FATHER OF REALITY
Senior Member
- Nov 3, 2014
- 123
- 100
Nadhani umeandika hoja MUHIMU yenye kushika hisia, na hivo kuna hatari ya kuzuia fikra yakinifu, tusipokuwa Makini wote tutashiriki kujilaani, kulaumu watu na kukosa hata mawazo suluhishi.
Katika kuelewa Jambo ili ulihukumu yapaswa akili na fikra yakinifu vishirikiane.
Mimi naungana na wasemao Tanzania ni tajiri sana Kwa minajiri ya rasilimali tulizonazo, bali tunaishi katika umaskini. Nadhani aliyetoa hoja hii na hata wengine walosimamia walibeba lengo jema la kuamsha tujitambue na tutazame tumejikwaa wapi ili ikiwezekana tujisahihishe ili tuanze mkakati wa kuutumia utajiri ghafi wa nchi kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa nchi na watu wake.
Natoa mfano; mwanafunzi ambaye anafeli sana mitihani lakini mwalimu wake akatambua kuwa ni mwenye uwezo mkubwa wa kuweza kufanya vizuri katika masomo yake, ili kumepower huyo mwanafunzi mwalimu atamwambia wewe ni mwanafunzi mwenye uwezo kimasomo, kisha atamweleza wapi anakosea na achukue hatua zipi, wewe usikiaye, tena Kwa kukosa tafakuri utambeza mwalimu Kwa kutazama matokeo ya sasa, ni ujinga Tu unaokuendesha, au wewe mtumwa sehemu fulani na umeaminishwa kwamba jamii yenu ilizaliwa kutumikishwa na kuishi katika hali ya umaskini, kisha anakuja mwenye akili anayetambua ukweli juu ya asili yako kwamba waweza kuwa huru na ukatafuta Mali hata kuwa tajiri na kutawala wengine. Mtu huyu ameenda mbali zaidi akijua historia ya vizazi vyako kwamba walikuwa wafalme, machifu na watu wenye utajiri mkubwa, mtu huyu atakuamsha Kwa kukuambia hivi wewe ndugu unafahamu kwamba WEWE NI MTAWALA WALA SI MTUMWA NA PIA WEWE NI TAJIRI SANA? That is an alert to you to discover yourself it makes you aware na itafanya uanze kujitafuta wapi ulikosea hata kuwa na hali hii, hiyo ni empowering of one self. Inatumika Kwa wachezaji, mwanasiasa mwenye kipaji hicho pasipo kukitambua n.k. Ni Sawa na kuona kipaji cha mtoto juu ya muziki na ukamwambia hivi unafahamu kuwa wewe ni zaidi ya mwanamuziki Fulani ( maarufu na mwenye mafanikio) Sasa ukiwa mjinga utaishia kubisha kwamba yule mtumwa si mtawala wala si tajiri ni masikini tu, au yule mtoto si lolote si chochote katika muziki, na kwa wakati huo ni kweli juu ya Hali zao hao.
Hii ni kukosa akili pembuzi iwezayo kutafsiri na kuchanganua maudhui ya Jambo fulani na nguvu ibebayo kufanikisha Jambo husika. Hiyo ndo akili ndogo, pia ni ujinga.
Hebu fikiria kidogo, tutegemee mawazo yako uliyoandika kukomboa taifa toka umaskini, tunatokaje, hata ukiitwa ushauri utashauri nini zaidi ya kubariki mzungu aliyekulaani Kwa kukufananisha na nyani.
Kuna tatizo kubwa sana juu ya sisi wabeba hoja tudhaniazo ni hoja jadidu na yakinifu, tatizo hili ni kutetea au kulaani jambo pasipo uelewa wa kina, kwa mfano unayoyasema juu ya jamii zetu, kuwa wachafu, wasiojali mazingira, tegemezi, wenye kulaumu laumu tu, walojaa ubinafsi, watesi juu ya jamii yao wenyewe na mwingine mengi. Naandika tena Kwa herufi kubwa, HAKUNA JAMII YOYOTE ISIYOPITIA HAYO, HAIPO DUNIANI HAIPO. Kikubwa wao hawakujilaani, na kwa bahati hakuwepo wa kuwalaani, wakasumbuliwa na hayo huku wakitafuta namna ya kujikwamua.
