Utajiri wa Magofu ya Rapta

Hii story ni tamu
Big up mwandishi
Whether iwe ya kutunga kama wengi wanavyokosoa
Iwe ya kweli
Au mixer
Inafundisha reality na kutembea kimawazo
Kikubwa exposure na kufikirisha…
 
Story nzuri sana mkuu. Hapa nina arosto kama yote ebu shusha episode nyingine fasta.
 
Honey trap ni mbinu inayotumiwa sana na mawakala kutoka Mashirika ya kijasusi ili kupata taarifa kutoka kwenye point iliyokusudiwa. Mbinu hii inahusisha mahusiano ya kimapenzi au kingono kabisa baina ya wakala (trapper) na mtu aliyekusudiwa kutoa taarifa au mtu mwenye access ya taarifa hiyo ambayo ni taarifa ya siri. ( confidential information).

Hii mbinu mara nyingi hutumiwa na mawakala wa kike na ni mbinu m'badala baada ya kuona mbinu zote zimefeli.

Yaani apa agent ana amua ku sacrifice mwili wake kwa muhusika ili tu kupata info, wapo wanaofikia hatua ya kuliwa tunda kabisa na wapo wanaofanikisha misheni bila kuliwa tunda.

Inategemea na utashi wa agent lakini pia na ujanja wa mtu ambaye ni targeted na mwenye taarifa hizo ambazo ni confidential.

Tumeshuhudia mara nyingi mbinu hii ikitumika sanasana kwenye Mashirika ya kijasusi kama vile KGB ( Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti) au kwa maana nyingine “Committee for State Security.” hili ni shirika la kijasusi kwenye umoja wa kisoviet wakati huo huo china pia imehusishwa sana kwenye matumizi ya mbinu hii.

Kutoka kwa KGB na China kuna misheni nyingi zinazojulikana zilizohusisha mbinu hii lakini kwa shirika kama CIA bado hakuna ushahidi wa moja kwa moja uliohusisha matumizi ya honey trap kwenye kutafuta taarifa za siri.

Wapo wanaotumia neno hili mbali na mazingira ya kijasusi japo neno hili kwa mara ya kwanza lilitumika kwenye shughuli za kijasusi. mfano watu hutumia pia neno hili honey trap kwenye shughuli za utalii wakimaanisha kitu chenye kuvutia au kuwavuta watu.

Asili ya neno hili kama nilivyosema apo awali lilianza kutumika kwenye ulimwengu wa kijasusi na muasisi ni bwana mmoja kutoka uingereza aliyeitwa John le Carrè a , ambaye mnamo miaka ya 1970's alitoa kitabu maarufu sana kilichoitwa “Tinker Tailor Soldier Spy".

Mpaka hapo nadhani umepata picha ikitokea siku umekutana na neno Honey trap kwenye mazingira yoyote yale basi hizo apo juu ndio maana zake.

Japo kwa sasa ata gold diggers au wadangaji kwa kiswahili wanatumia neno hilohilo Honey trap kwenye misheni zao, wenyewe wanamaanisha kumtega mtu kimapenzi ili tu waweze kupata pesa kutoka kwa yule anaemtega.

Kinacholengwa wakati wa honey trap sio lazima taarifa pekee hapana ata mauaji pia hutekelezwa kupitia mbinu hii hii ya honey trap.

Yaani binti anaanzisha mahusiano ya kimapenzi ili tu kukutengenezea mazingira ya kuku assassinate ki rahisi. Apa wale wazee wa kula tunda kimasihala ndio tunawapoteza sana kwa staili hii.

Kwenye makala mbalimbali tumeshakutana na visa vinavyohusisha watu kuoana na mbaya zaidi wengine walizaa mpaka na watoto kumbe mwanamke yupo kazini na sio ndoa ya kweli kutoka moyoni.

( Sina kisa cha kweli kuhusu uwepo wa ndoa hizi bali nimewahi kuisikia tu story hizi kwenye vijiwe vya kahawa)

Ahahaha ahahaha hahaha hizi kazi nyingine ni utumwa kwelikweli yaani ni utumwa wa kifikra mpaka kimwili.

Hatimae tayari tumejua nini maana ya honey trap au sexpionage kwa jina jingine kama linavyotumika kwa baadhi ya watu na maeneo.


Kwa kuhitimisha tu ni kwamba sexpionage ni mbinu inayohusisha mapenzi katika kukamilisha shughuli za kijasusi.

Mara zote trapper anakua ni jinsia ya kike huku akim target mtu wake ambaye mwenye hizo taarifa za siri na mtu huyo anakua mwanaume.

Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kwamba Russia na China ndizo nchi ambazo mpaka sasa kuna ushahidi wa kuwepo kwa visa mbalimbali vya kijasusi vinavyohusisha mbinu hiyo ya honey trap.

