo kabla ya mauziano yalipwe na muuzaji".

Kwahiyo acheni ubahili na ujuaji muepuke hasara zisizo za lazima [emoji28]
 
Point yangu ni kwamba kama una akili timamu lazima uende wizarani kujiridhisha kuwa hati ni safi haina makando kando
Hati kuchukulia six months ni uzembe wako tuu ukijiongeza haiwez chukua muda wote huo
Sawa na kuelewa ila ukienda wizara nakuwapa number ya hati wata isashi na kuonekana ni sahihi, kumbuka hiyo ilio nao mkonono ni duplicate sio original kwa hiyo haitakua na shida utaridhika, siku ya kubadili itakubidi uwape hiyo ndo wakutegenezee mpya ndo utagundua hiyo ni dup na ulishamlipa pesa kitambo, sijui umenisoma?
 
Back
Top Bottom