Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
⚡🥂Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 07.
Kwakuwa Mwakisaka ndiye aliyekuwa mwenyeji wangu sikuwa na hofu kabisa kwasababu ni mtu ambaye tulifanya nae kazi kwa muda mfupi na alikiwa mtu mwema,baada ya kufika kivukoni(feri)tulikata tiketi za kivuko na tukawa tumefanikiwa kuvuka ng'ambo ya pili,baada ya kufika upande wa pili yaani Kigambo,jamaa aliniambia inapaswa tupande gari zilizokuwa zinaelekea Kibada kwa kuwa ndiyo njia yenyewe hiyo.
Tulifanikiwa kufika hapo kwenye mradi mkubwa kabisa uliofahamika kama DEGE ECO VILLAGE,kiukweli nilikuwa nashangaa sana namna ambavyo watu wanatumia fedha,ule mradi ndugu zangu ulikuwa mkubwa mno,na kwa waliobahatika kufika huko au wanaotokea huko watakubaliana nami.
Hatukutaka kupoteza muda kabisa ilibidi Mwakisaka aniambie tuulizie namna ya kupata kibarua kwasababu tulikuta watu wakiwa wanachakalika kinoma.Kuna jamaa tulimfuata tukaanza kumuulizia namna ya kupata kibarua siku hiyo.
Jamaa "Hapa kwetu yupo foreman ambaye ndiye msimamizi wetu,ukienda kule mbele pia wanae foreman wao"
Mwakisaka "Foreman wenu yuko wapi tujaribu kuongea nae?"
Jamaa "Nadhani atakuwa anazungukia maeneo anayosimamia,subirini tu hapa atakuja"
Tulisogea kando tukawa tunaendelea kuushangaa ule mradi wakati huo tunamsubiri mtu tuliyeambiwa ndiye foreman wa hapo tulipofikia.Baada ya muda wa nusu saa jamaa mmoja mweusi aliyekuwa mnene na kitambi cha kutosha akawa amekuja na ndipo yule jamaa alitukonyeza ya kwamba jamaa ndiye foreman wa lile eneo.Tulimfuata na kumjulia hali jamaa kisha Mwakisaka akaanzisha maongezi nae.
Mwakisaka "Kaka tunatafuta kazi ya kibarua "
Foreman "Aliyewaambia hapa tunaajili vibarua nani?"
Mwakisaka "Hakuna mtu aliyetuambia kaka tumekuja kuona kama tutapata"
Foreman "Hapa hatuajiri kwa sasa,siku tukiajiri vibarua mtapata taarifa"
Baada ya yale majibu ya kukatisha tamaa Mwakisaka aliamua akae kimya kisha jamaa akaanza kuondoka kuzunguka nyuma ya yale majengo yaliyokuwa mbele yetu.Sasa yule jamaa aliyekuwa kibarua pale akawa amemuita Mwakisaka akamwambia bila pesa ni ngumu sana kupata kibarua kwasababu hata wao walihonga ndipo kupata kibarua,jamaa akasema twende tukaongee nae kikubwa.Nilimwambia Mwakisaka hiyo kazi ya kuongea na jamaa aniachie mimi,akikataa basi tungerudi zetu kwa Mushi kule kivule kuendelea na ufyatuaji wa tofali.
Niliamua kuzunguka ule upande alokuwa amekwenda yule foreman na bahati nzuri nilimuona akiwa anaingia kwenye jengo moja,nilitembea kwa haraka ili kumuwahi kabla hajafika kwa watu wengi ikawa shida kuzungumza nae.
Mimi "Kaka kakaa"
Foreman "mmmh nambie"
Mimi "Kaka tusaidie ndugu yangu na kama ni chochote tutakupatia"
Foreman "Wewe si ndo upo na yule mwenzio nimewaambia hamna kazi!"
Mimi "Kaka tusaidie ndugu yangu!"
Foreman "Nyie mnatokea wapi?"
Mimi "Wote tunatokea kivule"
Foreman "Kivule?,sasa kivule hadi kuja kufanya kazi huku hamuoni tutasumbuana?"