Kwenye simulizi hii tumeona kitu cha tofauti kidogo ambacho chenyewe pia ni mbinu hiyohiyo ya Honey trap.

lakini imetumika na mwanamke yaani Manuela ameitumia kwa Catarina japo Catarina hakuwa na taarifa zozote lakini bado lengo la misheni lilimtaka Manuela aanze na Catarina ili kumfikia Javier kirahisi.

Turudi kwenye simulizi yetu,

Fatemeh Alidai mtihani wa pili wa kuhakikisha anapata anachokitaka kutoka kwa Javier ndio ulikua mgumu na hapo alitakiwa kuwa karibu na mtu ambaye aliishi room moja na Javier.

Aliamini kumuingia Javier haraka haraka si kazi rahisi hivyo basi ili kupata taarifa za awali zilizomuhusu Javier alilazimika kuweka ukaribu na Gatkuoth.



Lakini kwa bahati mbaya sana Gatkuoth alikuwa tayari amesha athirika na madawa vya kutosha hivyo ata wangemshirikisha bado ingekua kazi ngumu kwa upande wa Manuela.

Nini kilimuua Gatkuoth?

Kama unakumbukumbu nikiwa haullaga Javier aliwahi kusema kifo cha Gatkuoth ambaye alikua ni kijana mweusi mrefu sana kutokea Sudan kilisababishwa na sumu aina ya strychnine.

Na kwa mujibu wa Javier ni kwamba Catarina alihusika moja kwa moja na kifo cha Gatkuoth kwani hakuweza kumdhania Manuela kabisa.

Kitu cha kufurahisha ni kwamba kwa mujibu wa fatemeh yeye alikua anaamini kifo cha Gatkuoth kilisababishwa na Javier na washirika wake japo hakua amejua sababu ya washirika hao kumuua Gatkuoth kwani hakuwahi kumshirikisha kabisa kwenye misheni yake.

Sasa basi nini kilimuua Gatkuoth na sababu ya kifo chake ni ipi?

Fatemeh anamuhisi Javier na washirika wake wakati huo huo Javier anamuhisi Catarina, sababu ya Javier ni wivu wa mapenzi Lakini upande wa fatemeh bado hajapata sababu ya Javier kuhusika kwenye kifo cha Gatkuoth.

Je! Nani yupo sahihi? Na kuna siri gani nyuma ya kifo cha Gatkuoth.

Mpaka hapo niliamua kumwambia fatemeh kuhusu kile nilichoambiwa na Javier Kuhusu kifo cha Gatkuoth. Nilimueleza fatemeh kuwa kwa mujibu wa Javier ni kwamba Catarina ndie aliyemuua Gatkuoth kwa Sababu ya wivu wa mapenzi.

Javier aligundua uwepo wa sumu aina ya strychnine kwenye mwili wa marehemu Gatkuoth wakati ukiuandaa kwa ajili ya mazishi na yeye ndiye aliyemzika Gatkuoth.

Maneno yale ni kama fatemeh hakuwahi kuyasikia popote kuhusu kifo cha Gatkuoth, Alidai kwa kuwa alishaona hawezi kumtumia Gatkuoth hivyo hakuona maana kabisa ya kudili na kifo chake.

Lakini swala lililomstua fatemeh ni baada ya mimi kumwambia kuwa Javier aligundua uwepo wa sumu kwenye mwili wa marehemu huyo. Na kilichomfanya Javier kugundua sumu hiyo ni viashiria vilivyokuwepo kwenye mwili wa marehemu ambavyo tulishavitaja hapo awali.

Sasa basi nini kilichomstua fatemeh, matumizi ya strychnine ndicho kilichomstua fatemeh alidai kwa miaka kadhaa sasa sumu hiyo imekua ikitumika kwenye mauji na kundi la watu aliowafahamu vizuri kabisa.

Lakini bado hakutaka kuamini kama ni kweli watu hao wamehusika na kifo cha Gatkuoth kwani haoni sababu ya watu hao kufanya hivyo.

Nilimuuliza fatemeh kuhusu jinsi gani mimi nimetumika kwenye mpango wao, je ni kweli wao ndio walipanga mimi nikafikie kwenye chumba kile cha javier na je! Walianza kunifikiria kunitumia mimi kabla hata sijatoka dar es salaam.



Fatemeh alisema mpango wa kunitumia mimi ulikuja siku moja kabla sijafika hapo, waliamua kufanya hivyo baada ya kugundua kama kwa jinsi walivyoniona nikiwa safarini waliamini kama nikikaa na javier angeweza kuniamini sana.

Kwanini Javier angeniamini? Ni kwasababu na yeye alikua anatafuta mtu wa kumshirikisha kwenye mambo yake tutayaona huko mbele, na waliamini kwa character na muonekano wangu ungemvutia Javier kunitumia kwenye mishemishe zake.

