Utajiri upo katika kilimo bora cha mpunga, chukua nondo hizi

Utajiri upo katika kilimo bora cha mpunga, chukua nondo hizi

Siri moja naweza kukwambia ni huwezi kuwa mkulima na msambazaji kwa wakati m'moja lazima uchague moja. Uwe mkulima uuzie wafanya biashara au uwe mfanyabiashara ununue kwa wakulima.

Chagua moja kama unataka kuiona faida.
Ni muhimu kuzingatia machaguzi ya njia moja ili ufanikiwe vizur
 
Vipi kwa mtu anaye taka kununua mpunga na kuja kuuza ?
Hainashida ni chaguo lako unaweza kwenda shambani kwa mkulima ukanunua gunia la mpunga la Kuanzia kilo 100 ukasafirisha mjini kukoboa Kwa gredi nzuri wew unauza/na kusambaza mchele kwenye masoko Na maduka makubwa Kwa Oda,ukiwa unapata oda nyingi xenye mzunguuko ni biashara inayolipa vizuri Sana.
 
Ushukuru haujakutana na KIMYANGA na Mafuriko mimi mwaka huu heka 40 zote zimeenda na maji....
Daa Pole Sana Ndg Hizo ni changamoto za kilimo ila usikate tamaa huku wenyewe pia tulipgwa na ugonjwa wa Manjano,pamoja na miche kunyauka yenyewe Yaani kila dawa unayopga haifui dafu Ila kwa sasa tumepata dawa ya kudhibiti Manjano inaitwa Byajuta inasaidia so tupambane
 
Halina akili hilo achana nalo,mm ni mkulima mkuu nakuelewa haswa,harafu kuna upumbavu nauoaga humu yaan mtu akiwa na jambo la maana anataka ku-share basi wapumbavu kama hao hawakosekani.

Harafu mtu huyohuyo anaweza kutoa mfano nchi kama Bangladesh wanafanikiwa vipi kwenye kilimo wakati sisi tunashindwa,na ukija humu mtu huyohuyo anaona kama unataka kuwaingiza watu chaka.

KUNA MUDA NASEMAGA TUNASOMA ILA ELIMU ZETU HAZINA MSAADA WOWOTE.
Kabisa mkuu bila sisi wakulima kushare ujuzi pamoja na changamoto tunazokumbana nazo tutachelewa kufanikiwa kupitia kilimo tunapaswa tuwe updates kila wakati Ndg
 
KILIMO BORA CHA MPUNGA:
A: kuandaa shamba
  • shamba lilimwe vizur na kusawazishwa liwe level (Hallow)
  • Piga dawa ya magugu kabla ya kupanda Kama Bafoseti
  • weka mifereji ya Maji vizuvizur
  • Andaa majaruba mapema yawe level kupitika Kwa maji
B: UANDAAJI WA MBEGU NA KUPANDA
  • Kwa kilimo Cha nchi kavu kwenye miinuko andaa Mbegu kama,BAROKA,TUMAINI,PATO,FARAJA,WAB zinahimili magojwa na ukame kwenye hekta Moja Tumia kilo 80 au ekari Moja debe mbili,Unaweza mwaga Kwa mistari au zigi zaga
  • Kwa kilimo Cha umwagiliaji kwanza andaa Mbegu kama SARO 5,KOMBOKA,TAI,TARIKI,SUPA
  • Andaa kitalu Cha mita 5 Kwa 20 tuta
  • Loweka Mbegu Kwa siku tatu Kisha kasie kwenye kitalu
  • Mbegu itakaa kwenye kitalu Kwa muda wa Siku 21-28 hamisha kwenye majaruba Ukiwa Tayar ushachavyanga na kupiga dawa ya kuua magugu
  • Panda Kwa mistari mche Hadi mche ni sm 15 Kwa sm15
  • Miche 2-3 kw Shina Moja pandikiza Kwa kamba
C: UWEKAJI WA MBOLEA
- Mbolea ya kupandia kama DAP.,NPK ,MINJINGU kilo 40 Kwa ekari moja
zinasaidia kutoa mizizi na pacha
- Mbolea ya kukuzia Kuna nyakati Mbili
(1) Wakati wa kupacha hii unaweza MBOLEA siku 14 baada ya kupandikiza UREA ,SA, CAN
(2) Wakati wa mimba dume hii siku 25 kabla ya kuchanua UREA,SA inasaidia ujazo wa punje na uzito

