Utajuaje kama huna nafsi au umeuza nafsi

Utajuaje kama huna nafsi au umeuza nafsi

Watu wenye nafsi wengi wao hatuna alama M kwenye viganja vya mkono. Ukiwa na M kwenye alama za viganja vya mikono jua kwamba destiny yako tayari ilisha pangwa kama utafanikiwa unafanikiwa kweli na kama ukiwa maskini unakuwa maskini kweli. Mtu asiyekuwa na M ndio mwemye chaguo la maisha yake kupanga kila kitu anachotaka kumiliki katika maisha.

Ukiwa na nafsi ni rahisi kufanikiwa sana kwani nafsi ndio inakuunganisha na mungu aliye juu zaidi kupitia uwezo wa ubongo wako. Mfano simu bila mnara haiwezi kufanya kazi vizuri kwakuwa hakuna network. Ndio hivo kwenye upande wa nafsi ukiwa nayo unaweza kuwa na mawazo chanya mfano amani na upendo na mafanikio kila saa ambapo mawazo haya chanya yanakuungalisha na Universe au Nature.

Kwa sasa angalia vinganja vyako utapata jibu. Tafuta kitabu cha the secret cha rhonda byrne. Nafsi yako ndio inakuunganisha na Most High God kama huna nafsi unaunganishwa na Dark Lord au Luciferiana Order ambapo unakuwa adui na binadamu wenzako kwakiwa unakuwa umetawaliwa na chuki wivu na roho mbaya watu wakifanikiwa unaumia.


Tell me more kuhusu watu wenye M kiganjani. Please all to that...
E.g their life in general, wealth and prosperity, successes and failures im life, Relations and possible remedies to the bad energies associated
 
Kila binadamu aliye kamilika lazima apitie kipindi cha mateso makubwa sana katika maisha yake hiyo ninkawaida cha msingi kuwa na Imani kila nafsi itajaribiwa
Out of topic, Je unaamini uwepo wa majini !? ( Sina uhakika Kama Ni majini au Ni Nini maana nimekuwa katika jamii ambayo inatuaminisha kuwa hao ndio majini ) hapa naongelea Watu ambao Wana pandisha mapepo ' Je ile hali Ina sababishwa na ninini !? Mpaka baadhi ya ile Hali ninini ambacho huwa kina mkuta !?

Katika jamii zetu nimewahi kukaa na watu wenye Hayo mapepo sijui ndio majini ' na huwa yana waingia baadhi ya watu na kuanza kuwashrutisha kufanya baadhi ya Mambo ambayo wao wanayatka na inapotokea binaadamu huyo akaenda kinyume na matakwa hayo maisha yake huwa yanaishia kuvurugika na kuandamwa na mikosi ama wengine kupatwa na umauti kabisa ' je Kuna ukweli wowote katika hayo !?
 
Meditation sio kwa watu wote ni kwabaadhi ya watu. Meditation ni utamaduni wa dini za kihindi ukihusisha mambo ya Yoga. Utaratibubwa dini ya new age ni pamoja na mafundisho ya meditatition. Kwa mtu mwenye nafsi moja au mwenye mungu ndani yake meditation sio kitu sahihi kwake kwani hawezi kuchukuliwa.

Meditation ilianza kuvuma na kuenea kuanzia miaka ya 80 ambapo madawa ya kulevya kama bangi, lsd, na mashroom vilitumika kama ishara ya kutuliza nafsi ya mtu ili kuweza kummunganisha na viumbe wa dimensions nyingine.

Ndio mana meditation inaendana na madawa ya kukevya kama bangi nk ili kumoa mtu uwezo wa kufikia hiyo state of altered reality. Meditation ni nzuri kwa watu ambao hawana nafsi. Ila kama wewe una ile sauti ya chini ndani yako sikushauri juu ya meditation kwani sio kwa ajili ya watubwote ni kwa baadhi ya watu tu hasa souless being Au NPC ndio utamaduni wao.
Okay through hiyo meditation ukisha ifanya. Na kuwakaribisha hao viumbe wengine na kuingia mwilini mwako , huwa unapata faida gani !?
 
