Utajiri wa Apple Inc. ni mkubwa kuliko GDP ya Afrika

Long term wealthy na short time Partying.......

Unaweza ukatumia hizo resources ukakata miti yote.., ukavua samaki wote na mwisho wa siku wajukuu zako wakafa njaa (kwa ufujaji wako na kutokuwa sustainable)

Nchi ambayo ina asset ya ardhi hence inaweza kulima na kujilisha na kutumia hio miti kujenga kibanda cha malazi bila kusahau hata kuvaa ngozi ili kupata mavazi kamwe huwezi kuwaita ni masikini.... Hata kama wenyewe wameridhika wajukuu zao watakuwa na nyezo za kuweza kupata their basic needs.... Nakuacha na msemo wa Wahenga Red Indians..... (Huenda ndio ukajua true / real wealthy) na sio advertised marketed abstract so called utajiri...

When the last tree has been cut down, the last fish caught, the last river poisoned, only then will we realize that one cannot eat money.
Mkuu naomba tuongee
 
90% wameikosa basic needs aisee.
Kama watu wanakufa kwa kukosa sh 500 ya panadol,wanakosa nauli mtu anatembea kwa miguu toka mwenge hadi mbagala,anakosa elf 20 ya kodi ya chumba.
Katu hawezi kuwa na amani au furaha.
90%? Mh! hiyo takwimu ni ya kutilia mashaka katika nchi ya uchumi wa kati hata kama ni uchumi wa kati wa chini.

Mi bado nisisitize kwamba hii dhana ya kuoanisha utajiri wa mali kuwa ndio utajiri wa roho na wa kweli ni dhana ya kimagharibi "Materialism" na tusipowekea breki na kuitathmini kwa upya inaweza kutuulia spirit na morale ya kizazi chetu kinachopaswa kuibeba Tanzania ya sasa na ya miaka mingi ijayo. Kuna kundi kubwa la watu wameibugia hii dhana (hasa baada ya utandawazi) wanaotafuta mali na utajiri kwa gharama yoyote ile. Matokeo yake watu wanapata mali na utajiri lakini havionekani kuwasaidia. Sipendi kutoa mifano lakini kama kuna kipindi katika historia ya maisha ya binadamu ambapo watu wana utajiri wa mali na pesa ni kipindi hiki tunachoishi sisi. Yet, I don't see kama watu wana amani na furaha, kila kukicha ni ugomvi na kulalamika.

Watu wafundishwe au wajifunze na kuelewa kuwa ridhiko la kweli la mtu si lazima lipatikane kupitia utajiri wa mali na fedha.
 
Mkuu nahisi chanzo chote ni pale ulipochomekea nadharia ya kimagharibi ya roho mtakatifu
 
Ingekuwa ni rahisi kiasi hiko kila mtu angekuwa tajiri basi... Afrika ndo bara tajiri kuliko mabara yote duniani.... kama unabisha sema su
 
Kampuni ya Apple ambayo inatengeneza bidhaa za iPhones na Mac imekuwa kampuni ya kwanza kufikia thamani ya dola trilioni 3 katika soko la hisa

Thamani hiyo ni kubwa kuzidi hata Pato la Ndani la Afrika(GDP) ambalo ni dola trilioni 2.6

Kampuni hiyo imefanikiwa kukua kwa kasi ndani ya miezi 16 ambapo #COVID19 imekuwa ikisumbua dunia
Wazungu wanatuzau sana Afrika ndio maana hata kwenye Ramani ya Dunia Afrika ni bara la 2 kwa ukubwa lakini limechorwa kadogo kanazidiwa na Ulaya na hata Amerika, huwezi ukasema Thamani ya hisa za Apple zinazidi thamani ya bara la Afrika kwa maana ya mapato wanaiba maliasili zetu hafu wanatuletea data zao za uongo
 
Kampuni ya Apple ambayo inatengeneza bidhaa za iPhones na Mac imekuwa kampuni ya kwanza kufikia thamani ya dola trilioni 3 katika soko la hisa

Thamani hiyo ni kubwa kuzidi hata Pato la Ndani la Afrika(GDP) ambalo ni dola trilioni 2.6

Kampuni hiyo imefanikiwa kukua kwa kasi ndani ya miezi 16 ambapo #COVID19 imekuwa ikisumbua dunia
Kwa nini unalinganisha THAMANI na GDP ?

THAMANI ya Apple ni kipimo cha utajiri wa mali zake zote ilizokusanya na kujijenga toka kampuni iundwe kama zingeuzwa leo kwenye soko la dunia la hisa, kizungu Market Capitalization.

GDP ya Africa ni thamani ya uzalishaji uliotokea Afrika kwa bidhaa na huduma zilizouzwa ndani ya Afrika ndani ya mwaka mmoja. Vitu viwili tofauti.

