Utajiri wa nchi ni akili za Watu sio rasilimali kama madini na nyinginezo

Nchi hii ina mambo, mfano kisiwa cha Ukerewe kimezungukwa na maji baridi safi ya ziwa Victoria. Lakini wakaazi wanalalamika ukame, bei ya vyakula kuwa juu n.k

Je uongozi wa mkoa wa Mwanza wameshindwa kukigeuza kisiwa cha Ukerewe kuwa shamba-darasa kwa kuwawezesha wakulima wote kufanya kilimo cha umwagiliaji chanzo kikiwa ni ziwa hilo lilolizunguka kisiwa hicho chote.

Nina uhakika kisiwa hicho kinaweza kuzalisha mazao ya chakula kwa wingi kwa kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji, na kutumia tunu alioijalia kisiwa hicho kiwe mfano kwa uzalishaji mkubwa wa nafaka kama nchi ya Ukraine.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe​



Kilimo​

Mazao yalimwayo kwa wingi katika Wilaya ya Ukerewe yenye visiwa 38 japo visiwa 15 vinatumika kama maeneo ya uvuvi ni muhogo, viazi vitamu, mpunga, matunda aina ya machungwa, maembe, mananasi, mapapai, kahawa, migomba, mazao ya

bustani na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage, njugu mawe na kunde. Mazao mengine yanayolimwa kwa kiasi kidogo ni mtama na rosella (choya). Mazao haya yanalimwa katika eneo la Ha.33, 765.5Ardhi iliyopo ni ndogo kuruhusu kilimo cha kupumzisha mashamba. Kwa hali hiyo kilimo kinahitaji kifanyike kwa tija ili uzalishaji wa mazao uweze kukidhi mahitaji ya wananchi wote ambao kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ni 347,145. Zao la alizeti linatiliwa mkazo badala ya zao la pamba ambalo katikamiaka ya 1970 lilikuwa zao maarufu la biashara ambalo lilikuwa linawapatia wakulima kipato. Lakini kutokana na upungufu wa ardhi hasa ukizingatia kuwa zao hili halitakiwi kuchanganywa na mazao mengine pamoja na kushuka kwa bei, zao hili lilionekana kutofanya vizuri.
Idara ya Kilimo ili iweze kutekeleza vyema ilani ya Uchaguzi ya CCM ni lazima ihakikishe inatekeleza majukumu mbalimbali ya msingi ili kuleta tija katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, kuendeleza na kuboresha huduma za ugani ikiwa ni pamoja na kuwezesha wakulima kuwa na vyama vya ushirika vilivyo hai na vyenye nguvu ya mtaji. Aidha kuwawezesha wakulima kuunda vikundi ili waweze kuwa na umoja wenye nguvu katika kufikisha bidhaa zao katika masoko ya mazao yao. Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ina jumla ya Vyama Vya Ushirika 71 vilivyoandikishwa chini ya Sheria Na.6 ya mwaka 2013 ya Vyama Vya Ushirika. Idadi ya VICOBA vilivyopo ni 150. Vyama vilivyo vingi vinakabiliwa na matatizo mbalimbali ambayo yanapelekea vyama hivyo kutofanya vizuri. halmashauri inakabiliwa na upungufu wa wataalam 4 wa Ushirika kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji wa vyama hivyo ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa mahesabu. Ili haya yaweze kufanyika kwa ufanisi Maafisa Ugani wanatakiwa kuboreshewa mazaingira yao ya kufanyia kazi. Maboresho hayo ni pamoja na kupatiwa nyumba za kuishi katika maeneo yao na kuwezeshwa vyombo vya usafiri hususani pikipiki ili kuwawezesha kuwafikia wakulima kwa urahisi na kwa muda muafaka pale huduma za ugani zinapohitajika.

Pamoja na Serikali kutilia mkazo juu ya kilimo cha umwagiliaji wakulima bado wanategemea mvua katika kilimo. Hii ni kutokana na kutokamilika kwa miundo mbinu ya umwagiliaji katika skimu za Bugorola na Miyogwezi. Miradi hii imekwamakukamilika kutokana na ukosefu wa fedha licha ya Ofisi hiyo ya Umwagiliaji

Source : Kilimo
 
Ujinga mtupu yaani tuna raw materials za kila aina lakini kutwa tunaomba misaada Ulaya, sababu kubwa ni kukosa akili
Ukitaka kujua hii nchi imejaa wapumbavu , tumeshindwa kutumia hata chuma kule Liganga na mchuchuma kuanza kuzalisha bidhaa za kilimo ,ujenzi nk ili tuondokane na utegemezi wa bidhaa toka nje ya nchi ambapo tunapoteza pesa nyingi za kigeni , wapumbaf huko serikalini ukiwauliza watakupa visingizio vya kiduwanzi mpaka utatamani kulia .
 
