Utafutaji wa kiwanja umenifanya nielewe mwanadamu ni hatari sana

Yalishawahi kunikuta haya mambo ya viwanja.

 
Anotaka kiwanja kwa upande wa Zanzibar maeneo ya njia ya Fumba anitafute

Ni muaminifu sina haja ya kumtapeli mtu maisha mafupi sana haya
Nb.ata ukiwa mtu wa bara usisikilize maneno ya mtandaoni njoo ununue kiwanja na unauziwa fresh
 
Kuna watu ni mafala sana wacha wapigwe tu.
Kuna mstaafu alinipigia anataka kiwanja akaja kukiona akakipenda akaomba aje alipie kesho yake.
Siku anakuja kulipia kafika gongo la Mboto kakuta spika linatangaza biashara ya viwanja chap kachukua namba kawapigia, wakamchangamkia Fasta wakampeleka site wakamuonesha maeneo akachagua akalipa milioni tatu cash. Majirani wamchongo, mjumbe wa mchango, mwenyekiti wamchongo.
Baada ya siku mbili anaenda site anakuta kiwanja kina tofari na ujenzi unaendelea.
Anatoa karatasi lake la mauziano hakuna hata mmoja anayetambulika kwenye mtaa ule. Kuanzia muuzaji hadi viongozi wa serekali ya mtaa.
Nadhani huwa wanapuliziwa.
 
Tembea Uone
Ndugu yangu alitaka eneo na nna rafiki alikua na kiwanja chake mbezi beach upande wa st mary’ tukaenda kulicheki
Alikua hajenda kama mwaka

Unajua kilichochotokea, tumekuta kimejengwa ghorofa nne wapo wanafanya skimming, ujenzi una miez sita mwenyew yupo ulaya huko

Ana hati ya miaka mitano, wakat yule rafik, yake tangu 2005, hizo beacon zinasoma tofauti kidogo yan mbele ya like jiwe la kwanza. Na alokua jiran pale ndo aliuza akahama
 
Sahihi, vinginevyo utakuwa unafanya mambo at your own risk
 
Ikawaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…