Utajiri wa nchi ni akili za Watu sio rasilimali kama madini na nyinginezo

Bara la Afrika Ina watu takribani billion 1.35 Taifa la Uswis lina watu million 8.97 Taifa la Uswis kiuchumi linabeba bara Zima la Afrika kwasababu Africa imebeba mabilioni ya watu wajinga.

Kiukweli maendeleo ni rasilimali watu wenye ubongo pevu na si vitu
Hongera mleta mada
 
 
Ongezea hapo wanakata miti halafu wanaitisha Dua kuombea mvua[emoji23][emoji23][emoji23]kama sio kurogwa ,Mungu anatuona jinsi tulivyoenda kinyume na nature.

Hahaaa wanakata miti kwanza kosa waweke juhudi ya kutunza mazingira kwa sheria kabisa kwamba kila mji lazima uwe na miti ya matunda hata miwili, taasisi zote shule zote nanserikali nanprivate lazima ziwe na miti, hospitali zote lazima ziwe na miti ya kutosha, makanisa na misikiti lazima wapande miti, masoko yote lazima yapande miti isiyopungua 25 au 30 , lakini anasubiriwa mwamposa aombee mvua
 
We are rich in natural resources but poor in terms of quality human resources and financial muscles.
Kwani wewe unaelewa nini kuhusu utajiri?
Achana na Eurocentric view fikiri kwa Afrocentric view utapata picha pana.
Hao unaowasifia Wana akili hawana huo utajiri na ndiyo maana walikuja huku kuuchukua kimabavu.Ni sawa na wewe umepigika na life town,alafu unapata fununu kuwa kule Nyamongo Mkanda wa madini umetema,utabaki mjini na akili yako au utaenda kusaka utajiri???
 
Sasa kama wanaume 10 weupe walikuwa wakivamia kijiji cha watu 2000 halafu wanaume wote kijijini wanakimbia na kuwaacha wake zao wabakwe hamuoni kuna kitu hakipo sawa hapo?
 
Vitu vyengine ni mifumo tu mibovu na kukosa uzalendo na si kwamba hatuna akili, mikataba isiyo na manufaa kwa taifa ni vitu ambavyo sio kwamba wenye kufanya hivyo hawana akili au hawajui wananachokifanya.
 
Chakufanya;
I. Tujifunze kuwa na Akili ili tuwe nchi yetu itajirike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mada imekushinda toka mwanzo hadi mwisho! Sasa kama umeficha madini hapo katikati ambapo sikupasoma kwa kukosa uvumilivu na niliyosoma mwanzo mwa mada na mwisho wake, lawama ni yako kwa mtindo wako mbovu wa uandishi.

Niliposoma kichwa cha habari tu, nikavutiwa sana na kutaka kujuwa yaliyomo ndani ya mada yenyewe.

Mstari wa kwanza tu, nikaona mada imepinda. Sikukata tamaa nikajikaza nivute subira. Nikasoma hadi nusu ya andiko; nikaishia hapo. Sikuwa na nguvu tena za kuendelea hadi mwisho wa andiko refu lisilokuwa na mvuto kulisoma.
Lakini nikawa na wasiwasi kwamba pengine nikiruka hadi kule mwisho nitakuta mambo yanayohusiana na kichwa cha mada yenyewe, hata kama itakuwa ni katika mhitasari tu!

Looo, sikuona kitu. Nikaamua kunyanyua hayo niliyobamiza hapo juu kwa kuwa 'disappointed' na mada nzima, isipokuwa kichwa chake cha habari tu basi!

Pole yako ya kuwa na muda wa kupoteza, na pole yetu wasomaji wako kwa kupotezewa muda.
 
Sasa kama wanaume 10 weupe walikuwa wakivamia kijiji cha watu 2000 halafu wanaume wote kijijini wanakimbia na kuwaacha wake zao wabakwe hamuoni kuna kitu hakipo sawa hapo?View attachment 2418903View attachment 2418904View attachment 2418915
Wewe, 'mkulu senkonda' si mtunzi wala mwanzilishi wa haya uliyoyaweka hapa, umeyanyanyua tu toka mahala, lakini hukutaka kuonyesha ulikoyatoa.
Unafanya kazi chafu bila ya kujuwa ni nani unayemfanyia kazi hiyo, tena bila malipo yoyote. Hii inadhihirisha wazi kabisa wewe kuwa mfano wa hao weusi wanaosemwa kwenye mada yenyewe.

Sasa kama hata huwezi kutambua kwamba Xi Jinping hawezi kusema hayo yanayosemekana kayasema, wewe akili yako itakuwa imelala kabisa.
 
Hizo akili km waliopata bahati kutuongoza km hawana hesabu maumivu
 
Umemsaidia sana mleta mada kunyoosha mada yake, lakini sijui kama anaelewa ulichomweleza hapa.
 
Acha nijaribu, hata kama sitapata jibu.

Naomba mwenyekujua, mambo manne yaliyosemwa na Mwalimu Nyerere kwamba yanahitajika ili nchi yetu ipate maendeleo.

Tafadhali yaweke hapa chini tuyapime kama yanahusiana kwa vyovyote katika kujibu maudhui ya mada hii inayojadiliwa hapa.
 
Nimesoma heading yako na content nimeona umekosea mahala, kutokana na ulichoandika kwenye content, ulitakiwa kusema kwenye heading yako inahitajika akili ya kusimamia rasilimali tulizonazo, na sio kusema tunatakiwa kuwa na akili bila rasilimali.

Mfano wa madini uliotoa, hapo umeshaonesha umuhimu wa rasilimali, kwa hiyo kinachotakiwa kuwepo ni akili za kuzisimamia, na sio rasilimali zisiwepo kabisa iwepo akili pekee kama ulivyoandika.
 
Watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora.
 
Vitu vyengine ni mifumo tu mibovu na kukosa uzalendo na si kwamba hatuna akili, mikataba isiyo na manufaa kwa taifa ni vitu ambavyo sio kwamba wenye kufanya hivyo hawana akili au hawajui wananachokifanya.

Kutokujua unachokifanya ndio kukosa akili Kwenyewe huko
 

Nchi ili ipate maendeleo Jambo kubwa kuliko yote ni Akili.
Kama Watu hawana akili hata wangeishi peponi lazima pangedorora.
 

Bila Akili hivyo vitu haiviwezi kuwa Rasilimali.
Ili kitu kiwe Rasilimali lazima Akili iwepo.

Jambo lolote lile linaweza kuwa Rasilimali ukiwa akili ipo.

Mfano, kabla ya Wazungu kuja mambo mengi hayakuwa Rasilimali, kama nawe ya dhahabu hayakuwa madini mpaka wenye akili walipokuja.

Gesi ya mtwara tupo nayo miaka nenda Rudi lakini hatukujua kama ipo na hata tungejua tusingejua matumizi yake Kwa sababu hatuna Akili.


Akili ndio hukipa kitu thamani, kitu chenyee Kama kitu hakina thamani mpaka akili ikipe thamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…