Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

My feet we nenda kale matunda yako kimasiara huko acha kuwatisha watu humu ,huna mamla wala uwezo was kufanya hvyo [emoji41]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Bila shaka wewe ndie Kilieri mwenyewe maana unaandika Kilevi Levi sana,unashobokea story za watu kindezi afu unajiita Dr? Mkuu ficha ujinga wako na ujuaji wako mwenzako Popoma hana Amani wiki ya pili hii
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 06.




Fedha niliyokuwa nimeitafuta kwa jasho na damu na baada ya kuuza mali za duka letu la vipodozi tukawa tumegawana na rafiki yangu kipenzi ikawa imeishia mikononi mwa ndugu yangu ambaye niliamini tungefanya biashara ikashamiri kama alivyokuwa akiniambia lakini haikuwa kama nilivyodhani!.Nilipanga niendelee kuwa subira uenda mwisho wa mwezi angeenda kwa wale jamaa pale Tandika akapewa faida ya pesa aliyokuwa ameweka hapo dukani kama alivyoniambia,niliamua kuupa muda nafasi ingawa Jamaa baada ya kupewa taarifa na mkewe kuhusu hizo hela alikata mawasiliano kabisa kwa takribani wiki mbili.

Sikutaka kabisa kukaa kizembe pale kwa Kileri,niliamua kuzunguka kutafuta kazi ya kufanya angalau nianze kutengeneza pesa,sasa niliamua kutembea mdogo mdogo kama naelekea Banana na kuna mahali nilifika nikakuta jamaa wanafyatua tofali za blocks,eneo lile halikuwa mbali na nyumbani kwa kileri,ilikuwa takribani mita kama 1000 hivi,nilijisogeza mpaka pale nikawa nimeongea na jamaa mmoja ambaye ndiye alionekana kuwa kiongozi wa ule mradi.

Mimi "Kaka kwema"

Jamaa "Kwema,vipi hali"

Mimi "Safi kaka"

Mimi "Naweza kupata angalau kibarua kaka?"

Jamaa "Kibarua kama kipi unaweza!"

Mimi "Chochote tu kaka"

Jamaa "Unao uzoefu wa kufyatua tofali?"

Mimi "Hapana kaka ila kubeba na kupanga naweza"

Jamaa "Unaitwa nani?

Mimi "Naitwa Umughaka"

Jamaa "Ok sawa"

Aliendelea "Sudiiiiiii !"

Jamaa "Sudi eeeh !"


Sudi "Nambie "

Jamaa "Njoo mwanangu"


Sudi "Nambie "

Jamaa "Jamaa anahitaji kibarua,vp kuna sehemu umchomeke?"

Sudi "Hapa nafasi haziishagi ni nguvu zake tu"

Jamaa "Sawa muangalizieni"

Sudi "Mbona kama umependeza,unataka leo leo au ulikuja kucheki kwanza"

Mimi "Kaka nipo tayari kwa kazi"

Sudi " Hizo nguo huzipendi au!"

Mimi "Nitavua nitabaki na bukta"

Sudi "Sawa,twenzetu"


Baada ya maongezi ya muda mfupi,jamaa aliyeitwa Sudi alinichukia mpaka eneo la kazi kisha nikavua nguo zangu nikawa nimebaki na bukta(boksa),sasa Sudi akawa ameniambia nitakuwa nachukua tofali zitakazokuwa zinafyatuliwa na mashine na kisha kwenda kuzipanga kwenye eneo la wazi lililokuwa limetengwa kwa kazi hiyo.

Niliifanya ile kazi kuanzia muda ule hadj jioni mida ya saa 12,kiukweli haikuwa kazi ya kitoto hata kidogo,kwakuwa niloshafanya kazi nzito na ngumu kuliko ile,sikuona tatizo lolote japo jamaa waliponiangalia walidhani mimi ni lele mama lakini nilipoanza kupiga mzigo hawakuamini!.Eneo lile kulikuwa na kinyumba kidogo na kwa nyuma kulikuwa kumejengwa choo pamoja na bafu,hivyo baada ya kumaliza kazi nikawa nimeingia kuoga,nilipomaliza kuoga,yule jamaa ambaye nilienda kumuomba kazi aliinita akanipatia elfu 3 ambayo ni kama posho ya kibarua.Ilikuwa ni hela ndogo sana lakini sikukata tamaa kwakuwa kwa wakati huo sikuwa na kazi yoyote!.

