Utajiri wa Apple Inc. ni mkubwa kuliko GDP ya Afrika

Utajiri wa Apple Inc. ni mkubwa kuliko GDP ya Afrika

Wamewazidi hata bara la Australia mkuu usituonee Waafrica.

Pia wameuzidi uchumi wa Russia, Brazil, Canada, South Korea, Mexico, Italy, Spain na France...kifo cha wengi harusi😅😅😅

Kama kampuni ya Apple ingekuwa nchi ingekuwa ya 6 kwa uchumi mkubwa duniani ikitanguliwa na U.S.A, China, Japan, Germany, U.K kwa mtawalia
Uchambuzi mujarab kama huu vijana wajinga wajinga kama mtoa post hawawezi kuu comprehend!
 
Afadhali kuzizidi baadhi ya nchi za ulaya kuliko kuzidi bara zima, inatia huzuni
Wamewazidi hata bara la Australia mkuu usituonee Waafrica.

Pia wameuzidi uchumi wa Russia, Brazil, Canada, South Korea, Mexico, Italy, Spain na France...kifo cha wengi harusi[emoji28][emoji28][emoji28]

Kama kampuni ya Apple ingekuwa nchi ingekuwa ya 6 kwa uchumi mkubwa duniani ikitanguliwa na U.S.A, China, Japan, Germany, U.K kwa mtawalia
 
Show off tu, mtu anakwambia iPhone ipo secured ukimuuliza anatunza siri gani nzito kwenye simu? Jibu hana
Sasa kama mnadharau tecno ya laki tatu mnakimbilia iPhone ya mil3 , lakni mostly matumizi ni Yale Yale , tumepandikiziwa mentality ya ajabu Sana , wacha tu hao aple wapige pesa
 
Utajiri wa kweli ni haki, amani na furaha binafsi ya mtu anavyovipata kupitia Roho Mtakatifu. Haya, linapokuja kwenye mambo ya msingi kama hayo mtu mtu anayemiliki au kufanya kazi Apple anaweza kuwa maskini sana kuliko yule anayemiliki au kufanya kazi kwenye genge la matunda chini ya mwembe.

Omba Mungu akunyime vyote lakini akupe utajiri wa vya rohoni.
Mkuu acha kijiliwaza kwa maneno ya kimasikini .Piga kazi uwe TAJIRI kumbuka umasikini ni LAANA,kumbuka pia katika watu wa MUNGU wenye Imani kubwa I mean Mababa wa Imani akina IBRAHIM,ISAKA NA YAKOBO,DAUDI na mwanae MFalme SELEMANI walikua matajiri wakubwa Sana.Kumbuka MWENYEZI MUNGU haupendi umasikini kwa Sababu ndo chanzo Cha dhambi.
 
Utajiri ni Pesa ?

Na Rutuba, Mazao, Maziwa, Bahari na Mito yenye chakula mfano samaki ni umasikini ? Kwahio nchi ni Tajiri kutokana na kuwa na Rasilimali Watu na Ardhi (Real Estate) hii iwe kesho, au keshokutwa bado itakuwa valuable sababu ndio source of wealthy..... Ni kama mgodi kutokuuvuna mgodi leo na kuondoa hizo dhahabu na kuzivaa haimaanishi hapo chini hakuna dhahabu....

Ngoja nikupe tu wazo Hivi unadhani ni fedha kiasi gani itabidi uzitoe ili uweze kumiliki tu sehemu kama Bariadi, Maswa au hata tuseme Timbuktu ? (Huwezi sababu hizi sehemu ni priceless)..., Ingawa Apple ukifika dau tu kwa Shareholders wanakupa chako na ku-shake your hand.....
Mkuu kwenye Ulimwengu wa Capitalism pesa ndo utajiri na sio ardhi .Ardhi ilikua utajiri kipndi Cha fudalism.Nakupa mfano,Leo hii tunajenga SGR na Nyerere hydropower je kwa nini tunakopa hela wakati tuna hiyo Ardhi,bahari,maziwa ,mito na mbuga za wanyama? Viongozi wetu Huwa wakienda Ulaya kutafuta wawekezaji si Huwa wanatafuta matajiri wenye hela ?DUNIA ya Leo mwenye hela ndo anaweza kufanya chochote kumbuka Hilo
 
Cash is the King sababu ya liquidity..., ni rahisi kujua value ya 100 USD haraka haraka kuliko gunia la maharage (huenda ni 5 USD, au 20USD) inategemea na demand and supply at the given time.... Ingawa vitu kama ardhi, maziwa, misitu their valuable kulingana na manufaa yake kwa jamii (Hata kama at a given time monetary value yake ukisema ni senti mbili) haibadilishi real value yake kama nguzo ya jamii.....