Fatemeh aliendelea kusema kuwa kabla hata sijafika alishapewa details zangu zote yaani alikua na file langu kuanzia siku nazaliwa mpaka ile siku napanda meli ya Panama kuelekea haullaga.

Na waliompatia file hilo walimuambia anaweza kunitumia mapema sana kabla sijaingia kwenye mikono ya Javier, na ule unyanyasaji aliokuwa ananifanyia Javier ilikua ni mbinu moja wapo ya kuniangalia na kuniandaa kwa ajili ya kunishirikisha kwenye mambo yake.

Fatemeh alidai kuwa anapaswa sasa kufuatilia kifo cha Gatkuoth kwani kunaweza kuwepo na sababu ya msingi sana kama kweli Javier haku husika.

Baada ya maongezi yale nilimuuliza fatemeh kuhusu jina la mtu anayeitwa Tala,

Ni kama fatemeh hakutarajia kusikia jina lile kutoka kwangu hasa kwa kipindi kile.

FATEMEH: where did you hear that name?
( Umeiskia wapi hilo jina)

Niliamua kumueleza pia situation nzima mpaka naipata au naikuta ile memo sehemu ambayo nilikua na salia pale chini. Fatemeh aliniambia kuwa jina la Tala ni jina lake la zamani sana kabla zahra ajambadilisha na kumuita fatemeh.

Fatemeh ni jina la mama yake na Zahra, zahra alifanya hivyo baada ya kuanza kumlea Rasmi fatemeh kama mtoto wake kwani licha ya umri wa zahra hakuwahi kubahatika kupata mtoto.

Sasa basi jina la Tala ata yeye fatemeh hajui kama aliwahi kuitwa jina hilo kwani alikuja kusimuliwa na zahra mwenyewe hapo baadae akiwa ameanza kukua.

Hivyo kwa maneno marahisi jina la Tala aliitwa fatemeh akiwa bado mdogo sana kiasi kwamba ata yeye mwenyewe hakumbuki kabisa kama aliwahi kuitwa na yeye kuitika zaidi ya kusimuliwa na zahra.

Fatemeh Alidai kwamba mtu huyo alikua anamjua vizuri sana kama ameweza kujua jina la Tala hivyo aliuliza kama kuna mtu yeyote ninaweza kumuhisi alikua ananifuatilia kwenye mizunguko yangu ya siku ile.

Jasusi ni mtu anaetembea akiwa sensitive sana na mazingira yote yanayozunguka, apa namaanisha atakua makini kuanzia na watu wanaomzunguka popote alipo lakini pia bila kusahau vingine vyote.

Sasa basi kwa mujibu wa swali la fatemeh kwangu, kama ningekua jasusi ningeweza kuhisi uwepo wa watu wanaonifuatilia lakini kwa bahati mbaya sisi ambao sio majasusi tunatembea kama bata.
 
At least umekuwa muelewa kidogo kwan story ilianza kupoteza mvuto.
Ulimaliza week moja bila kutuma na hakuna hata mtu mmoja aliyeuliuzia .

Mwanzoni hii story ilikuwa inamashabiki Kama laki hv . Amsha Broo maana kadri inavyosomwa ndio mashabiki wanaongezeka
Na baadae hata ikiisha Tutalipia ili tuwe nayo maghetoni maana mbali na kuburudisha ina Elimisha pia.
 
Kwani kwa unavyo ona hii story itaisha? Hizi nidalili za msimuliaji kuwakimbia wasimuliwaji, .... Zamani alikuwa akichelewesha kutuma episode aliomba samahani sikuhizi akichelewesha kutuma episode tunasema mchawi elfu tatu....
 
Kwani kwa unavyo ona hii story itaisha? Hizi nidalili za msimuliaji kuwakimbia wasimuliwaji, .... Zamani alikuwa akichelewesha kutuma episode aliomba samahani sikuhizi akichelewesha kutuma episode tunasema mchawi elfu tatu....
Mchawi aftat Wallah
 
Msimtafute wala nini ataleta kwa muda wake
Hizo hela hatuna
 
TUNAENDELEA

Baada ya kuona nimemuacha fatemeh njia panda kutokana na lile swala la kumtajia jina la Tala, niliona kama nimemuongezea mawazo ya kumfanya aendelee kutafakari. Na sio hilo tu ata baada ya kumwambia kuwa javier hakuhusika na kifo cha Gatkuoth pia lilimfanya atafakari upya swala hilo.

Niliamua kumuacha peke yake na mimi nikaelekea kwenye room yangu kwa ajili ya kupumzika sikutaka kumsumbua kabisa kwa siku hiyo.

Kabla sijalala nilitafakari sana kuhusu swala la mzee shahzad, nilitamani nimalizane nalo mapema ili nirudi tena bongo kujaribu bahati yangu kuona kama naweza kupata Chochote.