D: PALIZI
-Ni muhimu shamba lipaliliwe Kuanzia siku 16 mpaka 24 tangu kupandikiza au kumwagwa
-kuna Njia tatu za PALIZI
(1) Kutumia mashine ya palizi
(2) Kungolea Kwa mkono
(3) Kutumia viatilifu vya kuua wadudu kama PILAR SPIRIT 167 OD,RICE CLEAR 100SC,PILARILO 500EC

E: MAGONJWA
  • Ukungu,mabaka baka,mnyauko wa majani,kimnyangaa, Kuwepo Kwa funza weupe
  • Tiba kung'oa mimea iliyoathiliwa, Nyunyiza dawa kama THIODEN,ENDOSULFET,FETHIONI Kila baada ya wiki Mbili ikiambatana na MBOLEA za Busta kama SUPER GLOW, FINCH NK
F: ULINZI NA MAVUNO
  • Ni muhimu kulinda ndega mapema pindi mpunga unapoanza kuchanua mpaka kuvuna
  • Ni muhimu kuwahi kuvuna usiuachie ukauke Sana mpaka upukutike shambani.
KILIMO CHA MPUNGA NI UTAJIRI MKUBWA USIO NA KIFANI MKAWE NA MAANDALIZI MEMA
BY MHINA JR
Naunga mkono hoja
 
Mwaka huu mwishoni na mimi nitalima angalau ekari mbili, primarily kwa ajili ya chakula Cha familia. By the way mwaka huu Sengerema mpunga umekubali sana, wasingekuwa waganda tungeupikia ugali.
 
KILIMO BORA CHA MPUNGA:
A: kuandaa shamba
  • shamba lilimwe vizur na kusawazishwa liwe level (Hallow)
  • Piga dawa ya magugu kabla ya kupanda Kama Bafoseti
  • weka mifereji ya Maji vizuvizur
  • Andaa majaruba mapema yawe level kupitika Kwa maji
B: UANDAAJI WA MBEGU NA KUPANDA
  • Kwa kilimo Cha nchi kavu kwenye miinuko andaa Mbegu kama,BAROKA,TUMAINI,PATO,FARAJA,WAB zinahimili magojwa na ukame kwenye hekta Moja Tumia kilo 80 au ekari Moja debe mbili,Unaweza mwaga Kwa mistari au zigi zaga
  • Kwa kilimo Cha umwagiliaji kwanza andaa Mbegu kama SARO 5,KOMBOKA,TAI,TARIKI,SUPA
  • Andaa kitalu Cha mita 5 Kwa 20 tuta
  • Loweka Mbegu Kwa siku tatu Kisha kasie kwenye kitalu
  • Mbegu itakaa kwenye kitalu Kwa muda wa Siku 21-28 hamisha kwenye majaruba Ukiwa Tayar ushachavyanga na kupiga dawa ya kuua magugu
  • Panda Kwa mistari mche Hadi mche ni sm 15 Kwa sm15
  • Miche 2-3 kw Shina Moja pandikiza Kwa kamba
C: UWEKAJI WA MBOLEA
- Mbolea ya kupandia kama DAP.,NPK ,MINJINGU kilo 40 Kwa ekari moja
zinasaidia kutoa mizizi na pacha
- Mbolea ya kukuzia Kuna nyakati Mbili
(1) Wakati wa kupacha hii unaweza MBOLEA siku 14 baada ya kupandikiza UREA ,SA, CAN
(2) Wakati wa mimba dume hii siku 25 kabla ya kuchanua UREA,SA inasaidia ujazo wa punje na uzito

D: PALIZI
-Ni muhimu shamba lipaliliwe Kuanzia siku 16 mpaka 24 tangu kupandikiza au kumwagwa
-kuna Njia tatu za PALIZI
(1) Kutumia mashine ya palizi
(2) Kungolea Kwa mkono
(3) Kutumia viatilifu vya kuua wadudu kama PILAR SPIRIT 167 OD,RICE CLEAR 100SC,PILARILO 500EC

E: MAGONJWA
  • Ukungu,mabaka baka,mnyauko wa majani,kimnyangaa, Kuwepo Kwa funza weupe
  • Tiba kung'oa mimea iliyoathiliwa, Nyunyiza dawa kama THIODEN,ENDOSULFET,FETHIONI Kila baada ya wiki Mbili ikiambatana na MBOLEA za Busta kama SUPER GLOW, FINCH NK
F: ULINZI NA MAVUNO
  • Ni muhimu kulinda ndega mapema pindi mpunga unapoanza kuchanua mpaka kuvuna
  • Ni muhimu kuwahi kuvuna usiuachie ukauke Sana mpaka upukutike shambani.
KILIMO CHA MPUNGA NI UTAJIRI MKUBWA USIO NA KIFANI MKAWE NA MAANDALIZI MEMA
BY MHINA JR
Kilimo cha Mpunga ni kigumu mno. Yaani kina risks za kutosha upande wa maji na jua kali. Maji yakiwa mengi sana yakasababisha mafuriko na mpunga ukizama ujue umeliwa. Jua likiwa kali sana ujue umeliwa pia. Muhimu ni kutumia umwagiliaji ndio suluhisho pekee. Binafsi huwa nalima kwa ajili ya kujikimu mimi mwenyewe na familia yangu na kuuza pia.
 
