Utajiri wa Magofu ya Rapta

📴
 
Upo sahih
 
TUNAENDELEA WAKUU

Fatemeh hakutaka kujibu swali langu, na mimi nilimuuliza kwa makusudi ili tu nimtoe kwenye mood aliyokuwa nayo kuhusu kile tulichokua tunakiongelea. Kitu kingine alichokua anataka ku enjoy fatemeh ni kile kitendo cha kutembea umbali mrefu kidogo kwa mguu.

Hivyo kutokana na ka umbali kalikokuwepo kutoka eneo lile mpaka tulipo egesha gari tulitumia dakika kadhaa kutembea na huku tukiongea mambo mengi. Kwa upande wangu nilimsimulia japo kwa uchache Kuhusu baadhi ya mambo kwenye maisha yangu ambayo niliamini hayajui.

Bilashaka tulienjoy sana siku hiyo kwa upande wangu nilifurahia mazingira yale lakini pamoja na vinywaji vilivyopatikana eneo hilo. Tulibeba kwenye vifungashio vitu kadhaa na wakati tukitembea kuelekea tulipo egesha gari ni wazi yoyote angetuona angeamini tulikuwa wapenzi.

Tukiwa kwenye gari tunaelekea nyumbani fatemeh aliilaza kabisa siti yake na jambo hili lilifanya niweze kuiona vyema shape au umbile lake.

Fatemeh alianza kunizoea kiasi kwamba ata ile desturi ya kijistiri sana akiwa na mimi ilipungua tofauti na kama ilivyokua hapo awali wakati ndio tunafika kutokea haullaga.

Ulikua ni usiku ulioenda sana japo sikumbuki ilikua ni saa ngapi, ila kwa hakika nilimuona fatemeh akiwa amefurahia mtoko ule kwani ulimpunguzia baadhi ya mambo yaliyokua yamejaa kichwani mwake.

Tulikaribia jengo ambalo ndilo lilikua na apartments ambazo alikua anaishi fatemeh, hivyo tulipitiliza moja kwa moja mpaka eneo la basement ambapo tulitakiwa kuegesha gari ile.



Baada ya kufika eneo la basement nilimshtua fatemeh ambae alionekana kuanza kutekwa na usingizi nadhani sababu ya uchovu wa usiku ule.

Fatemeh alinyanyua siti ili aweze kutoka ndani ya gari lakini alikutana na mdomo wangu moja kwa moja na kama kawaida yake hajawahi kupinga zaidi ya kunikimbia ikitokea amepata nafasi.

Tukiwa kwenye moment ile kuna mambo mengi yanabadalika kwenye mwili wa fatemeh hususani joto la mwili na mapigo ya moyo hubadilika ghafla na kupanda wakati huo huo.

Kitu cha tofauti kwa siku ya leo ni kwamba fatemeh alitumia nguvu kubwa kunivuta na kunishikilia ikiwa ni ishara hakutaka tuwahi kumaliza jambo lile haraka haraka ni kwamba alihitaji tutumie muda kidogo.

Jinsi mwili wa fatemeh ulivyokuwa mlaini huwezi amini ukiambiwa alikuwa ni ninja wa kike na kiukweli nilikua natamani sana siku moja nimuone akiwa kwenye harakati hizo za kininja anafananaje.

Siku hiyo tulijitahidi kwenda mbali kwani nilifanikiwa kutoa koti lake refu kwa upande wa juu hivyo nikiwa nakaribia kuitoa blazia. Tulisikia Bonnet inagongwa kwa nyuma na mtu ambaye hatukumjua ni nani.

MIMI: what the f**k
( Ujinga gani huu )

Na wakati ule fatemeh pia alistuka ni kama mtu aliepotelewa na fahamu na hivyo hapo ndio zilikua zinamrudia.

Nilishuka kuonana na mtu huyo wakati fatemeh akijirudishia nguo zake ambazo hakumbuki zilivuliwaje ndani ya dakika chache zile.

Aliyekua anagonga ile bonnet alikua ni askari wa eneo lile na aliongea lugha ambayo siku ifahamu na nilipo muuliza kama anaongea kingereza alijaribu na jambo lake lilikua ni kusisitiza tume park gari sehemu ambayo sio sahihi na ata mimi baada ya kuangalia niligundua ni kweli.

Nilirudi ndani ya gari ili kuhakikisha naiegesha sehemu niliyoelekezwa na yule askari lakini nikiwa Ndani ya gari fatemeh aliuliza niliwezaje kuzitoa nguo hizo kwa dakika chache vile. Sikumjibu zaidi ya kutabasamu tu huku nikiwa makini kuhakikisha sikosei kwa kile nilichokua nakifanya.