Na pia nilitamani sana kukutana na watu ambao aliwasema kuwa wangenisaidia kwenye project hiyo lakini shida ilikua masharti ya fatemeh ambae hakutaka nikutane na watu wa aina yoyote pasipo idhini yake.

Baada ya mawazo ya hapa na pale nilifikia conclusion kwamba nisubiri fatemeh apitiwe na usingizi kisha nishuke basement nikaongee na Mohamed.

Sababu ya kwenda basement kwanza kabisa ni kumuuliza Mohamed kama ni kweli yeye alikuwepo kule clinic ya moyo nilipoenda na shahzad.

Kama ni kweli ni yeye, je! Na yeye ni mgonjwa au alikua ananifuatilia mimi kwenye mizunguko yangu na kama alikua ananifuatilia basi ni wazi atakua anamjua huyo Tala ambae kwa mujibu wa ujumbe ule nilitakiwa kuwa namsikiliza sana na nisipuuze kile alichokuwa ananiambia.


Basi bwana baada ya masaa kama mawili hivi niliamini fatemeh hawezi kuendelea kuwa macho kwani nilimuacha na mawazo mengi sana baada ya kumpa stories za javier na kile ki memo kilichoandikwa Tala.

Nilishuka na kuelekea basement kwa kutumia lift, jengo lile lilikua kimya zaidi mida ya usiku mnene kama ule. japo mara nyingi jengo hilo lipo kimya lakini kwa mida ya usiku ukimya ule huongezeka maradufu.

Nikiwa basement eneo ambalo nilitegemea kumkuta Mohamed kama alivyosema siku ile kwamba nikiwa na changamoto yoyote naweza kumkuta mahali apo.

Haikua hivyo kabisa kwani nilimkuta bwana mmoja mnene sana lakini alionekana kuwa lindo mida ile, na alipo niona tu aliniuliza kama niihitaji kukutana na Mohamed.
Sikujua ni kitu gani kilimfanya ajue ninataka kuonana na mohamed usiku huo. Lakini bila kuongea maneno mengi alinielekeza sehemu ambayo naweza kuonana na mohamed.

Aliniambia ili kumpata Bwana huyo Mohamed niende floor ya juu kabisa yaani floor ya mwisho ya jengo lile huko ndiko naweza kumkuta Mohamed. Kwakua nilisha dhamiria kuonana na mohamed basi nilianza safari ya kuelekea mahala nilipo elekezwa.

Haikuchukua muda mrefu kabisa kufika huko kwa sababu ya uwepo wa lifti ndani ya jengo lile. Nilipofika maeneo yale nilisikia sauti ya mtu akinikaribisha na bila shaka alikua ni Mohamed mwenyewe.

Lile eneo kwakule juu ya jengo lile kulikua na plain kabisa yaani hakukua na chochote na sikujua Mohamed alikua anafanya nini kule.
Mohamed alinikaribisha kwa maneno mawili tu huku akisema anatumaini nimeanda kule au nimemfuata maeneo ya huko kwakua kuna changamoto nimekumbana nayo.

Alisisitiza tu changamoto hiyo isiye ya mapenzi wala isiye inayohusu pesa. Na kwa kujiamini kabisa nilimwambia hivyo alivyovitaja haviwezi kuwa tatizo kwangu kwani vyote ninavyo.

Kuhusu mwanamke ninae binti mzuri ambae yeye mwenyewe alinishuhudia siku ile tukiwa tunadendeka ndani ya gari, na kuhusu pesa mwanadada huyo anazo za kutosha ata kumlipa yeye na kibarua chake cha ulinzi wa jengo lile.

Ni kama Mohamed kuna jambo alitaka kuliongea kuhusu ile kauli yangu ya kua nina mpenzi lakini nilimuona anasita kuitamka.

MOHAMED: What has brought you to me?
( Nini kimekuleta kwangu)

Kwa kujiamini kuliko pitiliza nilimkazia sura Mohamed huku nikumuuliza swali moja tu.

MIMI: I want to know why you're investigating me so much? I last saw you in the mosque yesterday
( Nataka nijue kwanini unanichunguza sana nilikuona msikitini jana)

MOHAMED: hhaahh ahaha hahah I'm glad to see you in that look,
( Nimefurahi kukuona kwenye muonekano huo)

Apa Mohamed alimaanisha amefurahi kuniona nikiwa serious lakini pia nikiwa najiamini na maneno yangu ya uongo.
Lakini pia alisema hakutarajia kama kuna muda nakua vile alijua mimi ni yuleyule wa kupelekeshwa na fatemeh kwenye kila kitu.

Ila alisisitiza jambo moja, alidai fatemeh ni kiumbe Smart sana kuliko navyofikiria hivyo hakuna jambo naweza kufanya nikamficha yeye eti asijue nitakua najidanganya.

Mohamed aliomba nieleze jambo lililonipeleka huko mapema sana ili ikiwezekana nirudi nyumbani haraka.