Okay through hiyo meditation ukisha ifanya. Na kuwakaribisha hao viumbe wengine na kuingia mwilini mwako , huwa unapata faida gani !?

Hupati faida yoyote Utakuwa umepoteza nafsi yako na watakuwa wamepata kiti. Na cha muhimu hutaweza kuji control ufahamu wako na ikikuzoea mwisho wake utakuwa huwezi kutofautisha mawazo yako na mawazo ya hao viumbe kwani watafunga ile intrnal dialog iliyopo ndani yako
 
Hupati faida yoyote Utakuwa umepoteza nafsi yako na watakuwa wamepata kiti. Na cha muhimu hutaweza kuji control ufahamu wako na ikikuzoea mwisho wake utakuwa huwezi kutofautisha mawazo yako na mawazo ya hao viumbe kwani watafunga ile intrnal dialog iliyopo ndani yako
Okay naomba unijibu post #183
 
Tell me more kuhusu watu wenye M kiganjani. Please all to that...
E.g their life in general, wealth and prosperity, successes and failures im life, Relations and possible remedies to the bad energies associated

Mkuu hii mada ni ndefu ila nitakuelesha kwa ufupi tuu manake ili uweze kusoma alama za vidole vyako lazima ujue misingi mitano ya mistari iliyopo kwenye kiganja cha mkono.

Kuna mstari wa ndoa chini ya kidole kidogo , kuna mstari wa maisha au umri wa kuishi huu umepita karibu na gumba, kuna mstari waa kichwa ni ule wa katikati , kuna mstari wa moyo na mstari wa pesa. Kila mstari una maana yake kulingana na urefu au ufupi wake. Kuna alama nyingine kama X na Delta. Hii alama ya delta ni kama pembe tatu ni wachache ambao wanayo
 
Out of topic, Je unaamini uwepo wa majini !? ( Sina uhakika Kama Ni majini au Ni Nini maana nimekuwa katika jamii ambayo inatuaminisha kuwa hao ndio majini ) hapa naongelea Watu ambao Wana pandisha mapepo ' Je ile hali Ina sababishwa na ninini !? Mpaka baadhi ya ile Hali ninini ambacho huwa kina mkuta !?

Katika jamii zetu nimewahi kukaa na watu wenye Hayo mapepo sijui ndio majini ' na huwa yana waingia baadhi ya watu na kuanza kuwashrutisha kufanya baadhi ya Mambo ambayo wao wanayatka na inapotokea binaadamu huyo akaenda kinyume na matakwa hayo maisha yake huwa yanaishia kuvurugika na kuandamwa na mikosi ama wengine kupatwa na umauti kabisa ' je Kuna ukweli wowote katika hayo !?

Majini wapo wa jamii tofauti sana kuna majini wenye asili ya falme za kiutawala na mali yani majini matajiri ambayo majini wa namna hii hutumiwa na watu wenye pesa nyingi sana kupitia vito na madini ya thamani kubwa kwenye pete mtu hutembea nayo ndiyo huwavuta hawa majini na kuna majini waliotoka katika falme za chini ambao hao ni maskini na mara nyingi hukaa chooni hasa kichafu au majalalani au kutumwa na majini haya ya chini ni rahisi kuyatoa.

Mtu mwenye majini au mapepo wachafu ina maana yake kuwa mtu huyo hana nguvu za kiroho za kumlinda in short hana ulinzi wowote. Ukiona mtu amepandishq haya mapepo jua yeye mwenyewe amekubali kwa kujua au bila kujua mara nyingi huanzia kuweka mikataba yao ndotoni.