Baada ya malipo niliondoka zangu kwa kutembea kurudi kwa Kikeri ambapo ndipo nilipokuwa nimefikia.

Niliendelea kuifanya ile kazi kwa siku kadhaa,sasa ilikuwa kwamba mteja amiweka oda ya tofali tunapakia na kwenda kushusha tulikuwa tunapewa posho ya upakiaji na ushushaji elfu 2 kila mmoja,hivyo ukijumlisha na ile posho ya ufyatuaji na ubebaji kwenda kuanika ambayo ilikuwa buku 3,kwa siku nilikuwa napata zaidi ya elfu 10,kwasababu kwenye upakiaji na ushushaji kwa siku tulikuwa tunapata oda hata za wateja 3 hadi 4 kwa siku.

Kuna siku nilipomaliza kazi nimerudi nyumbani pale kwa ndugu yangu Kileri nikamkuta yupo,sasa sikutaka kuzungumza nae pale ndanj ilibidi nimwambie shemu tunatoka kidogo.Dhumuni la mimi kumtoa pale nyumbani nilitaka anieleze ukweli kuhusu ile hela kwasababu ilikuwa ni mwezi umekatika na hakukuwa na mrejesho wowote kuhusu faida kama alivyokuwa ameniambia.


Mimi "Ndugu yangu hujanipa mrejesho wowote kuhusu biashara"

Kileri "Kaka wewe acha tu"

Aliendelea "Kiukweli kaka niwe mkweli,wewe ni ndugu yangu sitaki kukuficha"

Kileri "Ile hela ulinipa nilienda kulipa deni nililokuwa nadaiwa na yule jamaa(Jamal) na kuna kiasi cha fedha niliona nijengee choo kilichokuwa cha mabati"

Aliendelea "Juzi kabla hujaja mama yake mke wangu alisema anakuja sasa nikaona nitengeneze angalau vyumba viwili niweke vigae ili kuwe na muonekano kaka"

Mimi "Kaka ni heri ungeniambia tangu mapema nikiwa Tarime kwamba unashida na hela ningekutumia kwakuwa wewe ni ndugu yangu"

Mimi "Lakini kitendo cha kufanya mimi kuja huku nikiamini tunakuja kufanya biashara wakati ni uongo,umenikosea sana ndugu yangu"

Kileri "Nitampigia Marwa nyumbani nimwambie aniuzie vile vi ndama vyangu halafu nitakulipa,wewe ni ndugu yangu"

Mimi "Wewe acha tu,kama ipo ipo tu kaka!"

Mimi "Wala usijali kuhusu hiyo hela"


Kiukweli nilijisikia hasira sana na nilijiona ni mpumbavu sana kumpatia Kileri ile hela ambayo haikufanya jambo la maana zaidi iliishia kwa wanawake zake na utumbuaji wa starehe,sikukata tamaa niliamini kama niliweza kuipata hiyo hela basi nitaweza kuipata nyingine.Japo alijitahidi kunieleza maneno mengi lakini bado nilimuona ni muongo kwasababu mkewe alikuwa ameniambia kila kitu.


Niliendelea kupambana katika ile kazi ya tofali pasipo kukata tamaa,nilikuwa natafuta hela angalau nikapange chumba changu ili niweze kujisogeza zaidi.Kuna siku nikiwa na jamaa zangu kwenye gari tukiwa tunapeleka tofali kwa mteja,kuna jamaa mmoja nae alikuwa mfanyakazi mwenzangu hapo site alikuwa akituambia kama vipi twende kwenye mradi wa nyumba huko kigamboni uliokuwa ukifahamika kama DEGE.


Mwakisaka " Mwanangu kama mko tayari kesho tuibuke Dege kuna jamaa zangu wako kule wanasema kuna hela nzuri"

Mimi "Dege ndo wapi?"

Mwakisaka "Kigamboni huko kuna nyumba zinajengwa kama utitiri!"