Aliendelea "Ni bora hata mngekuwa hapa maeneo ya jirani"
Mimi "Tutaweka kambi maeneo haya kaka wala hilo lisikupe taabu"
Foreman "Hapa jirani haturuhusu watu kukaa kwasababu za kiusalama"
Mimi "Sijamaanisha hapa kwenye mradi kaka,tuta tafuta eneo maeneo ya jirani tutaweka kambi"
Foreman "Tukubaliane,mtanipa elfu tano tano kila siku kwa muda wa wiki moja"
Aliendelea "Na iwe siri,ikiwa vinginevyo mi nitawaruka na kuwageuka"
Mimi "Hakuna tazizo kaka"
Foreman "Kamuite mwenzio mje niwakabidhi huku juu!"
Niliondoka kumfuata Mwakisaka na kumueleza kila kitu jamaa alichosema na jamaa akaniambia hakuna tatizo;Tuliondoka kumfuata yule foreman ambaye alituchukua mpaka kwa jamaa wengine akamuacha hapo Mwakisaka kisha akaniambia tena nifuatane nae,mimi pia akawa amenipeleka kwenye kikosi kingine.
Tukaanza kuifanya kazi ya kibarua rasmi na kwa siku tukawa tunapewa elfu 15,ishu ya kula pamoja na maji ya kunywa ilikuwa ni juu ya yako wewe kibarua uzuri ni kwamba,kwenye kundi ambalo mimi nilikuwepo walikuwa wamejitolea kuchanga fedha na kununua vyakula kisha kuna mtu walikuwa wanamlipa anakuja kuwapikia,hivyo na mimi baada ya kuingia kwenye kundi la wale jamaa niliamua kuchangia elfu 10 kwa kila wiki kwa ajili ya huo mpango.
Miongoni mwa wale jamaa pia walikuwa wametengeneza matenti ya maturubai kuishi hapo maeneo ya jirani,niliamua kichangia fedha na mimi ili kukaa hapo,sasa bahati nzuri ni kwamba wikiendi tulikuwaga tunapumzika na hiyo niliitumia kwenda kufata virago vyangu kwa kaka Kileri na kurudi kambini,sikutaka kabisa kuhangaika na mambo ya jiji la Dar es salaam,fokasi yangu ilikuwa ni kwenye kufanya kazi na kutunza malipo yangu kwenye simu.
Nilipopambana ndani ya miezi mitano kwenye ule mradi nilipata kiasi kisichopungua Tsh milioni 1.3,sasa nilimuomba Mwakisaka aniambie ni eneo gani ni zuri kwa kupanga chumba na angalau linakuwa na maisha nafuu kwa hapa Dar es salaam.
Mwakisaka "Mwanangu mimi nakaa Gongo la mboto na nikuzuri sana"
Mimi "Kwahiyo kipindi kile ulikuwa unatoka Gongo la Mboto mpaka Kwa Mushi?"
Mwakisaka " Nilikuwa nakaa kulekule kivule kwa ndugu yangu mmoja"
Aliendelea "Kama unataka chumba we sema nimpigie simu jamaa mmoja pale kitaa akutafutie chumba"
Mimi "Nahitaji kaka"
Mwakisaka "Basi ngoja nitamcheki mshikaji"
Kweli,baada ya Mwakisaka kuwasiliana na jamaa yake na kumjulisha nilikuwa nahitaji chumba jamaa alianza kutafuta na akasema endapo angepata basi angetujulisha.
Baada ya siku tatu yule jamaa aliyepewa kazi na Mwakisaka ya kutafuta chumba akawa amesema nyumba imepatikana maeneo ya mwisho wa lami lakini ni vyumba viwili ambavyo malipo ilikuwa ni elfu 45 kwa kila chumba na ilipaswa kulipwa kwa miezi 6.
Mwakisaka "Jamaa anasema nyumba imepatikana Gongo la mboto mwisho wa lami"
Mimi "Mwisho wa lami ni maeneo ya wapi?"