Kila binadamu ana akili.

Tutofautishe akili na nyanja za fikara kama kuchakata data, kufanya maamuzi, kuhifadhi kumbukumbu, kukariri maarifa, kuthamanisha vitu, kuvumbua mambo mapya, kujenga taswira kubwa kutoka kwenye mambo madogo au kupata vingi kwa kutumia vichache, na kutumia yote haya kutatua matatizo kwenye maisha kwa ujumla.

Suala ni kuwa akili za watu wetu zimekuzwa na kuendelezwa katika maeneo gani ya fikara?

Tusisahau kuwa binadamu wenzetu waliotangulia kujiendeleza kwenye hizo nyanja kwa sababu ya changamoto za kimazingira walichukua hatua za makusudi kabisa kutudumaza kifikra na mpaka leo, wengi wetu hatujaweza kujikomboa kwenye hicho kifungo. Kinyume chake maelfu ya watu wetu bado wanazidi kujipeleka kwenye hivyo vifungo na kuwashawishi wengine pia waingie huko.

Viwango vya kukua na kuendelea kwa akili vinatofautiana pia ikiwa pamoja na mivuto mbalimbali inayowashawishi watu kuendeleza akili zao kwenye nyanja ambazo zina matokeo tofauti yakiwamo yale ambayo hayana tija ya kweli kwa jamii(nadhani kwa Tanzania hawa wapo wa kutosha).

Kwa maoni yangu,akili za watanzania wengi zimeendelezwa kiasi cha kutosha tu kukidhi mahitaji ya muhimu kama chakula, mavazi, na makazi. Kilichobaki ni akili za kiharamia ambazo hata wanyama wanazo, na zile za kusubiri ujio wa pepo( mbingu)

Kwa kuacha kukuza na kuendeleza akili zetu kufikia viwango stahiki, na kuachia zitawaliwe na watu wa nje na vibaraka wao wa huku kwetu ndio tumefikia hii hatua ya kushindwa kumiliki na kuendeleza rasilimali zilizopo kwenye himaya yetu.

Mkuu Robert Heriel, akili zipo lakini hazijaendelezwa na mbaya zaidi, zinatawaliwa na watu wasio na na nia njema kwa jamii yetu, ndani na nje ya nchi.

Lakini panga pangua, hata kama uletaji wako wa mada hii haujakidhi ladha ya kiuandishi ya baadhi ya wasomaji wako, bado uko sahihi kabisa.

Utajiri wa kwanza kabisa ni akili.
Ukikosa akili hata uwe na rasilimali kiasi gani, utaishia kuwa maskini tu!
 
Asante sana mleta hoja. Naiunga mkono 100% kwani na mie nawaza kama wewe. Waafrika ni wajinga sana yaani dumbs.. hatuamini katika akili. Serikali inategemea watu wasio na akili kuongoza.. watu wasio na akili, au wenye kufanya kazi zisotumia wala kuhitaji akili ndo wanaotumia V8. Wale wenye najukumu ya kutia maarifa na akili kizazi cha sasa kama vile walimu, wahadhili na wanataaluma wengine, hawathaniniwi.. Akili itakuja vipi na utajiri utatoka wapi?
 
Ndo kutokuwa na akili kunakuwa hivi.. pole yako sana..
Kwa Tz na Africa kwa ujumla, watu wa jamii yako mko wengi sana..

Akili, akili.... Akili ni utajiri
 
Ndo kukosa akili kwenyewe.. unaweza kuthibitisha hayo mabwawa 31 yako wapi exactly? Yaani utaje location, (kijiji, kata, wilaya, mkoa).. vinginevyo hizi ni propaganda ambazo hutumika kwenye mataifa yenye watu wajinga.. yaani (dumb nation)

Hayo mambo ya Kidunda ni uwongo, uwongo uwongo.. mmekalia uwongo, mnakula uwongo na mnanuka uwongo..
Poor you!
 
Kweli akili ni mali.. ambayo bahati mbaya wewe huna.. ukame katika eneo hili la Africa ni kitu cha kawaida, na kimsingi kila baada ya miaka 5, lazima itokee ukame kwa miaka 2 hadi 3.. hii iko hivyo na inajulikana na watu wenye akili miaka kibao iliyopita.. serikali inaongozwa kwa kiwango kikubwa na watu wasio na akili.. kwa hiyo kwao fact kama hii ni vigumu kuiona, wao na maccm wanajitetea kuwa ukame haujaletea na ccm.. hapo ndo utagundua akili zilivyo chache kabisa..