Unadhani kwanini ukienda kukopa popote unahitaji collateral ya kitu halisi...., Hizi FIAT Money ambazo Federal Reserves inaweza kuamua wakaingia kwenye makabrasha yao wakaprint za kutosha au kwa njia nyingine Pesa ambazo zinatengenezwa out of thin air (Yaani nchi yetu ikienda kukopa trillion kadhaa Benki inaissue hizo pesa out of thin air (At that Time Sio kwamba Benki inamiliki hizo Pesa binafsi..., na zinaongezeka / zinaongezwa tunaporudisha huo mkopo na riba (Yaani Creating Wealthy from Debt) In short hii hali sio sustainable na wala usishangae value za pesa kushuka na inflation na Boom and Bust Cycles ambazo haziishi....., Zamani Federal Reserves yoyote ilikuwa hairuhusiwi ku-print pesa zaidi ya Gold Reserves iliyonayo (leo hii ni uamuzi tu hata wakiamua kuingiza sokoni matrillions of money)....

In short the FIAT monetary system is DECI on Steroids......

Point ya pili ni kutokujua nguvukazi tuliyonayo sisi kama Taifa / Nchi..., wewe kwenda kujenga choo unaomba mkopo wa dollar wakati nguvu kazi za wazazi kujikusanya weekend moja tu wangeweza kuunganisha nguvu (matofari yapo, mchanga upo na mafundi wapo) sio kwamba inahitaji technical know how ya expert wa kulipwa in foreign currency.....
 
Utajiri wa kweli ni haki, amani na furaha binafsi ya mtu anavyovipata kupitia Roho Mtakatifu. Haya, linapokuja kwenye mambo ya msingi kama hayo mtu mtu anayemiliki au kufanya kazi Apple anaweza kuwa maskini sana kuliko yule anayemiliki au kufanya kazi kwenye genge la matunda chini ya mwembe.

Omba Mungu akunyime vyote lakini akupe utajiri wa vya rohoni.
Masikini ndiyo huwa nawapendea hapa. Hatukosagi maneno ya kujifariji
 
Masikini ndiyo huwa nawapendea hapa. Hatukosagi maneno ya kujifariji
Mkuu si kujifariji ni ukweli mtupu. Hebu chukua hata dakika moja kutafakari: hivi mtu tajiri kwelikweli kipesa ana kitu gani cha ziada ambacho mtu wa kawaida hana iwapo wote wana furaha, amani na wanaishi kwa haki?

Mnapenda sana kutukuza maisha ya kifahari bila sababu za msingi.
 
Mkuu acha kijiliwaza kwa maneno ya kimasikini .Piga kazi uwe TAJIRI kumbuka umasikini ni LAANA,kumbuka pia katika watu wa MUNGU wenye Imani kubwa I mean Mababa wa Imani akina IBRAHIM,ISAKA NA YAKOBO,DAUDI na mwanae MFalme SELEMANI walikua matajiri wakubwa Sana.Kumbuka MWENYEZI MUNGU haupendi umasikini kwa Sababu ndo chanzo Cha dhambi.
Watu wanaojielewa hawapigi kazi ili wawe matajiri. Utajiri hauwezi kuwa lengo au kusudi la maisha ya mtu duniani. Unaweza kuwa tajiri sana wa mali na bado ukawa maskini sana, huyo Steve Jobs wa Apple alifariki hata kabla ya muda (na kaliishi maisha yake yote kakiwa na stress na kukondeana) maana katika utajiri wake bado alikosa ridhiko la kweli. Pesa si kila kitu.
 
Long term wealthy na short time Partying.......

Unaweza ukatumia hizo resources ukakata miti yote.., ukavua samaki wote na mwisho wa siku wajukuu zako wakafa njaa (kwa ufujaji wako na kutokuwa sustainable)

Nchi ambayo ina asset ya ardhi hence inaweza kulima na kujilisha na kutumia hio miti kujenga kibanda cha malazi bila kusahau hata kuvaa ngovi ili kupata mavazi kamwe huwezi kuwaita ni masikini.... Hata kama wenyewe wameridhika wajukuu zao watakuwa na nyezo za kuweza kupata their basic needs.... Nakuacha na msemo wa Wahenga Red Indians..... (Huenda ndio ukajua true / real wealthy) na sio advertised marketed abstract so called utajiri...

When the last tree has been cut down, the last fish caught, the last river poisoned, only then will we realize that one cannot eat money.
Kukata miti kunaendana na kupanda miti.
 
Watu wanaojielewa hawapigi kazi ili wawe matajiri. Utajiri hauwezi kuwa lengo au kusudi la maisha ya mtu duniani. Unaweza kuwa tajiri sana wa mali na bado ukawa maskini sana, huyo Steve Jobs wa Apple alifariki hata kabla ya muda (na kaliishi maisha yake yote kakiwa na stress na kukondeana) maana katika utajiri wake bado alikosa ridhiko la kweli. Pesa si kila kitu.
Sijakuelewa hata unachokipinga ni kipi.
 