Cha kusikitisha ni pale mleta hoja nadhani kwa ujinga tu au Kwa hasira juu ya mawazo fulani inatolea mfano jamii zilizoendelea kama kwamba zilizaliwa hivyo, brother kuna kazi imefanyika na ilianzishwa na wachache wenye fikra yakinifu, ndugu yangu HAKUNA JAMII YENYE WATU WAADILIFU NA WENYE AKILI TUUU PASIPO JUHUDI ZA WACHACHE WENYE KUTHUBUTU KUFUTA UJINGA WA WENGI.
Hivi unafahamu waafrika wengesema watu wa jinsia moja waoane kinyume kabisa na nature, tungeitwa hata mavi, Hilo kwako si shida, hawa watu wamepitia mengi maovu, ujambazi ulokithiri, kupigania uongozi, Vita vya kiraia, uuwaji watu wadhaniwao kuwa wachawi, vipindupindu, kunya bila kujisafisha na mengineyo.
Nini kifanyike. HAMNA HAJA YA KUJILAANI. Tunaweza kujikwamua toka ujinga huu na umaskini huu Ila si Kwa kutegemea mikakati ya wengine ambao kimsingi ni wafaidika wakubwa wa rasilimali zetu, tuweke malengo yetu wenyewe kama ni elimu tuwe very selective and serious tukitengeneza mitaala itayolenga utumizi mzuri wa rasilimali zetu, Pia kubadilisha mtazamo juu yetu wenyewe, kuwa na utashi wa kisiasa hili halitafanikiwa over night ni mchakato mfano kuandika au kuigiza mawazo ya namna ambayo yataamsha watu na kujitambua. Sisi waandikaji tuandike pasipo kuchoka, watu watakapochoshwa na kuona hatma ya maisha yao ipo mashakani watajitafuta kwa kurudia maandiko kama haya, historia yao na kutafuta wapi wamejikwaa.
Angalizo: Kwa mitazamo tuliyonayo sasa hasa wasomi na wanaodhani kuwa wanaharakati wa taifa hili, HATUTAMUELEWA KIRAHISI ALIYEBEBA MAONO YA KWELI YA KUJIKWAMUA TOKA MADHILA HAYA. Maana matatizo yetu ni complex alafu tunakazana kuyatatua kwa simple means.
Ukikuta wasomi wanavoainisha mbinu za kufikia maendeleo ya kweli na kufuta umaskini, utaona ni raisi mno, na Kwa mtindo huo basi nchi zote zingekuwa zimejikwamua toka umaskini na kuwa tajiri.
Naamini njia za maendeleo si njia nyeupe na za wazi, na yeyote azijuaye wanyonyaji wetu hupiga kelele usiku na mchana wakituaminisha huyo siye.
Wengi walozitoa nchi zao walau kwa kiwango fulani na kufanya zijitegemee, hawakufuata njia za uchumi kwa mazoea.
NAAMINI SOTE TUNA LENGO MOJA, NA HIZI NDO HARAKATI ZA KUJITAFUTA TUMEJIKWAA WAPI.
Tusijibanze nyuma ya uhasama wa kisiasa, tuwe watumwa wa ukweli tutachambua pasipo kupepesa.
Akili zipi ni akili kweli katika kujikomboa kutoka umaskini na ujinga tuuishio sasa. Hilo nadhani ni swali kwetu.
Niaminivyo hata hawa viongozi wetu huwa nadhamira ya kujiondoa katika MADHILA HAYA Ila hukwama katika njia, na wengi huchagua kukomboa maisha yao Tu. Ili tuendelee tunauhitaji njia zote, huo ndo ukqeli, yaani njia halali na haramu, busara na uwehu, upole na unabe, demokrasia na penginepo pasipo demokrasia, mawazo shirikisho na muda mwengine wazo la kijasri pasipo ushirikiahaji, kufuta Sheria na pengine kuvunja Sheria, ukweli na uwazi na pengine uwongo na uficho, yote yalenge kujenga taifa na watu wake. Maendeleo ni Complex by nature.