Ukitaka kutulinganisha na thamani ya Apple basi thaminisha utajiri wa Afrika, jumlisha thamani ya kila kitu kilichomo Africa.

Anza na Tanzania, jumlisha viwanja vyote, bandari, majengo, migodi, cash money, mabasi, ma reli, ma bomba ya mafuta, mabwawa ya umeme, mashamba, mbuga, wanyama, ma airport, mahoteli yote ya Tanzania. Jumlisha thamani yake. Apple yenye THAMANI ya $ 3 tril ingeweza kuinunua Africa kwa $ 3 trillion ?

Unashindanishaje UTAJIRI wa Azam/Bakressa toka aanze biashara (Market Capitalization, au Thamani) versus KIPATO cha mwaka huu tu cha Mo Dewji/Muhammed Interprises kwa mauzo ya ndani ya Tanzania tu (GDP) ???????
 
90%? Mh! hiyo takwimu ni ya kutilia mashaka katika nchi ya uchumi wa kati hata kama ni uchumi wa kati wa chini.

Mi bado nisisitize kwamba hii dhana ya kuoanisha utajiri wa mali kuwa ndio utajiri wa roho na wa kweli ni dhana ya kimagharibi "Materialism" na tusipowekea breki na kuitathmini kwa upya inaweza kutuulia spirit na morale ya kizazi chetu kinachopaswa kuibeba Tanzania ya sasa na ya miaka mingi ijayo. Kuna kundi kubwa la watu wameibugia hii dhana (hasa baada ya utandawazi) wanaotafuta mali na utajiri kwa gharama yoyote ile. Matokeo yake watu wanapata mali na utajiri lakini havionekani kuwasaidia. Sipendi kutoa mifano lakini kama kuna kipindi katika historia ya maisha ya binadamu ambapo watu wana utajiri wa mali na pesa ni kipindi hiki tunachoishi sisi. Yet, I don't see kama watu wana amani na furaha, kila kukicha ni ugomvi na kulalamika.

Watu wafundishwe au wajifunze na kuelewa kuwa ridhiko la kweli la mtu si lazima lipatikane kupitia utajiri wa mali na fedha.
Unazungumza dhana mbili utajiri wa roho na wa mwili
 
Kwa nini unalinganisha THAMANI na GDP ?

THAMANI ya Apple ni kipimo cha utajiri wa mali zake zote ilizokusanya na kujijenga toka kampuni iundwe kama zingeuzwa leo kwenye soko la dunia la hisa, kizungu Market Capitalization.

GDP ya Africa ni thamani ya uzalishaji uliotokea Afrika kwa bidhaa na huduma zilizouzwa ndani ya Afrika ndani ya mwaka mmoja. Vitu viwili tofauti.

Ukitaka kujua utajiri wa Afrika, jumlisha thamani ya kila kitu kilichomo Africa.

Anza na Tanzania, jumlisha viwanja vyote, bandari, majengo, migodi, cash money, mabasi, ma reli, ma bomba ya mafuta, mabwawa ya umeme, mashamba, mbuga, wanyama, ma airport, mahoteli yote ya Tanzania. Jumlisha thamani yake. Apple yenye THAMANI ya $ 3 tril ingeweza kuinunua Africa kwa $ 3 trillion ?

Unashindajishaje UTAJIRI wa Bakressa toka aanze biashara na KIPATO cha Mo Dewji cha mwaka huu, kwa mauzo ya ndani ya Tanzania tu (GDP) ???????
Kwa thamani ya utajiri wa mali kwa Afrika huyo apple anaingia mara elf moja kwa utajiri uliopo Afrika.Hata wa TANZANIA tu afiki,Congo ndio nchi ya kwanza duniani kwa utajiri asili,sizungumzii utajiri pesa.tza top five imo
 
Unazungumza dhana mbili utajiri wa roho na wa mwili
Ndiyo, ila utajiri wa roho (amani, furaha na haki tele) huo ndio wa muhimu zaidi. Ukiwa navyo vyote sawa, ila ukiwa na mali ila ukakosa vya rohoni kwangu mimi nakuona bado maskini tu.
 
True thus madikteta na wasiojulikana wao Wana KILA kitu lakini utajiri wa rohoni ni sifuri hofu na mashaka vimewajaa
 
Kweli, na ni lazima tuwe makini na kuzikataa falsafa au mitizamo inayojaribu kutuaminisha kwamba maisha yetu ni maskini au hayana thamani kwa sababu hatuna vitu na pesa mingi.
 
Mkopo wa 1.3 trilioni Tsh umezua tafrani, imekuwa mjadala wa kitaifa
Ndo ujue Afrika ni masikini
 
Back
Top Bottom