Hakuna binadamu yoyote yule mwenye uwezo wa kutoa majini awe mganga au mchungaji au shehe ila tu mwenye uwezo wa kufukuza hayo majini ni huyo aliyekumbwa na hayo majini kujikomboa mwenyewe kupitia nguvu ya nafsi yake afanye nadhiri ya nafsi yake kukataa kuingiliwq na jini au kiumbe yoyote kwani yeye alizaliwa huru na mwili nafsi na roho na ataishi hapa duniani akiwa huru na akifa afe akiwa huru. Kila binadamu amezaliwa akiwa huru utumwa wa majini unakuja pale mtu anapo yakaribisha.

Majini yanatumia hofu kutawala watu ili kuyaondoa inabidi mtu aone thamani ya ubinadamu wake kwanza. Akishaona thamani ya nafsi yake majini hayata msogelea.
 
Utulivu wa nafsi ni mafanikio. Nitoe angalizo tuu kuwa Hii mada sio kwa ajili ya kila mtu ni kwaajili ya watu wachache sana ndio wataelewa.

Kwa mujibu wa tafiti za kiroho inathibitishwa kuwa asilimia 75 ya wakazi wa hapa duniani hawana nafsi. Ikumbukwe binadamu anakamilishwa na vitu vitatu ambavyo ni mwili, nafsi na roho. Nikisema tafiti za kiroho namanisha wenye uwezo wa kuona vitu wanaona jinsi demons au mapepo wanavyoruka kutoka ndani ya mtu mmoja na kwenda kwa mtu mwingine.

Kwa mfano mimi kuna kipindi nilikuwa nashambuliwa sana na demons au mapepo kupitia empty souls au watu wasiokuwa na nafsi ambao wanaingiliwa na mapepo bila wao kujua na kujikuta wakifanya vitu vya ajabu mbele yangu ili kunipa hofu kuwa kuna kituhakipo sawa.

Mapepo walinishambulia sana kwa kupitia watu hawa ambao hawana nafsi mfano nilikuwa nafatiliwa na watu kila niendapo, kila kazi nikifanya naharibiwa au nasambaziwa taarifa za uongo za kunichafua bila mimi kujua. Miongoni mwa vitimbi ni kukohoa ovyo kucheka ovyo na chuki za waziwazi kwa watu ninao wajua na hata nisio wajua au kufatiliwa na watu wanaovaa aina fulani za nguo lakini mwisho wa siku nilishinda mbinu za adui.

Badae nilikuja kupata Maarifa ambayo yalinifungua nikajua baadhi ya siri za ulimwengu ikiwamo baadhi ya siri za mfalme suleiman ndipo nilipojua ukweli kuhusu “Tzvarnoharno” nguvu ya Tzvarnoharno ni kubwa sana. Pale mtu anavyo pata kujifahamu yeye ni nani na asili yake ni nani huanza kushambuliwa katika ulimwengu wa roho kama wewe una roho ndogo unaweza kudhani unalogwa lakini kama ni mtu wa imani utajua ni devil yule mwovu anakujaribu.

Fanya utafiti au reseach juu ya neno “Tzvarnoharno” utajua baadhi siri za mfalme suleimani kwanini aliweza kuwamiliki majini 72 na kuyatumikisha atakavyo.

Chanzo cha binadamu/ watu kukosa nafsi ni moja ni kuzaliwa ukiwa hivyo ukiwa huna nafsi hii inaitwa glitch in the matrix na mbili ni kuuza nafsi ili uweze kutumika kama chombo (vessel/portal) na viumbe wa daraja la chini kama vijini. Mtu mwenye vijini au anayepandisha kijini huyo hana nafsi wala nguvu yoyote ya kiroho na muda wote huwa na hisia kama upepo unaingia mwilini mwake.

Kukosa nafsi kwa lugha rahisi naweza kutoa mfano wa kifaa kama Computer. Bila kuwekwa Operating system computer haiwezi kufanya kazi kwamfano huo ni kwamba ili uweze kutumia vizuri computer ni lazima uwe na Windows bila hiyo windows inakuwa computer ambaye haija kamilika.