Aliendelea "Halafu kule vibarua kwa siku waliniambia wanakula elfu 15"

Zomela "Tatizo kigamboni ni mbali,hiyo hela inaishia tu kwenye nauli"

Mwakisaka "Sasa hiyo nauli kwani unaenda wapi?,watu huko wamepiga kambi halafu wewe unaongelea masuala ya nauli tena"

Aliendelea "Mimi kesho ngoja niende nikacheki"

Zomela "Tatizo huko unaweza kwenda ukakosa na ukirudi huku nako unakuta wameweka mtu mwingine,tena nianze kufanya kazi kutafuta kazi"

Mwakisaka "Kwani utasema unaenda wapi?,kule tunaenda kimya hivyo si rahisi mtu kujua,tukipata ndo hivyo tusipota tunarudi"

Zomela "Hao jamaa zako wanauhakika?,siyo tunachoma nauli tu!"

Mwakisaka "Aliye tayari kesho twende tukikosa tunarudi"

Baada ya yale mazungumzo nilimwambia Mwakisaka mimi nitakuwa tayari kuungana nae na kuelekea huko Kigamboni kusaka kibarua cha elfu 15.

Mimi "Kwahiyo tutakutana wapi?"

Mwakisaka "Kwani siunasimu?"

Mimi "Ndiyo"

Mwakisaka "Nigei namba yako asubuhi nitakushitua"

Nilimpatia namba yangu ya simu Mwakisaka kisha tukaendelea na mambo mengine.

Ilipofika alfajiri mida ya saa 11,Mwakisaka alinipigia simu na akawa ameniambia tuonane pale Banana na nikifika nimwambie,kweli nilianza kuhangaika na usafiri wa kunitoa huko kivule ambao ulikuwa wa changamoto sana,nilihangaika kupambania usafiri hadi saa 12 asubuhi ikanikuta bado sijapata gari,nilikuja kupata gari imejaa ikabidi nining'inie hivyo hivyo kibishi ilimradi nifike.Nilipofika pale Banana nilimpigia Mwakisaka ambaye yeye alikuwa amefika kitambo akinisubiri mimi!.


Mwakisaka "Shwari?"

Mimi "Shwari kaka"

Mimi "Zomela yuko wapi?"

Mwakisaka "Yule hawezi kwenda,ameshapazoea pale kwa Mushi kama kwao"

Aliendelea "Hapa itabidi tupande magari ya kivukoni"

Tulikaa pale stendi tukawa tunasubiri magari ya kivukoni yaliyokuwa yanatokea Gongo la mboto ili tupande tuondoke,gari nyingi zikawa zinapita zimeshona watu kama utitiri,kiukweli nilikuwa nashangaa sana ile hali kwakuwa hata Mwanza sikuwahi kuona gari zinajaa kiasi kile!.

Baada ya muda kupita kuna gari ambalo lilikuja likiwa angalau na nafasi ya kusimama na tukapanda hilo.



Itaendelea.......
Kama ulifanya kazi pale dege karibu na cheka uko vzr
Muda siiyo mrefu nitashare picha ya majengo hayo kwa wasiofahamu ,kipindi Cha jiwe Kama yalitelekezwa HV



Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Bila shaka wewe ndie Kilieri mwenyewe maana unaandika Kilevi Levi sana,unashobokea story za watu kindezi afu unajiita Dr? Mkuu ficha ujinga wako na ujuaji wako mwenzako Popoma hana Amani wiki ya pili hii
Naona Popoma mmemtendea ubaya tayari ,,😂😂 nyie watu sio waungwana kabisa😂
 
Nisikuchoshe na usinichoshe, tusichoshane!.

Kwanza kabisa nipende kuwashukuru wote ambao mmeendelea kuwa na mimi bega kwa bega tangia mwanzo wakati naanza kusimulia visa vya maisha yangu ambayo nimeyaishi na kuyapitia kama mwanadamu.

Simulizi yangu ya kwanza kabisa hapa JF imefahamika kama "TULICHOMFANYA YULE MCHAWI HATOKUJA KUSAHAU KAMWE" hii inapatikana kwenye jukwaa hili la Entertainment,simulizi hii iliangazia namna tulivyopata shuruba ya ushirikina wakati ambao nilienda kumsalimia baba yangu mdogo aliyekuwa mwalimu katika shule moja ya sekondari huko mkoani Tabora,kiukweli ni mkasa ambao sitokuja kuusahau kamwe kwasababu ndipo niliamini wachawi wapo na uchawi upo!