Mwakisaka "Hapo hapo Gongo la mboto sema ni mbele kidogo"
Mimi "Sawa,na wewe ndiyo unaishi huko?"
Mwakisaka "Hapana,mimi naishi Mzambarauni"
Mwakisaka "Ila jamaa anasema amepata chumba na sebule kwa elfu 45 kwa kila kimoja na inalipwa miezi 6,vp?"
Mimi "Sawa,hakuna tazizo"
Mwakisaka "Ngoja nimwambie amwambie mwenye nyumba atulie kesho kutwa tukakicheki"
Mwakisaka aliwasiliana na yule jamaa akawa amemwambia amwambie mwenye nyumba jumapili tungeenda kukitazama ikiwezekana nilipie kabisa.
Namshukuru Mungu baada ya kwenda kuingalia ile nyumba niliipenda na nikawa nimelipia miezi sita,hela iliyobaki nikanunua godoro na mashuka nikawa nimeyaweka na mimi kufunga chumba kisha kurudi Kigamboni kuendelea na kibarua.
Kila nilipokuwa ninapata hela nilikuwa nikinunua kitu kimoja baada ya kingine na kuweka ndani na hatimaye vyumba vikawa na muonekano mzuri,kiukweli pamoja na mateso ya kushinda juani niliyokuwa nayapitia kule kigamboni lakini nilihakikisha najinyima kiasi kwamba hadi malengo yangu yatimie.
Ule mradi wa Dege kuna muda ukawa umesimama kidogo hivyo kwa muda ule nikaenda kukaa kwangu nilikokuwa nimepanga,sasa pale nilipokuwa naishi kulikuwa na geti na tulikuwa wapangaji kadhaa na kila mtu alikuwa na ishu zake.
Sasa kuna jamaa mmoja alikuwa akiitwa Steve yeye tulitokea kushibana sana na tukawa marafiki,jamaa alikuwa akifanya kazi kampuni ya Tigo kama msajili line za simu,kwakuwa ule mradi ulikuwa umesimama kwa muda usiojulikana,jamaa aliniambia kama vipi aniunganishe na timu leader wake anipatie kodi ya kusajili line za simu nami nianze kuwa msajili laini.Jamaa aliniambia ni kazi ambayo ilikuwa na pesa sana ila watu walikuwa wakiichukulia poa.
Steve "Ngoja kesho nitamueleza team leader kama vipi akupe kodi ili uanze kufanya kazi"
Mimi "Kazi inafanyikaje kaka"
Steve "Kazi ni nyepesi sana kaka utaelekezwa namna ya kuifanya"
Kwakuwa kwa muda huo sikuwa na kazi baada ya kusimama kwa mradi,niliona jamaa atakuwa amenisaidia sana ili kuweza kujinasua na ukata ambao ulikuwa ukininyemelea baada kuwa nakula hela nilizokuwa nimezitunza bila kuzizalisha.
Itaendelea.........
NzuriUtajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 04.
Sasa muda ambao mke wa anko anafika pale nyumbani mimi nilikuwa nyuma ya nyumba ambapo kulikuwa kuna kama kibustani kidogo ndani yake kulikuwa kumepandwa miwa ambayo ilikuwa imekuwa mikubwa na hakukuwa na walaji,niliona nikate zangu muwa nikaa chini nikaanza kutafuna,kumbe aliingia chumbani anakolala yule mzee ambaye ni baba yake na akakuta amejisaidia kitandani na hakukuwa na mtu aliyemwangalia na kumjali,kwa mawazo yake yeye alidhani mimi nimemuona yule mzee na nikamuacha kama alivyo ili aendelee kuteseka!.
Akili na mawazo yake yalimtuma vibaya kwasababu sikuwa nimeingia mle chumbani tangia mchana,pia yule mzee alikuwaga kama na kakiburi fulani hivi ambako kalikuwa ka kijinga,anaweza kuwa amebanwa na haja kubwa wala asiite mtu yeyote,utakuta ameinyanyuka ameingia chooni na amechafua vibaya bila hata kuflashi.Inawezekana alifanya makusudi siku ile ili kunikomoa.
