Utajiri upo katika kilimo bora cha mpunga, chukua nondo hizi

Siri moja naweza kukwambia ni huwezi kuwa mkulima na msambazaji kwa wakati m'moja lazima uchague moja. Uwe mkulima uuzie wafanya biashara au uwe mfanyabiashara ununue kwa wakulima.

Chagua moja kama unataka kuiona faida.
Ni muhimu kuzingatia machaguzi ya njia moja ili ufanikiwe vizur
 
Vipi kwa mtu anaye taka kununua mpunga na kuja kuuza ?
Hainashida ni chaguo lako unaweza kwenda shambani kwa mkulima ukanunua gunia la mpunga la Kuanzia kilo 100 ukasafirisha mjini kukoboa Kwa gredi nzuri wew unauza/na kusambaza mchele kwenye masoko Na maduka makubwa Kwa Oda,ukiwa unapata oda nyingi xenye mzunguuko ni biashara inayolipa vizuri Sana.
 
Ushukuru haujakutana na KIMYANGA na Mafuriko mimi mwaka huu heka 40 zote zimeenda na maji....
Daa Pole Sana Ndg Hizo ni changamoto za kilimo ila usikate tamaa huku wenyewe pia tulipgwa na ugonjwa wa Manjano,pamoja na miche kunyauka yenyewe Yaani kila dawa unayopga haifui dafu Ila kwa sasa tumepata dawa ya kudhibiti Manjano inaitwa Byajuta inasaidia so tupambane
 
Kabisa mkuu bila sisi wakulima kushare ujuzi pamoja na changamoto tunazokumbana nazo tutachelewa kufanikiwa kupitia kilimo tunapaswa tuwe updates kila wakati Ndg
 
Naunga mkono hoja
 
Mwaka huu mwishoni na mimi nitalima angalau ekari mbili, primarily kwa ajili ya chakula Cha familia. By the way mwaka huu Sengerema mpunga umekubali sana, wasingekuwa waganda tungeupikia ugali.
 
Kilimo cha Mpunga ni kigumu mno. Yaani kina risks za kutosha upande wa maji na jua kali. Maji yakiwa mengi sana yakasababisha mafuriko na mpunga ukizama ujue umeliwa. Jua likiwa kali sana ujue umeliwa pia. Muhimu ni kutumia umwagiliaji ndio suluhisho pekee. Binafsi huwa nalima kwa ajili ya kujikimu mimi mwenyewe na familia yangu na kuuza pia.
 
Vipi msimu huu mvua hazijaathiri kilimo cha mpunga?
Mwaka huu kilimo cha mpunga kimeathirika sana katika maeneo ya mabonde, mfano Kyela. Aidha, kwa upande wa maeneo ambayo huwa hayapati mvua za kutosha mavuno yamekuwa vizuri mwaka huu,, mfano Tunduma.
 
Siri moja naweza kukwambia ni huwezi kuwa mkulima na msambazaji kwa wakati m'moja lazima uchague moja. Uwe mkulima uuzie wafanya biashara au uwe mfanyabiashara ununue kwa wakulima.

Chagua moja kama unataka kuiona faida.
Kwa kilimo cha mpunga namshauri awe msambazaji anayenunua kwa wakulima.
 
Wastani gunia 40 Mpaka 50
Yaani kwamba heka Moja ya Mpunga inatoa gunia 40 hadi 50???

Mimi ni Suka na nimelima sana mwaka 2015-2017. Mashamba ya mpunga duthumi- na Mlimba morogoro.

Heka moja ikikubali inatoa wastani wa gunia 7-10 za mpunga na si zaidi ya hapo!!.
 
Yaani kwamba heka Moja ya Mpunga inatoa gunia 40 hadi 50???

Mimi ni Suka na nimelima sana mwaka 2015-2017. Mashamba ya mpunga duthumi- na Mlimba morogoro.

Heka moja ikikubali inatoa wastani wa gunia 7-10 za mpunga na si zaidi ya hapo!!.
Tatizo unalima kienyeji, jaribu kutumia mbegu ya saro 5 then weka hata mifuko 2 ya mbolea unaweza kuona tofauti
 
Update Bado tunaendelea na mapambano ya zao la mpunga mpaka Sasa tunakaribia kuanza kulinda maana 80% ushaweka mimba za kutosha ingawa umepetia changamoto kadhaa kama baadhi ya ndiwa unavyoonekana ila maendeleo mazuri Kuanzia Kesho tunapga booster za mwisho.
 

Attachments

  • IMG_20240804_091216.jpg
    1.9 MB · Views: 23
  • IMG_20240804_091209.jpg
    2.5 MB · Views: 21
  • IMG_20240804_091152.jpg
    2.5 MB · Views: 22
  • IMG_20240804_091147.jpg
    2.5 MB · Views: 24
  • IMG_20240804_090947.jpg
    2.8 MB · Views: 22
  • IMG_20240804_090943.jpg
    1.9 MB · Views: 22
  • IMG_20240804_090920.jpg
    2.4 MB · Views: 20
  • IMG_20240804_090916.jpg
    2.9 MB · Views: 20
  • IMG_20240804_085948.jpg
    2.6 MB · Views: 17
  • IMG_20240804_085942.jpg
    2.3 MB · Views: 16
  • IMG_20240804_085930.jpg
    3.3 MB · Views: 17
  • IMG_20240804_085836.jpg
    3 MB · Views: 18
  • IMG_20240804_085427.jpg
    2.6 MB · Views: 14
  • IMG_20240804_085705.jpg
    3.2 MB · Views: 15
  • IMG_20240804_085709.jpg
    2.8 MB · Views: 13
  • IMG_20240804_085749.jpg
    2.5 MB · Views: 13
  • IMG_20240804_085744.jpg
    2.6 MB · Views: 13
  • IMG_20240804_090950.jpg
    2.4 MB · Views: 14
  • IMG_20240804_091051.jpg
    2.8 MB · Views: 15
  • IMG_20240804_091137.jpg
    2.7 MB · Views: 22
Ni kilimo cha kumwagilia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…