Utajiri wa 'ngende' (ushirikina) una masharti magumu kuliko utajiri wowote ule duniani

Yaani had wewe ulobahatika kwenda shule ulienda?? Aisee.
 
Formular ya pesa ni hardworking, nidhamu ya pesa, kuthamini muda, kutafuta na kubuni fursa mpya kila siku, kuhakikisha unadominate soko ya bidhaa yako, uaminifu, kua mkweli, hakikisha huduma au bidhaa yako inakua bora kwa viwango, hakikisha unakua na customer care nzuri, hapo umemaliza mengine ni mbwembwe kwa wasijiamini kwani mganga kama anaweza kukugawia utajiri kwa nini yeye afe fukara unadhani yeye anakupenda sana kuliko anavojipenda,? Wengi wao matapeli tu
 
Hii kitu hii mkuu digba sowey anasema alitapeliwa ngoja nikitulia nije kuelezea stori ya rafiki yangu ambaye ni mmakonde na ilibidi arudi kwao kuadjust.

Edit:

Nimerudi- nina rafiki tulijuana kupitia ishu za kuuza muvi mshkaji akaja akaoa baada ya muda ile ndoa ikawa miyeyusho kwakua binti akajidhihirisha kwamba anataka kuishi maisha ya juu mno.

Mume ana simu ya kawaida yeye anaingia mchezo ili afanye birthday au anunue simu baadaye zikaanza na dharau. Hapo wana mtoto mmoja jamaa akaona asikonde kwenye ndoa akaazimia kumuacha mwanamke.

Haka ni kastori karefu lakini ni kwamba akamuacha na jamaa akawa ameenda kijijini kwao kuadjust ili ofisi imlipe mimi nikaiescape hiyo proposal kwa kusema sina nauli. Mchizi kufika kule akapigwa manyanga akaambiwa kwamba kuna kitu umetumiwa na mwanamke wako kwahiyo tuanze na hilo kwanza.

Wakaanza na hilo kisha ikaja biashara kupigwa ndumba.

Akarudi akatuhadithia yaliyotokea. Biashara yake imeflourish kwa maelezo yake anasema anaweza kutengeneza 30K to 50K siku ambazo siyo J3. J3 anatengeneza kuanzia 50K to 100K.

So nafikiri ina ukweli wake na kuna hiyo chapter ya utapeli kama ya digba sowey
 
Bahati yako ulitapeliwa pesa tu ungefirw* fanyeni kazi vijana pesa za bure hakuna dunia hii.
 
Meneja ana gari kali boss anakomaa na baiskeli
 
Naomba rejea mkuu ayo mandiko
Mathayo 12


25 Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama.
26 Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?


Marko 3


23 Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani?
24 Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama;
25 na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
26 Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake, akafitinika, hawezi kusimama, bali huwa na kikomo.
 
Yaani had wewe ulobahatika kwenda shule ulienda?? Aisee.
Unajua mimi kwa ''ujinga'' wangu nilikuwa sidhani kama kuna binadamu tena kijana aliyesoma anaweza kuamini hayo mambo ya ''ngende'' na utajiri. Kumbe hata meseji za kitapeli zinazotumwa kwenye simu huwa zinapata ''mabwege'' wa kuliwa. Hata huyu mwanzisha thread anatafuta bwege wa kumliza na huenda kabisa akapata wengi. Kweli dunia ni mzunguko.
 

Ukweli elimu tuliyoipata haijatusaidia hata kidg...huyu bwana kwa mujibu wa maandiko yake ni mwalimu..duh💣
 
duh, ya kweli mkuu!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…