Jambo la kwanza nilishamueleza tayari japo hakunipa majibu ya kuridhisha kwanini alionekana kunifuatilia siku ya jana lakini kwa majibu yake yalionyesha hakua na muda huo kabisa.



Jambo la pili nilimueleza kama ataweza kunisaidia kufika kwenye kituo kilichoitwa nursery imam Ali. Nilimueleza kama nina shida ya kufika apo nionane na yeyote ambae alikua na muda mrefu kituoni apo.

Jibu la Mohamed lilikatisha tamaa kabisa, Mohamed alidai natakiwa kufuatilia mambo ya msingi na maana na yanayonihusu.

Apa alidai natakiwa kujua kwanza kwenye maisha yangu natafuta nini, nikisha kwisha kulijua hilo sasa nikomae na kutafuta kile chenye manufaa na sio ku dili na Mambo yasiyo na maana kwenye maisha yangu.

Sikuelewa kama Mohamed alijua ninataka kufika kituoni kwa dhumuni lipi,

Lakini kikubwa nilichoambulia kukisikia kutoka kwa Mohamed ni maneno magumu na ya vitisho.
Mohamed alisema kuna waliojifanya wana moyo kama wangu siku za nyuma kidogo, japo hakusema moyo kama wangu kivipi.

Alidai waliojifanya wana moyo kama wangu waliishia kufa kifo kibaya na kuzikwa kama mizoga baada ya miili yao kukaa zaidi ya siku mbili na kugundulika kama walishakufa.

Kuna muda nilihisi maneno yale kama yanamlenga Gatkuoth kwani kwa story za Javier ni kwamba mwili wa Gatkuoth ulikua na zaidi ya siku moja toka kufariki kwake na mpaka kugundulika kama alishaaga Dunia.

MIMI: Do you mean the death of Gatkuoth?
( Unamaanisha kifo cha Gatkuoth)


MOHAMED: No, I mean the death of someone who resembles you everything
( Hapana, namaanisha kifo cha mtu aliyefanana na wewe kilakitu)

Hakukua na haja ya kuumiza kichwa sana kwani kwa sentensi hiyo ni wazi kabisa mimi ndie nilikua nikifanana na Gatkuoth kila kitu.

Mohamed alimalizia kusema kuwa nina nguvu na nina akili timamu tofauti na yule aliyemuona mara ya kwanza hivyo basi nachopaswa kufanya ni kutumia akili zangu pamoja na nguvu zangu ili kutoka kwenye mtego ambao nimekua nikijiingiza kila siku.

Alidai kupitia mtego ule naweza kujiingiza kwenye matatizo makubwa sana ambayo yatanigharimu kuanzia mimi, ukoo wangu wote na mbaya zaidi ata kwa nchi yangu ambayo ni changa sana kwenye mambo yale.
Apa niliwaza jambo moja, kwani Mohamed alikua ni mlinzi tu pale kwenye lile jengo je aliwezaje kujua habari za kifo cha Gatkuoth.

Niliamua kujiondokea japo nilifika hapo kwa mbwembwe nyingi lakini kwa namna nilivyoondoka niliondoka kwa upole sana kwani maneno ya Mohamed ni wazi yalidhoofisha.

Haikunichukua muda mrefu kutoka floor ya mwisho juu kabisa ya jengo Mpaka kufika kwenye floor iliyokua na apartments ambayo ilikua inatumiwa na fatemeh.

Kitu cha kufurahisha baada ya kuingia ndani nilimkuta fatemeh akiwa amekaa kwenye kiti as if alikua ananisubiri kwa hamu sana nitoke kwenye ile safari yangu ya usiku usiku.


Baada ya kumkuta fatemeh kwenye pozi lile niliishiwa nguvu kabisa huku nikiwaza namuongopea kwa namna gani ili anielewe.

Kwa maneno machache sana fatemeh aliniomba kwa kua nimeshindwa kuwa muelewa basi kesho itakua siku ya mwisho kwenda kwa shahzad. Hivyo nachotakiwa kufanya ni kumueleza shahzad ukweli kwamba muda wa mimi kuendelea kuwepo Tehran umeisha natakiwa kurudi bongo.

Fatemeh alisema ameamua kufikia muafaka huo kwa kua ni heri nusu Shari kuliko shari kamili. Hivyo hatonipa nafasi ya kuongea lolote zaidi ya mimi kwenda kupumzika nikiwa najua kua kesho shahzad anatakiwa kumaliza program zote.

Alimalizia kwa kusema kama shahzad atasema hizo program zilizobaki zitatuchukua zaidi ya siku moja basi ata mlipia nauli na kilakitu ili tu nifuatane nae tuje wote bongo.
Fatemeh alisema kumbe javier alikua yupo sahihi sana kupitia matusi yale na maneno yote machafu kwangu. Ata yeye tayari alisha thibitisha kuwa kuna namna nina walakini kwenye uelewa wangu.

