Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe umeongea pointi, maana watu wanavyoangaika kama ni pesa nyingi sana,kiasi iwe ni maajabu kwa DIAMOND kuwa nayo.Pesa ya mboga hiyo ..mi ninayo mara mbili yake
Acha hasira, maana unaongea kama vile kakulazimisha uamini wakati yeye kaulizwa swali akalijibu, sasa wewe uwe umeamini au hujaamini hayo ni matatizo yako sisi hayatuhusu.Kwani hapa nipo kumpunguzia au kumuongezea nini, fisimaji wewe
[emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Tangu wameanza kuongeza sifuri, sitakaa nimuamini msanii yeyote
Unajua Shida ni kuwa chanzo cha habari hiyo yaweza kuwa ni kutoka kwa Diamond na watu wake ili kuwakoga wasanii wenzake. Bila kujua wakati mwingine ni kuwakaribisha watu wa kodi ku scrutinize mapato yako ili wakulipishe kodi kwa mujibu wa sheria.Sidhani kama ana utajiri huo
Umetumwa? Mi nina experience na interview za wasanii hasa wanapotakiwa kutaja gharama za video wanazoshoot South, networth n.k huwa wana mtindo wakufanya multiplication kwenye original figure ili ku-deceive public na kucreate attention tuwaone special sana,Acha hasira, maana unaongea kama vile kakulazimisha uamini wakati yeye kaulizwa swali akalijibu, sasa wewe uwe umeamini au hujaamini hayo ni matatizo yako sisi hayatuhusu.
Ndio nimetumwa, vipi na wewe unataka kunituma ........ Bado narudi pale pale je, inampunguzia nini kwa wewe kubishia kitu ambacho keshakiongea ......... iwe umeamini au hujaamini hilo ni tatizo lako,kwasababu yeye si kiongozi wa ngazi yoyote kwenye jamii,kwahiyo kama anaongopa anajiongopea mwenyewe si wewe wala mimi na ndio maana hajapanda jukwaani akasema hivo ila kaulizwa ndio akasema.Umetumwa? Mi nina experience na interview za wasanii hasa wanapotakiwa kutaja gharama za video wanazoshoot South, networth n.k huwa wana mtindo wakufanya multiplication kwenye original figure ili ku-deceive public na kucreate attention tuwaone special sana,
kwa taarifa yako tu Diamond wala msanii yoyote wa Bongo hakuna anayefikisha walau 3bil. Damn
Kumekuwepo na tetesi nyingi kuhusu utajiri wa Diamond umefikia kiasi gani. Hilo ni swali ambalo hajawahi kulijibu kwa uhakika zaidi ya kutoa tu hints na kuwaacha wanaouliza kubaki na majibu yao wenyewe vichwani.
Lakini kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip kilichorushwa Jumapili ya June 26, tunaweza kusema walau kwa uhakika staa huyo ana utajiri mkubwa kiasi gani. Diamond ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya bilioni 8.6.
Si kitu kinachoshangaza tena kwa Diamond kutokana na hatua aliyofikia akiwa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania kwa sasa. Fedha zake nyingi zinatokana na show zake zisizokauka za ndani na nje ya nchi, mikataba ya ubalozi na matangazo kutoka makampuni kama Vodacom, Cocacola, DSTV na Red Gold. Hivi karibuni alipata deal jingine la kutangaza huduma ya taxi ya Uber.
Pia amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia biashara ya nyimbo zake hasa miito ya simu, malipo ya mirabaha kutoka nchi za jirani kama Kenya bila kusahau biashara za mtandaoni zikiwemo Youtube.
Uwekezaji wake kwenye label ya WCB ni kitu kingine kikubwa ambacho kitaanza kumuingizia fedha nyingi siku za usoni. Hadi sasa amesaini wasanii wanne wakiwemo Rich Mavoko, Raymond, Harmonize na dada yake Queen Darleen.
Lakini pia staa huyo anafahamika kwa kuwekeza zaidi fedha kwenye ardhi na nyumba huku akidaiwa kumiliki maeneo mengi jijini Dar es Salaam.
Hahahahahah kwa hiyo wewe wakenya umewaona ndio mfano wa watu wa maana kwako alafu unamdharau Diamond!! Kweli dunia haiishi maajabu.Ivi kwanza unajua maana ya bilioni??
Bilioni halafu unakaa madale Nyumba ya kupanga ukuta umejemgwa juu ya bomba la dawasco
Asubirie kwanza hasira ya jiji
Humu ndani huwa mnapost upupu sana
Ndo maana wakenya wanawaona kama vibwengo