Kumbe muda huo Anko anapewa makavu laivu ilikuwa ni hiyo ishu na bahati mbaya sana Anko wangu alikuwaga akoromi kwa yule mwanamke bali hasira za kugombezwa na mkewe zilikuwaga zinaishia kwa wanae au mimi kwa wakati ule nipo kwake.
Muda huo ambao nipo zangu natafuna miwa sina habari,kumbe alimwambia yule mfanyakazi akaingia mle ndani akatoa yale mashuka akawa amemnyanyua mzee akampeleka bafuni mzee akajisafisha kisha akatandika shuka safi na kuweka mazingira ya chumba poa.
Mimi sikufahamu chochote kwasababu nilipomaliza kula miwa nikazunguka kule mbele ya nyumba ndipo nikakuta gari ya mke wa anko ikiwa imepaki nikajua atakuwa amerudi,sikutaka kuingia ndani kwasababu ilikuwa bado mapema,niliingia stoo nikachukua fagio la nje nikaanza kufagia pale nje.
Nilipomaliza niliingia ndani kuoga na kubadili nguo ili nije nikae sebuleni nitazame luninga,wakati naingia mle ndani nilikuta mzee amelala na kitandani kukiwa na shuka nyingine,sikufahamu kumbe dakika chache zilizopita hali ya mle ndani haikuwa nzuri,sasa huo usiku anko alivyorudi ndipo mkewe akamuamshia mtiti!.
Baada ya hayo malumbano Anko alivyorudi sebuleni alikuwa amebadirika na sikutaka kusema chochote mimi niliendelea kutazama luninga,chakula kilipotengwa alielekea kula na alipomaliza aliingia chumbani kwake!.Mkewe yeye sikuonana nae kwa siku hiyo.
Asubuhi kama kawaida wao waliondoka wakawa wamelekee kazini,pale nyumbani nikawa nimebaki mimi,yule binti wa kazi pamoja na mtoto mkubwa wa anko ambaye naye aliondoka ilipofika mida ya saa 3 asubuhi.Sasa baada ya yule mtoto wa Anko kuondoka,yule binti wa kazi alikuja kuniita nikanywe chai,muda huo nilikuwa nje napambana kungolea nyasi kwenye maua yaliyokuwa kando ya fensi.
Binti wa kazi " Hivi jana ulikuwa wapi?"
Mimi "Jana?,Jana saa ngapi?"
Binti wa kazi " Aliporudi Mama"
Mimi "Nilikuwa kule Bustanini"
Binti wa Kazi "Jana mama kagomba"
Mimi "Alikuwa anagomba kuhusu nini?"
Binti wa kazi "Aliporudi aliingia chumbani kwa babu akakuta babu kajinyea,alikuwa anakuulizia mi nikajua labda umetoka!"
Mimi "Alijenyea saa ngapi?,mbona mchana nilipotoka ndani alikuwa tu vizuri"
Binti wa kazi "Alikusema maneno mabaya sana,we acha tu"
Mimi "Mimi siyo mjinga nimuone huyo mzee akiwa anashida niache kumsaidia,mbona siku zote namuosha na kumpeleka chooni na mpira nambadilishia!"
Mimi "Jana nilikuwa bustanini na sikutoka nje kabisa"
Mimi "Kwani kabla sijaja hapa nani alikuwa akimuangalia mzee?"
Binti wa kazi "Nani zaidi yangu?wanae tu wala hawana time na babu yao"
Baada ya mazungumzo ya muda kadhaa nilinoti kitu kwa yule dada wa kazi ambacho hakutaka kabisa kuniambia,kwa kifupi yule mke wa anko inaonekana alitoa shiti nyingi dhidi yangu,niliamua kutulia na kutafakari.
Sikwenda kwa Anko uenda kwakusema nimepigwa na maisha ili anifadhili la hasha,nilienda pale kwasababu wakati nafika mjini mwenyeji wangu alikuwa hapatikani,sasa kuna muda nilikuwa nashangaa wanavyonichukulia ni kana kwamba nimepigwa na maisha!.