MIMI: But I didn't get out in search of women
( Lakini sikutoka nje kwa ajili ya wanawake)

FATEMEH: i don't give a f***
( Hainihusu na sijali)

Kwa mara ya pili ndani ya siku moja niijiona kabisa nimemkera binti huyu kwa viwango vya juu sana.

Kabla sijaingia kwenye chumba kile ninacholala nilijaribu kumueleza tena kama nilienda kukutana na mlinzi wa jengo lile ambae alijitambulisha kwangu kwa jina la Mohamed.

Kwa mujibu wa fatemeh alinijibu kwamba ndani ya jengo lile nisijisumbue kwa lolote Kwani sio mlinzi pekee ata mfagiaji wa mule alikua ni mtumishi wa idara ya MOIS.

Hivyo basi kwa majibu yale tu nikagundua hata Mohamed ni walewale machalii wa MOIS, na nilithibitisha hilo pia baada ya kukumbuka maneno ya Mohamed juu ya kifo cha mtu aliyefanana na mimi.

Nilibaki na swala moja kichwani, ilikuaje ndani ya idara moja watumishi wapishane taarifa. Yaani kwanini Mohamed ajue kuhusu kifo cha Gatkuoth wakati huohuo fatemeh ambae ndio alikua kwenye eneo husika asijue chochote kuhusu kifo cha Gatkuoth.

Lakini pia kwa namna nilivyokaa apo na fatemeh ilionekana wazi treatment ya fatemeh ni ya tofauti kabisa na wale wengine kwenye jengo hilo. Fatemeh aliwekwa under intensive care yaani kila alichofanya kiliratibiwa na watu ambao hatukuweza kuwajua je!! Huyu fatemeh ana nini hasa.
 
Siku hiyo usiku ulikua mrefu sana ukilinganisha na siku zote nilizowahi kukaa kwenye nyumba hiyo toka nimeingia jiji hilo la Tehran.

Sababu ya usiku huo kua mrefu ilikua ni kwa namna nilivyolala nikiwa na mood mbaya iliyosababishwa na kumkosea mwanadada fatemeh.

Baada ya kukucha nilitoka chumbani mapema sana nikitarajia nitakua wa kwanza kuamka. Lakini nilimkuta fatemeh akiendelea na shughuli nyingine na hili lilidhihirisha kwamba aliamka mapema zaidi.

Nilishindwa kabisa kuleta masiala yangu ya kilasiku kwa namna nilivyomuona fatemeh alivyosiku ile. Userious wake uliongezeka kwa viwango vya SGR ( jokes) kiasi kwamba hata Salam yangu aliipokea as if tumeonana jana yake.

Kwa mood aliyokua nayo fatemeh asubuhi ile sikutaka kuendelea kuwepo Ndani ya nyumba ile kwa muda huo hivyo nilikua natafuta namna nzuri ya kumuaga mapema zaidi ili nikamalize siku yangu kwa mzee shahzad.

FATEMEH: you can't leave without having a breakfast
( Huwezi kuondoka bila kupata kifungua kinywa)

Ni kama fatemeh aliyasoma mawazo yangu kwa Wakati ule, kwani kitendo cha kuniambia kuwa siwezi kuondoka bila kupata kifungua kinywa ni wazi alijua nilikua natafuta timing ya kuondoka ndani mule.

Na ni wazi alijua nimeogopeshwa na namna alivyoniwekea sura ya ukauzu iliyonifanya nishindwe ata kumsogelea kama ilivyo kilasiku.

FATEMEH: Congratulations, i finally discovered something in my department
( Hongera sana umenifanya nimegundua kitu kwenye idara yangu)

Fatemeh alisema pia amekumbuka kauli yangu ya siku ya kwanza Tunaingia ndani ya apartment ile, nilimwambia kuwa hatujakutana kwa bahati mbaya mimi na yeye.

Alisema kuna jambo ameligundua Ndani ya idara yake na pasipo mimi ingemchukua mda mrefu sana kuligundua swala hilo hivyo ananishukuru kwa kutokusikia kwangu.

Nilijaribu kumuuliza ni jambo gani hilo Lakini alidai niende kwanza nikamalizane na shahzad kisha nikirudi na yeye atakua amemaliza jambo lake ambalo amelianzia utafiti kuanzia usiku wa jana.

Wakati huu ni kama fatemeh alianza kubadilika na kuonyesha sura ambayo nilikua nimeizoea masiku yote ya apo nyuma.

FATEMEH: stop being a chicken,
( Usiwe muoga muoga)

Samahan napenda kutumia lugha au maneno ambayo yalikua yanapendwa kuzungumzwa na fatemeh moja kwa moja.