Simulizi ya pili ilikuwa ni muendelezo baada ya hiyo ya kwanza,simulizi hii ya pili niliona nianze kusimulia baada ya mimi kwenda shule ya upili(Advance)na wakati nilipo maliza matokeo yangu hayakuwa mazuri hivyo nikatimuliwa na Mzee(Baba)yangu nyumbani nikaingia mtaani kupambana,simulizi hii inafahamika kama "NILIVYONUSURIKA KIFO BAADA YA MZEE KUNITIMUA NYUMBANI" na inapatikana kwenye jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko.

Sasa leo nimeona niwaletee na niendelee na masimulizi ya maisha yangu ili kuwapa hamasa vijana wenzangu kuweza kupambana na kutokata tamaa mapema!,dhumuni la masimulizi yangu ni kutoa funzo kwa watu,na sipo hapa ili kujipatia fedha kwa njia ya ulagahai,mimi binafsi ninajiweza kwasababu ni mpambanaji na sihitaji hata mia mbovu ya walalahoi wenzangu!.

Mimi binafsi nimfanyabiashara, nimejiajiri kwa kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria almaarufu kama Bodaboda, shughuli zangu huwa nazifanyia hapa Bunju, ingawa ki makazi naishi mbezi Inn ila kikazi nafanyia Bunju. Sasa kama mtakumbuka kwenye simulizi ya mwisho nilisema ya kwamba,baada ya kuwa tumeuza lile duka la vipodozi ambalo tulikuwa tumefungua na rafiki yangu kipenzi Mtatiro (Kwa sasa anaishi nchini Uganda), tuliamua kugawana fedha kila mtu afe na chake, mimi niliamua kurudi zangu Tarime-Sirari, baada ya kukaa kule kuna ndugu yangu(Mtoto wa Baba yangu mkubwa) tuliwasiliana naye akaniambia nije Dar es salaam ili tufanye biashara ya uuzaji wa vyombo vya ndani kwasababu kwa wakati huo ilikuwa na pesa(Kwa maelezo yake).

Niliianza safari ya kuja Dar es salaam, sasa nilipofika Dar es salaam pale Ubungo(Kipindi stendi bado haijaamia mbezi), ile nimefika mida ya saa 5 usiku nikampigia simu mwenyeji wangu lakini majibu toka kwenye simu ni kwamba "Namba unayopiga kwasasa haipatikani,jaribu tena baadae", niliendelea kuipiga ile simu lakini majibu yalikuwa ni hayi hayo!.

Kwakuwa nilikuwa nimechoka,niliamua kumsikiliza moja ya watu ambao walikuwa wakinisumbua ili wabebe mzigo wa begi langu ili niwalipe posho, mpaka wakati huo nilikuwa makini sana kujilinda mimi binafsi pamoja na mzigo wangu, kilichofanya nikawa makini kupita kiasi ni stori ambazo mara zote nimekuwa nikizisikia kuhusu Jiji la Dar es salaam na vioja vyake.

Mimi " Mwanangu vipi!?"

Jamaa " Poa bro"

Mimi "Mbona mnavurugu,shida ni nini?"

Jamaa " Si huyu msenge,nimemwambia wewe ni wakwangu lakini hataki kusikia"

Mimi "Ok mnasemaje"

Jamaa "Bro we nipe begi mi nikubebee,achana na huyu muhuni atakuibia"

Mimi " Sasa wote mnang'ang'ania mzigo,nimpe nani na nimwache nani?"

Mimi "Sa sikia,begi langu nitalibeba mwenyewe,achaneni na mimi"

Baada ya kusikia rafudhi yangu na namna nilivyochukia nadhani waliamua kutii sheria bila shuruti,waliondoka wakiwa wananiangalia kwa uchungu na maumivu makali ya kukosa posho!.Kiukweli muda huo nilichokiongea ndicho nilichokuwa nikikimaanisha, kutokana na sifa mbaya za mkoa wa Dar es salaam nilikuwa nimesema yeyote ambaye angejitia kimbelembele kunikaba au kuniibia,basi siku hiyo ndiyo ingekuwa mwisho wa maisha yake!,Jeuri na kiburi cha kikurya vilinitia morali maradufu na niliwaona wale vijana wa pale stendi ni kama wanawake tu wasiokuwa na uwezo wa kunifanya chochote!.