Vipi msimu huu mvua hazijaathiri kilimo cha mpunga?
Mwaka huu kilimo cha mpunga kimeathirika sana katika maeneo ya mabonde, mfano Kyela. Aidha, kwa upande wa maeneo ambayo huwa hayapati mvua za kutosha mavuno yamekuwa vizuri mwaka huu,, mfano Tunduma.
 
Siri moja naweza kukwambia ni huwezi kuwa mkulima na msambazaji kwa wakati m'moja lazima uchague moja. Uwe mkulima uuzie wafanya biashara au uwe mfanyabiashara ununue kwa wakulima.

Chagua moja kama unataka kuiona faida.
Kwa kilimo cha mpunga namshauri awe msambazaji anayenunua kwa wakulima.
 
Wastani gunia 40 Mpaka 50
Yaani kwamba heka Moja ya Mpunga inatoa gunia 40 hadi 50???

Mimi ni Suka na nimelima sana mwaka 2015-2017. Mashamba ya mpunga duthumi- na Mlimba morogoro.

Heka moja ikikubali inatoa wastani wa gunia 7-10 za mpunga na si zaidi ya hapo!!.
 
Tatizo unalima kienyeji, jaribu kutumia mbegu ya saro 5 then weka hata mifuko 2 ya mbolea unaweza kuona tofauti
 
Update Bado tunaendelea na mapambano ya zao la mpunga mpaka Sasa tunakaribia kuanza kulinda maana 80% ushaweka mimba za kutosha ingawa umepetia changamoto kadhaa kama baadhi ya ndiwa unavyoonekana ila maendeleo mazuri Kuanzia Kesho tunapga booster za mwisho.
 
Attachments

  • IMG_20240804_091216.jpg
    IMG_20240804_091216.jpg
    1.9 MB · Views: 23
  • IMG_20240804_091209.jpg
    IMG_20240804_091209.jpg
    2.5 MB · Views: 21
  • IMG_20240804_091152.jpg
    IMG_20240804_091152.jpg
    2.5 MB · Views: 22
  • IMG_20240804_091147.jpg
    IMG_20240804_091147.jpg
    2.5 MB · Views: 24
  • IMG_20240804_090947.jpg
    IMG_20240804_090947.jpg
    2.8 MB · Views: 22
  • IMG_20240804_090943.jpg
    IMG_20240804_090943.jpg
    1.9 MB · Views: 22
  • IMG_20240804_090920.jpg
    IMG_20240804_090920.jpg
    2.4 MB · Views: 20
  • IMG_20240804_090916.jpg
    IMG_20240804_090916.jpg
    2.9 MB · Views: 20
  • IMG_20240804_085948.jpg
    IMG_20240804_085948.jpg
    2.6 MB · Views: 17
  • IMG_20240804_085942.jpg
    IMG_20240804_085942.jpg
    2.3 MB · Views: 16
  • IMG_20240804_085930.jpg
    IMG_20240804_085930.jpg
    3.3 MB · Views: 17
  • IMG_20240804_085836.jpg
    IMG_20240804_085836.jpg
    3 MB · Views: 18
  • IMG_20240804_085427.jpg
    IMG_20240804_085427.jpg
    2.6 MB · Views: 14
  • IMG_20240804_085705.jpg
    IMG_20240804_085705.jpg
    3.2 MB · Views: 15
  • IMG_20240804_085709.jpg
    IMG_20240804_085709.jpg
    2.8 MB · Views: 13
  • IMG_20240804_085749.jpg
    IMG_20240804_085749.jpg
    2.5 MB · Views: 13
  • IMG_20240804_085744.jpg
    IMG_20240804_085744.jpg
    2.6 MB · Views: 13
  • IMG_20240804_090950.jpg
    IMG_20240804_090950.jpg
    2.4 MB · Views: 14
  • IMG_20240804_091051.jpg
    IMG_20240804_091051.jpg
    2.8 MB · Views: 15
  • IMG_20240804_091137.jpg
    IMG_20240804_091137.jpg
    2.7 MB · Views: 22
Ni kilimo cha kumwagilia?

Back
Top Bottom