Fatemeh akiwa kwenye sura ya tabasamu alinicheka na kusema kwamba nimeonyesha udhaifu mkubwa sana kama mtoto wa kiume. Alidai amenuna dakika 10 tu kidume nimepanga kukimbia nyumba mbaya zaidi nakimbia na chai.

Apa alidai kwa taratibu zile au uoga ule niliouonyesha alafu najifanya nataka kumuoa niko serious kweli!!!
Niliishia kucheka tu kwakua kila alichokiongea kina ukweli zaidi ya asilimia 98 kwani ni kweli kabisa nilipanga kutimkia kwa mzee wangu shahzad asubuhi asubuhi.

FATEMEH: would you mind if I follow you (Tanzania)
( Utapenda kama nikikufuata Tanzania)

Duuuuh apo nikawaza naota au ni kweli fatemeh anamaanisha anachokisema, kwa mujibu wa fatemeh alisema akimaliza jambo lake ambalo amelianza atahitaji kupumzika mbali kabisa na Iran hivyo amechagua kuja bongo.

Ila kwa sharti moja tu hawezi kuishi hotel yoyote ile hivyo atahitaji tupate nyumba ambayo itakua pembeni kabisa ya mji.


Kwa haraka haraka unafikiri ningekataa kuja nae bongo, ahh ahh aaah yaani kwa kuwa hamjawahi kumuona fatemeh niseme hana tofauti na wa Sudan wa muhimbili.

Apo bwana kuna mawazo yakanijia hususani yale yaliyohusu team zetu za mpira za afrika, yaani nilisema away nimetoa suruhu lakini tukienda kwa mkapa hatoki mtu.

Na ni kama fatemeh alijua nawaza nini aliniangalia usoni akatabasamu kisha akanipiga busu zito na kunikaribisha kwenye meza ya Breakfast.

Fatemeh kama alibadilika ghafla sana asubuhi hiyo hivyo nilitamani kujua ana mpango gani ambayo anausuka kuhusu yeye na idara nzima ya MOIS. Kwani wakati tunaendelea na kifungua kinywa alisema mpaka asubuhi hiyo misheni yake aliyoianzisha usiku imefikia asilimia 75.
Kwa maneno marahisi ni kwamba mpaka asubuhi hiyo safari ya kwenda Dar na mimi imefikia kwenye takribani asilimia 75 ikamilike.

Kwa mujibu wa fatemeh ni kwamba alihisi kuna namna anatumika Ndani ya idara hiyo, hivyo siku hiyo amepanga kwenda kuonana na director moja kwa moja.

Hivyo basi akitoka kwa director atakua amepata majibu ya kumridhisha kulingana na kile anchokifanya idarani apo.

Kwa maelezo mafupi ya fatemeh alisema hizi idara za inteligensia sio kwamba kila anaefanya kazi ndani ya idara hizo anakua ni spy au jina jingine huitwa field agent. Hapana wapo wanaoajiriwa kwa shughuli nyingine nyingi kulingana na professional zao.

Idara hizi kuna kipindi zina ajiri engineers, computer programmers na taaluma nyinginezo kwa malengo ya kuchambua (uchambuzi yakinifu) wa taarifa ambazo field agent huzikusanya.

Sikua nimeelewa logic ya fatemeh baada ya kunielezea utaratibu huo ambao hapo awali sikuwahi kuujua kabisa.

Ila kwa maneno yale ya asubuhi ile nilielewa jambo lingine ambalo ni, kumbe bwana unaweza kuwa agent wa agent, apa namaanisha unaweza kutumiwa na agent ili tu kukusanya taarifa ambazo agent anaetambulika na idara anajua unaweza kuzipata.

Kwa lugha ya kisasa tunaweza kusema kuwa unakua chawa wa spy, yaani spy au field agent anakutumia wewe ili kupata kupata taarifa anazozihitaji.

At least asubuhi ile mood yangu ilianza kurudi baada ya kumuona fatemeh na yeye ameanza kukaa sawa na sio emotional tena kama alivyokua wakati tunaamka.

Fatemeh alinisisitiza nichangamke kwani muda si rafiki, natakiwa nionane na shahzad mapem zaidi ili kuhakikisha tunamaliza kilakitu kwani sitokuwa na nafasi nyingine ya kurudi kwa mzee huyo.

Baada ya kuwa nimeshajiandaa usafiri ulifika kama ilivyokawaida gari yetu ni ileile ya kilasiku. Nilitoka kwenye apartments zile huku nikiwa siamini kama ni kweli naenda kuonana na shahzad kwa mara ya mwisho.

Muda tunaoutumia tukiwa barabarani huwa sio muda mwingi kabisa kwanza kutokana na speed au mwendo kasi wa gari lakini pia hakukua na umbali kiiivyo kutoka kwenye jengo la apartment mpaka kwa shahzad.
Familia ya shahzad walishaanza kunizoea japo tulikua tunapishana sana kwenye mawasiliano ya lugha. Lakini mjukuu wake na shahzad ndio alionekana kunizoea sana kwa kuwa tulishaanza ku interact apo kabla.