Tulishuka na kuelekea eneo la lift ambapo ndani ya muda mchache tulikua tayari ndani ya apartment yetu. Tukiwa ndani nilikumbuka kuwa tumesahau vile vifurushi vilivyokua na bidhaa tulizo rudi nazo toka 30-Tir Street.

Hivyo nililazimika kurudi tena kwenye basement kwa ajili ya kuchukua mizigo ile lakini bado nilimkuta yule askari akiwa maeneo yaleyale.

ASKARI: sorry the new guy, is that your wife?
( Samahan kijana mgeni yule ni mke wako?)

MIMI: no! we friends
( Hapana sisi ni marafiki)

ASKARI: what do we call friends who kiss?
( Tunawaitaje marafiki wanao kiss)

Mpaka hapo nilitabasamu tu nikiamini jamaa kumbe aliona wakati namnyonya fatemeh hivyo ilitosha yeye kusema tulikua wapenzi na hakuna namna ningepinga.

Yule askari alinisifia kwa kusema kama nimeweza kung'oa yule mtoto basi mi ni hatari sana kwani binti huyo hakuwahi kuonekana na mtu yoyote toka ameanza kumjua.

Sio kuonekana kimapenzi tu bali ata kuonekana akiongea na mtu yoyote kwani ni binti ambaye yupo cool masaa 24 siku 7 za wiki. Jamaa alidai yeye pamoja na kukaa hapo sikuzote hajawahi ata kusalimiwa na binti huyo hivyo alijiuliza m'bongo mimi nina nini cha ziada.

Yule askari alikua anaongea maneno mengi sana lakini sikuyatilia maanani zaidi nilitoa snacks zilizo kwenye vile vifungashio na nikampatia asogeze masaa.

Wakati naondoka aliniambia anaitwa Mohamed na ikitokea siku nimepatwa na changamoto yoyote yupo pale nimuone lakini sio changamoto ya pesa wala mapenzi.

Nilirudi kwenye floor yetu chap na moja kwa moja nilienda kwenye room ya fatemeh ambapo nilimkuta ametoka kuoga akiwa na taulo tu. Na aliponiona alishangaa kwanini hakufunga mlango mpaka ameruhusu the African rude boy nimeingia.

Sikujali alichokua anaongea zaidi nilienda moja kwa moja bafuni kuweka mwili sawa na kuondoa uchovu. Fatemeh alisisitiza nisitoke uchi tu kwani hana mpango wa kuona linyoka langu.

Nilipotoka bafuni moja kwa moja nilijitupa kwenye kitanda na fatemeh alisimama kama mtu aliyesusa kulala mpaka niondoke. Nilichofanya pale baharia ni kujifunika shuka vizuri nikimaanisha ndio nimefika apo kama atataka ahame chumba na leo.



Nilipotelea usingizini mpaka asubuhi ambapo nilistuka na kukuta kuna mstari mreefu wa mito ukitutenganisha nilipo lala mimi na alipolala fatemeh. Niliishia kucheka tu na kumchungulia upande wa pili wa mito alipokua amejifunika mwili mzima na kuacha sura tu.

Alipogundua na muangalia alinionyesha ngumi akimaanisha nikimsogelea atanichakaza.

MIMI: you want to break my neck like a gringo in the mine
( Unataka univunje shingo kama mzungu wa mgodini)

FATEMEH: No! Damião lied to you
( Damião alikuongopea)



Nilimwambia haina shida ata kama ni kweli mi nipo tayari kwa lolote ata kama ataniua ni kama nzi kufia juu ya kidonda tu.

Hapo niligundua kuwa fatemeh hakuwa anajua kama nilikua na CV yake ya kimapigano ambayo nilipewa na bwana Damião.

Alinikurupusha kwamba natakiwa kwenda kwa shahzad hivyo nitoke kitandani nisiendelee kumpigisha stories. Nadhani alijua kuwa namlia timing na kama angeruhusu niendelee kuwepo pale dakika tano mbele zingekua nyingi sana na zingenitosha kuhakikisha anabaki kama alivyozaliwa.

Siku hiyo nilijipigilia kanzu yangu moja safi na expensive sana kwa sehemu za ukanda ule wote wa Tehran. Fatemeh alinisindikiza mpaka mlangoni nikapigwa good-bye kiss lakini alinisisitiza niache utoto na nisilete usumbufu mara nyingine kwa dereva.