Niliamua kujisogeza mpaka kwenye geti la kutoka nje,nilipotoka nje nilikuwa nikiendelea kushangaa pilika pilika namna zilivyokuwa za kutosha pale stendi,kiukweli sikuwahi kuona mji uliokuwa na pilika nyingi kama Dar es salaam,Mwanza nimekaa lakini hakukuwa na harakati za kutosha kama Dar es salaam.Nilichukua simu yangu nikawa nampigia tena mwenyeji wangu lakini simu yake ikawa haipatikani.Nilichukia sana kwasababu nakumbuka nilivyofika Singida alinipigia simu nikamwambia ya kwamba nimefika Singida na akawa amesema ikifika mida ya saa 2 usiku angekuwa amekuja pale stendi ili anisubiri nikifika tuondoke wote.

Kuna jamaa mmoja alikuwa kando ya geti la kutokea nje ya stendi pale Ubungo nilimsogelea nikawa namuuliza kuhusu Guest House yeyote iliyokuwa karibu ili niende nikalale na ikiwezekana asubuhi niendelee kumtafuta jamaa.

Jamaa "Sasa tutafanyaje ndugu!"

Aliendelea "Mwenyeji wako hajatokea?".

Mimi "Nimempigia simu lakini hapatikani!"

Jamaa "Duuuu mbona ni hatari!"

Aliendelea "Sasa sikia,wewe nyooka na hii barabara,unaona kwenye ile njia?"

Mimi "Ndiyo"

Jamaa "Hebu subiri"

Jamaa " Hassaniiiiiii"

Baada ya ya kuita hilo jina muhusika alifika


Jamaa "Hassani hebu nenda kampeleke huyu jamaa pale kwa Asteria,ukifika mwambie jamaa anataka chumba"

Aliendelea "Kaka nenda na jamaa atakupeleka kwenye Lodge ambayo kuna usalama na vyumba vipo vya kutosha,ila utamlipa maana kuna umbali"

Mimi "Hakuna tatizo"


Basi yule jamaa aliyeitwa Hassan akanichukua akanivusha barabara tukaikamata njia ya Ubungo Maziwa kuelekea kwenye hiyo lodge ambayo nimeambiwa kuna usalama na vyumba vya kutosha.Wakati tunakwenda na Bwana Hassan tulikuwa tunapiga stori za hapa na pale huku mikono yangu ikiwa bize imeng'ang'ania begi kwasababu ndilo lililokuwa na hela pamoja na nguo za kubadilisha,kiukweli nilikuwa nimesema endapo yeyote angejipendekeza kunikaba angejuta kuzaliwa.

Baada ya mwendo mrefu kidogo hatimaye tukawa tumefika kwenye Bar moja iliyokuwa inapiga mziki kwa sauti kubwa huku kukiwa na watu wengi.

Hassan " Nisubiri hapa nakuja"

Nilimsubiri Hassan pale nje baada ya kufika kwenye hiyo Bar na baada ya dakika 15 akawa amekuja kunichukua na kuongozana nae kuingia ndani.Tulipofika ndani ambako kulikuwa na kaunta,Hassan alinichukua tena kuelekea Uani ambako nilikuta kuna vyumba vingi ambavyo vilikuwa havipungui 10.

Sasa baada ya kufika pale Uani alikuja mwanamke mmoja mweusi mnene na ndiye aliyekuwa akiitwa Asteria,alimuita Hassan Pembeni wakawa wanaongea,sikufahamu kitu walichokuwa wanazungumza kwa wakati huo.Baada ya yale mazungumzo Hassan alirudi kwangu.


Hassan "Sasa bro,mimi nadhani nikuache wewe upumzike,niangalizie basi ustaarabu"

Mimi "Chumba changu cha kulala ni kipi?"

Hassan "Atakuonyesha Asteria,wala usijali kaka hapa ni nyumbani"

Baada ya maneno ya kutia moyo ya Hassan nikachomoa shilingi elfu 5 nikawa nimempatia kama posho ya kunipeleka hapo Guest.

Hassan "Aaah kaka hela gani hii?"

Mimi "Hela gani kivipi?"