Baada ya kupata kifungua kinywa niliamua nimsubiri Anko akitoka kazini ile jioni nimuage na kesho yake nisepe niwaache wapambane na matatizo yao na roho zao mbaya.Kweli,usiku ule kabla ya kula tukiwa pale sebuleni tukiangalia taarifa ya habari,nilimwambia kesho mimi nitaondoka.
Anko Nico " Utaondoka kwenda wapi?"
Mimi "Nitaenda kwa yule mtoto wa baba mkubwa"
Anko Nico " sawa siye tupo"
Baada ya hayo mazungumzo niliona kabisa nilikuwa sitakiwi.Ukiachilia Anko,lakini mkewe na watoto wa Anko walikuwa ni watu ambao hawana time na mtu,tangia nimefika hapo hawakuwahi hata kusema na mimi wala kujua hali ya maisha ya shangazi yao,walikuwa ni watu ambao hawakuwa na muda kabisa,pengine uzungu uliwaharibu au walilithi tabia za kwao mama yao.
Kesho yake nilimuaga yule mzee pamoja na yule binti wa kazi nikaondoka zangu,nilipotoka nje nilitembea hadi kituo cha daladala nikapanda kuelekea tegeta.
Kwakuwa nilikuwa nimeshawasiliana na Kileri akawa ameniambia anakaa Kivule na hivyo ilipaswa nipande magari yatakayonifikisha ubungo stendi ya daladala na nikifika hapo nipande za gongo la mboto nikashukie banana kisha nichukue za kivule.
Namshukuru Mungu nikawa nimefika na jamaa akaja kunichukua tukaelekea kwake.Nilipofika kwa jamaa nilikuta anakaa kwenye nyumba ambayo bado haijaisha na nilikuta mafundi wakiwa wanaweka vigae kwenye vyumba baadhi.
Kileri "Karibu wa kwetu,hapa mimi ndipo naishi na familia yangu"
Mimi "Hongera kaka umejitahidi"
Kileri "Kawaida tu,naipeleka mdogo mdogo mpaka itaisha,mjini hapa ukiwa na kwako unaepuka usumbufu wa kodi"
Baada ya mazungumzo ya hapa na pale,jamaa akawa ameniambia kesho yake tungeenda Tandika ambako alidai ndiko anakofanyia biashara ili nikajionee namna biashara ilivyo shamiri.
Ilipofika asubuhi tuliondoka kuelekea huko Tandika kama alivyokuwa ameniambia.Tulipofika hapo Tandika kuna duka moja la vyombo tuliingia lakini kuna kitu kikanishangaza.
Itaendelea......
Kuna watu wana kipaji cha kusave kutimiza malengo.
Lakini we UMUGHAKA unawezaje kuishi bia demu? Zaidi ya yule Monica mchawi kule
Madem hawakuwahi kuwa sehemu ya maisha yangu katika utafutaji japo nimekuwa nao kadhaa ila huwa sitaki sana kusimulia mambo ya mademu,nikimaliza hii stori nadhani sasa nitaanza kusimulia ya demu wangu Shamima wa Tanga alivyo fanya nikafeli shule,humo kuna kila kitu na kama wewe ni mpenzi wa migegeduo basi utafurahi na roho yako,endelea kusubiri!Kuna watu wana kipaji cha kusave kutimiza malengo.
Lakini we UMUGHAKA unawezaje kuishi bia demu? Zaidi ya yule Monica mchawi kule kijijini hujawahi simulia kuhusu mwanamke mwingine
Nshakupigia kuraMadem hawakuwahi kuwa sehemu ya maisha yangu katika utafutaji japo nimekuwa nao kadhaa ila huwa sitaki sana kusimulia mambo ya mademu,nikimaliza hii stori nadhani sasa nitaanza kusimulia ya demu wangu Shamima wa Tanga alivyo fanya nikafeli shule,humo kuna kila kitu na kama wewe ni mpenzi wa migegeduo basi utafurahi na roho yako,endelea kusubiri!