Lazima kifanyike kitu..
Akili haiji tu kiholela.. lazima watokee watu wachache wenye akili, wafanye mabadiliko ambapo nchi itawekeza katika kukuza akili ya watu wake.. sasa hili halifanyiki kabisa..
V8 moja na gharama za uendeshaji wake kwa miaka 2 ni sawa na gharama za kujenga shule moja nzuri ya msingi.. sasa jiulize zipo V8 ngapi? Hapo ndo ujuwe tunaongozwa na mapopoma.. yaani zero concept


 
...Maendeleo ni Complex by nature....

Umeandika mengi.. na pumba zikiwemo..
Maendeleo ni sayansi na wala siyo complex kama uavyotaka tuamini. Maendeleo ni CHOICE.. ili ufanye 'the right choice' lazima uwe na akili.. jambo ambalo mleta hoja amejikita kwalo.
Tz na Africa kiujumla tunashindwa kufanya right choices kwa sababu communities zetu hazina akili au haziko tayari kutumia hata akili kidogo iliyopo..
 
Sasa wewe mwenye akili mbona matumizi ya akili yako ni ulalamishi tuu nothing else..

Hizo Ni akili au matope?
 
Wewe Ni mpumbavu nianze kukuthibitishia hujui kwa kupata habari? Sasa una akili gani Kama nimekueleza wizara husika ambako unaweza kupata specific areas bado unaongea ufala..

Mapopoma Kama nyie mna akili za kwendea chooni na kulalamika tuu Hakuna kingine,wakati Serikali unasema imejenga Vituo vya Afya 234 vya Tozo mlikuja na upumbavu Kama huu huu ooh viko wapi mkapewa orodha mkapata aibu na kuanza kutafuta visingizio Mara ooh havifanyi kazi Ni majengo tuu na upuuzi mwingine Kama huu..
 
Nchi imejaa matapeli tupu
 
Unaonesha ulivyo first order dumb.. nimekuuliza hayo mabwawa 31 yako wapi exactly?
Anyway sitaki kupoteza muda kujibishana na dumb a§s kama wewe, form four failure flani hivi
 
Unaonesha ulivyo first order dumb.. nimekuuliza hayo mabwawa 31 yako wapi exactly?
Anyway sitaki kupoteza muda kujibishana na dumb a§s kama wewe, form four failure flani hivi
Na Mimi nikakwambia Kama hujui kwa kupata taarifa yaliko Basi Baki na utaahira wako.
 
Kwa kiasi fulani siungi mkono hoja zako. Akili kila mtu anazo, lakini maarifa yaliyopo kwenye hizo akili sio kila mtu anaweza kuyageuza yakawa utajiri. Nchi kuwa na resources au kutokuwa nazo sio hoja, hoja ni uwezo wa watu wa nchi husika kuzigeuza hizo resources kuwa utajiri. Akili +Elimu =Huzaa maarifa.
maarifa +resources =Huzaa utajiri.
Taifa tajiri, ni lile ambalo asilimia kubwa ya wananchi wake ni matajiri ingawa hata huko kwenye taifa tajiri na maskini wapo. Taifa maskini ni namba ya maskini ndani ya taifa kuwa kubwa kuliko matajiri 80/20 or 90/10 rule ndio huwa ina apply huko. Changamoto ya watanzania sio Akili, bali ni uwezo wa kubadili kile kilichopo kwenye akili kwa kushirikiana na resources zilizopo kuwa utajiri.
 
Ndo kutokuwa na akili kunakuwa hivi.. pole yako sana..
Kwa Tz na Africa kwa ujumla, watu wa jamii yako mko wengi sana..

Akili, akili.... Akili ni utajiri
EEeeeeHeeeee!

Sasa wewe hapa umetumia akili gani hasa!
 

Shukrani Sana Mkuu
 

Akili lazima zithibitishwe katika Mazingira ya nje. Mtu huwezi kusema kila mtu anaakili wakati hauna uthibitisho.

Uwezo wa kubadili changamoto kuwa fursa ni sehemu ya akili, uwezo wa kukabiliana na matatizo yanayozunguka jamii ndio akili yenyewe hiyo.
Sasa Kama mtu hawezi kukabiliana na matatizo na changamoto zinazomzunguka utasemaje anaakili?

Unapozungumzia Akili tayari umegusa Maarifa, ufahamu, tafakuri, Ujuzi ambayo hayo ndio yanaunda kitu inaitwa Elimu.
 
Hivi tunatofautishaje kutokuwa na akili za kufanya jambo fulani na kutoku dhamiria tu kufanya hilo jambo?
 
Mbona sioni mkitolea mifano au kulinganisha na waarabu ambao nao wametajirika kwa mafuta yao badala yake inatumika mifano ya wazungu tu au waarabu si mfano sahihi ya watu wenye akili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…