Hasaan "Aaaah Kaka yaani nikutoe kule stendi na nimeacha shughuli zangu halafu unanipatia buku tano?,hebu ongeza ongeza kaka angalau kesho niamkie supu"


Sikutaka mambo mengi na yule Jamaa ikabidi nizame tena mfukoni nikatoa elfu 5 nyingine nikampatia,hivyo kufanya jumla kuwa elfu 10.

Baada ya jamaa kuondoka lile eneo nikamfuata yule demu aliyeitwa Asteria ili aje anionyeshe chumba niingie kulala kwasababu nilikuwa nimechoka.

Asteria "Kaka ina maana Hujaambiwa huu si muda wa kulala?"

Mimi "Si muda wa kulala?"

Mimi "Si muda wa kulala kivipi?"

Asteria "Kaka hapa huwa hatulazi watu ila tunakodisha!"

Aliendelea "Hivi vyumba vinakodishwa kwa dakika na masaa,labda usubiri mpaka saa 9 wateja wakipingua ndipo tutakukodishia ulale"

Kiukweli baada ya ile kauli niliishiwa nguvu ghafla,sasa baada ya kuniambia maneno yale yeye aliondoka akaenda kuendelea na shughuli zake akaniacha pale Uani nikiwa sijui cha kufanya,sasa ndipo nilikuja kugundua ya kwamba,vile vyumba vilikuwa vinatumika kwenye biashara ya short time(Biashara ya Ngono),sasa kumbe ile Bar niliyopelekwa,pale nje kulikuwa na wanawake wanaouza miili yao(Dada Poa) na vile vyumba vilitumika kwa shughuli ya short time.

Itaendelea.

Muendelezo soma Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani
Wewe jamaaaa,hivi hii story Ni ya kweli au kufunga?
Asante kwa burudani
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 07.




Kwakuwa Mwakisaka ndiye aliyekuwa mwenyeji wangu sikuwa na hofu kabisa kwasababu ni mtu ambaye tulifanya nae kazi kwa muda mfupi na alikiwa mtu mwema,baada ya kufika kivukoni(feri)tulikata tiketi za kivuko na tukawa tumefanikiwa kuvuka ng'ambo ya pili,baada ya kufika upande wa pili yaani Kigambo,jamaa aliniambia inapaswa tupande gari zilizokuwa zinaelekea Kibada kwa kuwa ndiyo njia yenyewe hiyo.

Tulifanikiwa kufika hapo kwenye mradi mkubwa kabisa uliofahamika kama DEGE ECO VILLAGE,kiukweli nilikuwa nashangaa sana namna ambavyo watu wanatumia fedha,ule mradi ndugu zangu ulikuwa mkubwa mno,na kwa waliobahatika kufika huko au wanaotokea huko watakubaliana nami.

Hatukutaka kupoteza muda kabisa ilibidi Mwakisaka aniambie tuulizie namna ya kupata kibarua kwasababu tulikuta watu wakiwa wanachakalika kinoma.Kuna jamaa tulimfuata tukaanza kumuulizia namna ya kupata kibarua siku hiyo.

Jamaa "Hapa kwetu yupo foreman ambaye ndiye msimamizi wetu,ukienda kule mbele pia wanae foreman wao"

Mwakisaka "Foreman wenu yuko wapi tujaribu kuongea nae?"

Jamaa "Nadhani atakuwa anazungukia maeneo anayosimamia,subirini tu hapa atakuja"

Tulisogea kando tukawa tunaendelea kuushangaa ule mradi wakati huo tunamsubiri mtu tuliyeambiwa ndiye foreman wa hapo tulipofikia.Baada ya muda wa nusu saa jamaa mmoja mweusi aliyekuwa mnene na kitambi cha kutosha akawa amekuja na ndipo yule jamaa alitukonyeza ya kwamba jamaa ndiye foreman wa lile eneo.Tulimfuata na kumjulia hali jamaa kisha Mwakisaka akaanzisha maongezi nae.


Mwakisaka "Kaka tunatafuta kazi ya kibarua "

Foreman "Aliyewaambia hapa tunaajili vibarua nani?"