Bro story haiendelei usiku huu?Madem hawakuwahi kuwa sehemu ya maisha yangu katika utafutaji japo nimekuwa nao kadhaa ila huwa sitaki sana kusimulia mambo ya mademu,nikimaliza hii stori nadhani sasa nitaanza kusimulia ya demu wangu Shamima wa Tanga alivyo fanya nikafeli shule,humo kuna kila kitu na kama wewe ni mpenzi wa migegeduo basi utafurahi na roho yako,endelea kusubiri!
Zaman mkuu. Kura imepigwaPiga kura kijana stori ipo
Hapo kulipia chumba hela yote mie nisingeweza kulipa ,chumba kimoja godoro neti ya hema ndoo ya maji maisha yanasonga. Hela nyingi nawekeza nifanye biasharaMadem hawakuwahi kuwa sehemu ya maisha yangu katika utafutaji japo nimekuwa nao kadhaa ila huwa sitaki sana kusimulia mambo ya mademu,nikimaliza hii stori nadhani sasa nitaanza kusimulia ya demu wangu Shamima wa Tanga alivyo fanya nikafeli shule,humo kuna kila kitu na kama wewe ni mpenzi wa migegeduo basi utafurahi na roho yako,endelea kusubiri!
Leta hiyo ya kukunjana 😂..hii ya Sasa weka kapuniMadem hawakuwahi kuwa sehemu ya maisha yangu katika utafutaji japo nimekuwa nao kadhaa ila huwa sitaki sana kusimulia mambo ya mademu,nikimaliza hii stori nadhani sasa nitaanza kusimulia ya demu wangu Shamima wa Tanga alivyo fanya nikafeli shule,humo kuna kila kitu na kama wewe ni mpenzi wa migegeduo basi utafurahi na roho yako,endelea kusubiri!
Umesahau jana kuna mtu anaitwa dr namugari alisema umughaka ni mtu wa hovyo kuliko wote labda apigiwe kura ya mtu mzembe kabisa maana katika story zake zote yeye ndio anakuwa mhanga mara zote. Mtanzania Mnyonge22OUT OF TOPIC:
Tumpigieni KURA UMUGHAKA aweze Kushinda kwenye Mashindano ya Jamii Forum Entertainment. Hii ndo njia ya kumlipa kwa jinsi anavotuburudisha. Mpaka sshv tumepiga kura watu 14 tu, please Lets Support him.
Piga Kura kumchagua mwanachama bora wa JF Entertainment 2022
Katika kutambua umahiri wa baadhi ya wanachama, Jamii Forums inaendelea na mchakato wa kumpata mwanachama bora wa mwaka 2022. Tafadhali piga kura yako ili kumpata mwanachama bora wa mwaka 2022 kwenye Jukwaa la Entertainment. Kura zitapigwa kwa muda wa siku tano. Mchakato wa kupata majina...www.jamiiforums.com
😂😂😂😂Jinsi ulivyo tapeliwa hiyo 9M umenikumbusha nilivyompa mtu 500k aipeleke mahali nikampa na elf 15 ya nauli japo nauli ilikua hata elfu 3 inatosha kufika njian akaichezea kamari akaliwa yote alafu akanipigia simu kwa simu ya kuazima akanimbia "Bro naomba kama una elfu mbili nitumie nikifika huko tutaongea"
Nikamuulize hela imefika? Akanijibu usiwe na haraka bro we nitumie elfu mbili nije nikuelezee vizuri kwa simu hutanielewa.
Nilimpa jibu moja tu "usirudi nitakuua"
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Jinsi ulivyo tapeliwa hiyo 9M umenikumbusha nilivyompa mtu 500k aipeleke mahali nikampa na elf 15 ya nauli japo nauli ilikua hata elfu 3 inatosha kufika njian akaichezea kamari akaliwa yote alafu akanipigia simu kwa simu ya kuazima akanimbia "Bro naomba kama una elfu mbili nitumie nikifika huko tutaongea"
Nikamuulize hela imefika? Akanijibu usiwe na haraka bro we nitumie elfu mbili nije nikuelezee vizuri kwa simu hutanielewa.
Nilimpa jibu moja tu "usirudi nitakuua"