Jambo lingine lililo rahisisha mazoea baina yangu na mjukuu wa shahzad ni kile kitendo cha mjukuu huyo kuweza kuzungumza lugha ya kingereza. Hivyo basi uwezo wake wa kuzungumza lugha hiyo ndio ulifanya aendelee kutengeneza mazoea na mimi kila uchao.

Siku hiyo shahzad alishatangulia mapema zaidi kwenye ile maktaba ya nyumbani ambayo ilitumiwa na familia yake. Hivyo basi nilipofika niinyoosha moja kwa moja mpaka maktaba.

Wakati naelekea maktaba nilisindikizwa na mjukuu wa shahzad ambae baada ya kufika ndani ya chumba kile cha maktaba shahzad alimpa ishara ya kuondoka akitaka atupishe tuendelee na program yetu.

Baada ya Salam tu, nilianza kumpa maelezo yote kama nilivyoelekezwa na fatemeh kuhusu uharaka wa safari yangu.

Nilimwambia shahzad kuwa muda wangu wa kuendelea kuwepo Tehran umeisha hivyo natakiwa kurudi tena Tanzania kuendelea na majukumu mengine.

Kwa mujibu wa shahzad alisema ata yeye alitamani sana kujumuika nami tena kwenye project hii tatizo umri ulishamtupa mkono vya kutosha sana.

Alidai anaona kabisa naenda kufanikiwa kwenye hii project kwa kuwa tu dunia ilipofikia technology ipo juu sana na wataalamu wa archeology wapo wengi hivyo hakuna sehemu tutafeli kwenye project hii.
Kwa upande wake alisema kwa kua nimekua na haraka sana basi atajitahidi kufupisha kila kitu ili tu amalize maongezi yale. Na mwisho wa maongezi aliahidi kunipa vyote alivyoahidi kunipa ili tu vinisaidie kwenye mchakato mzima.

Baada ya sentence hiyo nilimkumbusha kuhusu pete ambayo alisema ni kitu cha kwanza cha muhimu sana. Alisema umuhimu wa pete hiyo tutaujua pale ambapo tutaona link itakayokuwepo baina ya watawala wa bahari na ulimwengu wa roho zetu za kibinadamu.

Mwisho alimalizia kwa kusema kuna mtu mmoja ambae nae kwa muda mrefu alikua anapambana kuelekea mji huo. Hivyo ameshampa taarifa mtu huyo kuhusu mimi hivyo basi mtu huyo atakua tayari kuungana na mimi ili kuelekea kwenye safari hiyo ya kuitafuta mali ya rapta.


Kiukweli sikua tayari kumpokea mtu yoyote ili kuungana nami kwenye project hiyo, lakini nilishindwa kuliweka wazi jambo hili mbele ya shahzad kwani angeniona mimi ni selfish.

Na hapo tungerudishana kulekule tulipotoka na bwana Javier kuhusu waafrika na roho zetu.

Hivyo nilimuuliza shahzad swali moja tu

MIMI: je Bwana huyo amekubali kuchangia gharama za mradi kuanzia mwanzo mpaka mwisho?

SHAHZAD: nitawakutanisha nyinyi wawili alafu mtajadili mpango mzima mnauendeshaje.

Sikutaka kuonyesha kama nimeingia unyonge kwa taarifa ile ila kiukweli ile taarifa ilinidhoofisha sana.

Baada ya taarifa hiyo ambayo ilihusu mtu nitakae enda kushirikiana nae huko rapta, shahzad alinipa ramani nyingine ambayo alidai ilichorwa na watangulizi wake wa awali.

Alidai ramani hiyo ndio kila kitu kuhusu mahala sahihi ulipo mji huo wa rapta, ramani ile ilionyesha pwani ya afrika mashiriki iliyojaa visiwa vingi viogovidogo na vikubwa.

Ramani hiyo ilichorwa miaka mingi sana baada ya kuwa mji wa rapta umeshazama tayari majini. Waliochora ni wale watangulizi wa familia ya Shahzad baada ya kuwa wamefika na kuuona mji mahala ambapo mji ulishazama.

Kwa mujibu wa shahzad ni kwamba ramani hiyo ilihifadhiwa pale kama kama hazina kubwa na pekee ya familia. Lakini alijitolea tu kunipa mimi kwa upendo hivyo alisisitiza ikitokea tumefumania chochote huko basi familia ile tusiisahau kabisa.
Ramani ile ilionyesha kitu gani na ni zipi sababu za kupotea kwa mji huo.



KULE WHATSAPP TUMEBAKI NA EPISODES 3 SIMULIZI IISHE
(Tunachangia buku tatu 0623 329512 )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…