Mtu wa k
Mkuu si kujifariji ni ukweli mtupu. Hebu chukua hata dakika moja kutafakari: hivi mtu tajiri kwelikweli kipesa ana kitu gani cha ziada ambacho mtu wa kawaida hana iwapo wote wana furaha, amani na wanaishi kwa haki?

Mnapenda sana kutukuza maisha ya kifahari bila sababu za msingi.
Kama upati basic needs utapata vipi furaha na amani
 
Haya mawazo yakimasikini ndio mana wa Africa hatuendelei
Kwa sentensi yako hiyo ya "Afrika hatuendelei" mi nafikiri maskini kweli kweli ni yule anayejipuuza eti kisa hana mali na pesa na kuishi na stress ya kutafuta utajiri.
 
Sijakuelewa hata unachokipinga ni kipi.
Mkuu pia kumbuka uwe TAJIRI au masikini kufa ni sheria na katka kufa mala nyingi mtu huanza kuugua na lazima akonde tu lakini hapa tuachoangalia je ukifka watoto wako watarithi nini?Ufukara au Mali?Watoto hurithi hurithi Mali hata vitabu vya duni Zote vinasisitiza hivo.Piga kazi Mungu atakubariki uwarithishe wanao Mali.
 
Kukata miti kunaendana na kupanda miti.
Mababu zetu wangekata hio Mibuyu ili kutengeneza furniture na kujipatia kipato leo hii mibuyu yote ingekuwa kama mchicha...., In short shortsightedness ya kizazi cha sasa ndio kinapelekea mabadiliko ya tabia nchi na dunia nzima kulipia gharama..... (Busara ni badala ya kutumia mbuyu kutengeneza furniture kwanini usitumie bamboo inayoweza kukua kwa haraka, na mibuyu ibaki kutupatia matunda)

As they say a flap of a butterfly wings in Amazonian Forests can Cause a Tsunami elsewhere..., Ingawa sidhani kama msemo huo ulikuwa una maana literally..., lakini a small change here or there can cause a big impact elsewhere.....

In short true value of things is seen through a marketed lens na unanunua kitu sio kwamba ni bora zaidi ya kingine bali ni kampuni ipi ina pesa zaidi za kufanya marketing (kwahio in the end its better marketers who wins na sio necessarily better product producers)....,
 
Mtu wa k

Kama upati basic needs utapata vipi furaha na amani
Mtu kama hana amani au furaha na haishi katika haki, huyo ni maskini kweli kweli bila kujali anafanya nini na anaishi wapi. Hivyo lengo la maisha yetu haliwezi kuwa kufukuzia (au kujilinganisha na) utajiri wa akina Apple na wenzake. Lengo la maisha yetu liwe kuitafuta na kuipata hiyo haki, amani na furaha. Na si lazima uwe tajiri kupata hiyo amani na furaha na wala si kweli kwamba waafrika walio wengi tumekosa basic needs katika maisha yetu.
 
90% wameikosa basic needs aisee.
Kama watu wanakufa kwa kukosa sh 500 ya panadol,wanakosa nauli mtu anatembea kwa miguu toka mwenge hadi mbagala,anakosa elf 20 ya kodi ya chumba.
Katu hawezi kuwa na amani au furaha.
 
Hazina thamani leo au jana vipi kuhusu kesho ? Na utajiri ni nini ? (Ardhi, Maziwa, Watu, au Umiliki wa Asset ; ambayo nchi ni asset)... Au ni makaratasi fulani ambayo kwa wakati huu tumepatana / wamepatana kwamba value yake ni kiasi fulani ila kesho tunaweza kubadilika kwamba karatasi hizo hata kuzichoma kama kuni hazina faida ?

Nchi inajivunia watu (loyal citizens) hata iweje ni wananchi wa taifa hilo..., Apple akifanya fyongo tu kesho watu watahamia kwenye Pears...., all in all nchi yenye ardhi na sovereignty huwezi kuilinganisha na abstract things kama stock prices or nguvu ya dollar (FIAT MONEY)..., Of course Brand name au Fame ya Brand inaweza ikawa valuable (lakini hizo ni perceptions na power of marketing which can change overnight); ila nguvukazi ya watu elfu kadhaa kule Burkina-Faso ni asset ambayo ikitumika inaweza hata kulima mchicha au kuvua dagaa....

Nakuacha na msemo wa Voltaire kuhusu Paper Money
Paper money eventually returns to its intrinsic value: zero.
Mkuu wewe unayajua sana haya masuala, umejibu vizuri sana. I wish tuwe na maongezi mbali na hapa jukwaani. Kama unaridhia nitaarifu kwa PM au hapahapa
 
Back
Top Bottom