Apo nikajua kumbe bwana dereva alishtaki tayari kama namzingua japo nilimzingua mara moja tu. Kama kawaida tulitumia mda mchache tu kwa speed kali ya gari ile mpaka Tunaingia kwa shahzad.


Nilipofika nyumbani kwa shahzad nilikaribishwa ndani na nikakaa sebuleni kumsubiri mzee mkongwe, na wakati huo nilimbatiza jina nilimuita mjanja wa mzizima.

Hakika shahzad alifurahi sana mara zote alizokua ananiona na furaha yake ilikamilika zaidi tulipokua tunaongea kiswahili.

Shahzad alitokea eneo lile la sebuleni na kumpatia kitu mjukuu wake kisha akiniambia tuelekee chimbo letu ili akanipe nondo za kutosha kwani alidai siku hiyo atakua na muda mchache sana wa kukaa kwenye chumba kile.

Sasa bwana kitu alichotoa shahzad kumpa mjukuu wake ilikua ni kikopo kidogo cheupe kimeandikwa RITALIN kikopo hiki ni kama kile alichokichukua fatemeh siku ile kwenye chumba changu.

Hivyo nilipanga tukiingia ndani ya chumba kile cha maktaba nimuulize ile dawa ilihusiana na nini japo sikupanga kumwambia nimeiona wapi.

MIMI: mzee Samahani ile dawa uliyompa mjukuu wako inaitwaje maana leo sio mara ya kwanza kuiona, nimeshaiona au kukutana nayo mara kadhaa siku za nyuma.

SHAHZAD: ile dawa inaitwa Methylphenidate, inatumika kwenye matibabu ya ugonjwa unaojulikana kama Attention-Deficit Hyperactivity Disorder. Au kifupi huitwa ADHD mara nyingi wataalamu wanatumia jina la psychostimulant kuitaja dawa hii.

MIMI: huo ugonjwa unakuaje maana mjukuu wako namuona ni mzima kabisa hajawahi kuonyesha dosari yoyote tokea nimefika hapa.

Shahzad alidai ugonjwa ule umekaa kisaikolojia sana hivyo ni ngumu kuona dalili kwa mtu mzima ambae ameanza tiba mpaka ukae nae karibu kwa muda mrefu lakini kwa mtoto unaweza kuona dalili hizo mapema.

Kwa mtoto mdogo unaweza kugundua mapema kupitia vitu kama,
  • mtoto anakua careless kiasi cha kutokuweza kutambua hatari, unaweza kuta mtoto anasogelea jiko nakushika moto kwa mikono na ata akiungua huweza kusahau na kurudia tena jambo lile lile.
  • kama yupo lika la shule apa unakuta mtoto kila siku akirudi nyumbani amepoteza aidha daftari au kalamu au begi zima. Mtoto wa hivi utapiga mpaka utamng'oa meno lakini tatizo linatokana na ugonjwa huo tajwa apo juu.
  • jambo lingine mtoto huchelewa sana kuongea ukilinganisha na watoto wengine ambao hawana shida hii.

Shahzad aliuliza nimeiona wapi dawa ile kwani haitolewi kiholela kama dawa nyingine kwa sababu tu Methylphenidate ina pharmacological effects ambazo ni sawa kabisa na cocaine.

Hivyo hupelekea watu wengi kuzitafuta kwa njia zisizo za halali kwa ajili ya matumizi yao binafsi na sio kwa ugonjwa kama inavyotumika na wenye shida hiyo ya ADHD.
 
Kwa hiyo fatemeh anaitumia hiyo ADHD kimagendo
 
"Aisee nilikua napika chakula fulani hivi maarufu kama chelow kebab kwa huku Iran"

"Huku" badala ya "huko/kule" ina maana bado upo Iran mzee?
 
"Aisee nilikua napika chakula fulani hivi maarufu kama chelow kebab kwa huku Iran"

"Huku" badala ya "huko/kule" ina maana bado upo Iran mzee?
Nadhani kaongelea kwa wakati uliopo na yeye ni muhusika mkuu hata alipo kua haulaga alikua anaongelea kwa wakati uliopo as if ni kitu kinachoendelea mda huu. Ni sehemu nyingi hasimulii kama ni wakati uliopita labda aliya nukuu matukio.
 
Wiki imeisha toka utume Last episode[emoji848][emoji848]
Broo story inapoteza mvuto kabisa ndio maana hata watu hawaulizii kama mwanzoni .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…