Utafutaji wa kiwanja umenifanya nielewe mwanadamu ni hatari sana

Utafutaji wa kiwanja umenifanya nielewe mwanadamu ni hatari sana

Yalishawahi kunikuta haya mambo ya viwanja.

 
Anotaka kiwanja kwa upande wa Zanzibar maeneo ya njia ya Fumba anitafute

Ni muaminifu sina haja ya kumtapeli mtu maisha mafupi sana haya
Nb.ata ukiwa mtu wa bara usisikilize maneno ya mtandaoni njoo ununue kiwanja na unauziwa fresh
 
Kuna watu ni mafala sana wacha wapigwe tu.
Kuna mstaafu alinipigia anataka kiwanja akaja kukiona akakipenda akaomba aje alipie kesho yake.
Siku anakuja kulipia kafika gongo la Mboto kakuta spika linatangaza biashara ya viwanja chap kachukua namba kawapigia, wakamchangamkia Fasta wakampeleka site wakamuonesha maeneo akachagua akalipa milioni tatu cash. Majirani wamchongo, mjumbe wa mchango, mwenyekiti wamchongo.
Baada ya siku mbili anaenda site anakuta kiwanja kina tofari na ujenzi unaendelea.
Anatoa karatasi lake la mauziano hakuna hata mmoja anayetambulika kwenye mtaa ule. Kuanzia muuzaji hadi viongozi wa serekali ya mtaa.
Nadhani huwa wanapuliziwa.
 
Hayo mnayoyasema inawezekana ikawa ni kweli ,Lakini sijawahi kuskia mtu akilalamika ametapeliwa kiwanja na ana Hati miliki ya wizara ya hicho kiwanja

Kwa Dunia ya Leo kama hao watu wengekuepo wangesha share experience yao

Kuhusu utoaji wa Hati miliki ya wizara , Mansipaa na halimashauri zinazingatia vitu vingi

Kuna zile cordinate point za beacons ambazo zinazunguka kiwanja ,zile ndo zinatambulisha mipaka halisi ya kiwanja

Ukiachana na hilo kuna hili la kuweka jina la mmliki kwenye ramani ya mipango mji

Kuna swala la Nida

Haya yote yafanyike alafu Bado kiwanja kimoja kitolewe hati tatu kwa wakati mmoja?


Basi tutakua na serikali ya hovyo sana


Me nna amini hilo haliwezi kutokea


Niwape mfano rahisi ,hili sakata linaloendeles kule bagamoyo makurunge baina ya serikali ya Zanzibar na watu walionunua kule , Serikali ya Zanzibar hawakua na Hati miliki ndo maana waliouziwa pale waliweza kufanikisha mpaka mchakato wa Hati miliki kutoka wizarani


Msichukulie mambo kirahisi hvyo

Kama kuna mtu ambaye ameshawai kutapeliwa kiwanja akiwa na Hati miliki ya wizarani aje hapa atupe hicho kisa chake
Tembea Uone
Ndugu yangu alitaka eneo na nna rafiki alikua na kiwanja chake mbezi beach upande wa st mary’ tukaenda kulicheki
Alikua hajenda kama mwaka

Unajua kilichochotokea, tumekuta kimejengwa ghorofa nne wapo wanafanya skimming, ujenzi una miez sita mwenyew yupo ulaya huko

Ana hati ya miaka mitano, wakat yule rafik, yake tangu 2005, hizo beacon zinasoma tofauti kidogo yan mbele ya like jiwe la kwanza. Na alokua jiran pale ndo aliuza akahama
 
Kuna Umuhimu sana wa kuwa na Hati miliki kutoka wizarani kwa kiwanja unacho miliki
Watu wengi wamezoea kununua viwanja kizamani ,ile ya kwenda kwa m/kiti au mjumbe kusainishana haitoshi inabidi watu wajiongeze
.kwa Kila kiwanja unachotaka kununua uhakikishe

Kimepimwa

Kuna ramani ya mipango mji eneo husika

Ikitokea unauziwa na mtu binafsi ni muhimu sana hicho kiwanja kiwe na Hati miliki kutoka wizarani ,kama hakina hiyo aliyekuuzia akupe ushirkiano kufanya mchakato wa Hati miliki ya wizarani

Note:
Ni muhimu sana
Sahihi, vinginevyo utakuwa unafanya mambo at your own risk
 
Tembea Uone
Ndugu yangu alitaka eneo na nna rafiki alikua na kiwanja chake mbezi beach upande wa st mary’ tukaenda kulicheki
Alikua hajenda kama mwaka

Unajua kilichochotokea, tumekuta kimejengwa ghorofa nne wapo wanafanya skimming, ujenzi una miez sita mwenyew yupo ulaya huko

Ana hati ya miaka mitano, wakat yule rafik, yake tangu 2005, hizo beacon zinasoma tofauti kidogo yan mbele ya like jiwe la kwanza. Na alokua jiran pale ndo aliuza akahama
Ikawaje
 
Back
Top Bottom