Mwakisaka "Hakuna mtu aliyetuambia kaka tumekuja kuona kama tutapata"

Foreman "Hapa hatuajiri kwa sasa,siku tukiajiri vibarua mtapata taarifa"

Baada ya yale majibu ya kukatisha tamaa Mwakisaka aliamua akae kimya kisha jamaa akaanza kuondoka kuzunguka nyuma ya yale majengo yaliyokuwa mbele yetu.Sasa yule jamaa aliyekuwa kibarua pale akawa amemuita Mwakisaka akamwambia bila pesa ni ngumu sana kupata kibarua kwasababu hata wao walihonga ndipo kupata kibarua,jamaa akasema twende tukaongee nae kikubwa.Nilimwambia Mwakisaka hiyo kazi ya kuongea na jamaa aniachie mimi,akikataa basi tungerudi zetu kwa Mushi kule kivule kuendelea na ufyatuaji wa tofali.

Niliamua kuzunguka ule upande alokuwa amekwenda yule foreman na bahati nzuri nilimuona akiwa anaingia kwenye jengo moja,nilitembea kwa haraka ili kumuwahi kabla hajafika kwa watu wengi ikawa shida kuzungumza nae.

Mimi "Kaka kakaa"

Foreman "mmmh nambie"

Mimi "Kaka tusaidie ndugu yangu na kama ni chochote tutakupatia"

Foreman "Wewe si ndo upo na yule mwenzio nimewaambia hamna kazi!"

Mimi "Kaka tusaidie ndugu yangu!"

Foreman "Nyie mnatokea wapi?"

Mimi "Wote tunatokea kivule"

Foreman "Kivule?,sasa kivule hadi kuja kufanya kazi huku hamuoni tutasumbuana?"

Aliendelea "Ni bora hata mngekuwa hapa maeneo ya jirani"

Mimi "Tutaweka kambi maeneo haya kaka wala hilo lisikupe taabu"

Foreman "Hapa jirani haturuhusu watu kukaa kwasababu za kiusalama"

Mimi "Sijamaanisha hapa kwenye mradi kaka,tuta tafuta eneo maeneo ya jirani tutaweka kambi"

Foreman "Tukubaliane,mtanipa elfu tano tano kila siku kwa muda wa wiki moja"

Aliendelea "Na iwe siri,ikiwa vinginevyo mi nitawaruka na kuwageuka"

Mimi "Hakuna tazizo kaka"

Foreman "Kamuite mwenzio mje niwakabidhi huku juu!"


Niliondoka kumfuata Mwakisaka na kumueleza kila kitu jamaa alichosema na jamaa akaniambia hakuna tatizo;Tuliondoka kumfuata yule foreman ambaye alituchukua mpaka kwa jamaa wengine akamuacha hapo Mwakisaka kisha akaniambia tena nifuatane nae,mimi pia akawa amenipeleka kwenye kikosi kingine.
Tukaanza kuifanya kazi ya kibarua rasmi na kwa siku tukawa tunapewa elfu 15,ishu ya kula pamoja na maji ya kunywa ilikuwa ni juu ya yako wewe kibarua uzuri ni kwamba,kwenye kundi ambalo mimi nilikuwepo walikuwa wamejitolea kuchanga fedha na kununua vyakula kisha kuna mtu walikuwa wanamlipa anakuja kuwapikia,hivyo na mimi baada ya kuingia kwenye kundi la wale jamaa niliamua kuchangia elfu 10 kwa kila wiki kwa ajili ya huo mpango.

Miongoni mwa wale jamaa pia walikuwa wametengeneza matenti ya maturubai kuishi hapo maeneo ya jirani,niliamua kichangia fedha na mimi ili kukaa hapo,sasa bahati nzuri ni kwamba wikiendi tulikuwaga tunapumzika na hiyo niliitumia kwenda kufata virago vyangu kwa kaka Kileri na kurudi kambini,sikutaka kabisa kuhangaika na mambo ya jiji la Dar es salaam,fokasi yangu ilikuwa ni kwenye kufanya kazi na kutunza malipo yangu kwenye simu.

Nilipopambana ndani ya miezi mitano kwenye ule mradi nilipata kiasi kisichopungua Tsh milioni 1.3,sasa nilimuomba Mwakisaka aniambie ni eneo gani ni zuri kwa kupanga chumba na angalau linakuwa na maisha nafuu kwa hapa Dar es salaam.

Mwakisaka "Mwanangu mimi nakaa Gongo la mboto na nikuzuri sana"

Mimi "Kwahiyo kipindi kile ulikuwa unatoka Gongo la Mboto mpaka Kwa Mushi?"


Mwakisaka " Nilikuwa nakaa kulekule kivule kwa ndugu yangu mmoja"

Aliendelea "Kama unataka chumba we sema nimpigie simu jamaa mmoja pale kitaa akutafutie chumba"

Mimi "Nahitaji kaka"

Mwakisaka "Basi ngoja nitamcheki mshikaji"

Kweli,baada ya Mwakisaka kuwasiliana na jamaa yake na kumjulisha nilikuwa nahitaji chumba jamaa alianza kutafuta na akasema endapo angepata basi angetujulisha.
Baada ya siku tatu yule jamaa aliyepewa kazi na Mwakisaka ya kutafuta chumba akawa amesema nyumba imepatikana maeneo ya mwisho wa lami lakini ni vyumba viwili ambavyo malipo ilikuwa ni elfu 45 kwa kila chumba na ilipaswa kulipwa kwa miezi 6.

Mwakisaka "Jamaa anasema nyumba imepatikana Gongo la mboto mwisho wa lami"

Mimi "Mwisho wa lami ni maeneo ya wapi?"

Mwakisaka "Hapo hapo Gongo la mboto sema ni mbele kidogo"

Mimi "Sawa,na wewe ndiyo unaishi huko?"

Mwakisaka "Hapana,mimi naishi Mzambarauni"

Mwakisaka "Ila jamaa anasema amepata chumba na sebule kwa elfu 45 kwa kila kimoja na inalipwa miezi 6,vp?"

Mimi "Sawa,hakuna tazizo"

Mwakisaka "Ngoja nimwambie amwambie mwenye nyumba atulie kesho kutwa tukakicheki"

Mwakisaka aliwasiliana na yule jamaa akawa amemwambia amwambie mwenye nyumba jumapili tungeenda kukitazama ikiwezekana nilipie kabisa.

Namshukuru Mungu baada ya kwenda kuingalia ile nyumba niliipenda na nikawa nimelipia miezi sita,hela iliyobaki nikanunua godoro na mashuka nikawa nimeyaweka na mimi kufunga chumba kisha kurudi Kigamboni kuendelea na kibarua.

Kila nilipokuwa ninapata hela nilikuwa nikinunua kitu kimoja baada ya kingine na kuweka ndani na hatimaye vyumba vikawa na muonekano mzuri,kiukweli pamoja na mateso ya kushinda juani niliyokuwa nayapitia kule kigamboni lakini nilihakikisha najinyima kiasi kwamba hadi malengo yangu yatimie.

Ule mradi wa Dege kuna muda ukawa umesimama kidogo hivyo kwa muda ule nikaenda kukaa kwangu nilikokuwa nimepanga,sasa pale nilipokuwa naishi kulikuwa na geti na tulikuwa wapangaji kadhaa na kila mtu alikuwa na ishu zake.

Sasa kuna jamaa mmoja alikuwa akiitwa Steve yeye tulitokea kushibana sana na tukawa marafiki,jamaa alikuwa akifanya kazi kampuni ya Tigo kama msajili line za simu,kwakuwa ule mradi ulikuwa umesimama kwa muda usiojulikana,jamaa aliniambia kama vipi aniunganishe na timu leader wake anipatie kodi ya kusajili line za simu nami nianze kuwa msajili laini.Jamaa aliniambia ni kazi ambayo ilikuwa na pesa sana ila watu walikuwa wakiichukulia poa.

Steve "Ngoja kesho nitamueleza team leader kama vipi akupe kodi ili uanze kufanya kazi"

Mimi "Kazi inafanyikaje kaka"

Steve "Kazi ni nyepesi sana kaka utaelekezwa namna ya kuifanya"

Kwakuwa kwa muda huo sikuwa na kazi baada ya kusimama kwa mradi,niliona jamaa atakuwa amenisaidia sana ili kuweza kujinasua na ukata ambao ulikuwa ukininyemelea baada kuwa nakula hela nilizokuwa nimezitunza bila kuzizalisha.



Itaendelea.........
Pole sana bro, shusha vitu
 
Kuna watu wana kipaji cha kusave kutimiza malengo.
Lakini we UMUGHAKA unawezaje kuishi bia demu? Zaidi ya yule Monica mchawi kule kijijini hujawahi simulia kuhusu mwanamke mwingine
 
Back
Top Bottom