Watoto wengi waliozaliwa kuanzia miaka ya 2000 (millennials) wengi wao hawana nafsi ni kama Bots tuu. Maisha yao ni vanity and greedy hawana uwezo wa kuchambua hoja au uwelewa wa kuwa na malengo katika maisha yao. Hawana malengo isipokuwa wachache sana ambao wamebahatikq kuzaliwa wakiwa kamili.

Katika mada zangu nimekuwa nikizungunzia kuhusu negative and positive energies. Negative energy mfano wake ni fears, worrying, hate, green, overindulge in sex, addictions drugs and cigarettes to mention the few.

Kwa upande wa positive energy mfano wake ni definite purpose in life, thinks of love, success, abundance,prosperity,courage and faithfulness to mention the few.

Katika mada zangu nimeweza kuelezea wasomaji wangu wachache kuhusiana na watu ambao ni narcissist au sociopaths ambao ni watu wenye negative energy na vilevile katika mada zangu nimweza kuzungumzia watu wema au wenye positive energy ambao ni empathetic au empaths.

Watoto wengi wanaozaliwa kipindi hichi hawana nafsi kama ukifanya uchunguzi kwa watoto tena ni rahisi sana kwa mtu anayekaa nyumba ya kupanga au uswahilini unaweza ukaona kuna watoto wa aina mbili wachoyo wenye wivu na watundu na vile vile ukaona watoto watoaji na watulivu. “ ondoa mtazamo kuwa hao ni watoto tuu” hakuna kitu kama hicho. Tabia ya mtu ni ile ya utotoni usidanganye hata kama mtoto wako anatabia hizo jua ndio hivo tena. Ndio mana wazee wwa zamani walikuwa wanauwa watoto wachanga kwani waliweza kujua kuwa huyu mtoto hana nafsi nilioewa maarifa kuhusu utamaduni wa kabila la wapare wa milimani kuna utamaduni wao unaitwa Nkumba Vana. Kwa mpare anajua hii ni nini.

Binadamu wanaozaliwa kipindi hiki hawana nafsi kwa sababu dunia kuanzia mwaka 2000 kulianza reincarnation of Souls za wafu wa miaka ya 1800-1900- mpaka mwanzoni mwa 1950 kumbuka kuwa nafsi ambazo zipo katika reincarnation cycle ni zile ambazo zilifeli mtihani wa maisha wakashindwa kufaulu mitihani yao ya maisha hivo inawabidi warudie mitihani yao ili waweze kuendelea mbele 5d au mbinguni.

Ninapo sema kila nafsi ina mtihani wa maisha mfano wake ni kama hivi unaweza kuta matatizo yako ni familia, kusalitiwa, roho mbaya, chuki, kukosa mke mume, kukosa true love au mahusiano, addiction ya madawa ya kulevya au ngono au urahibu wowote ule kwa kifupi mtihani wako wa maisha ili uwende mbinguni ni kile kitu kinachokutesa na kile kitu unachotamani kukiacha kakini huwezi. Kama Ukifabila kukamilisha hicho jua umefeli lazima urudi tena hapa duniani tena mpaka ufaulu.

Take notice kwamba hakuna dini wala maombi yatakayo kufanya uende mbinguni huo ni upigaji wa wanao mwabudu sun god au Black cube ( Saturn worship) huyu Saturn ndio Zohal mungu wa dunia hii au God of time yeye ndio mungu wa dini zote kubwa hapa duniani yeye ndio mkuu wa Matrix. God of many names. Yeye ndiye A kwa waislam na J kwa wakristo.

Kutokana na madhara makubwa ya biashara ya utumwa pamoja na vita vikuu vta dunia na machafuko roho nyingi za wanadamu ziliweza kuona ukatili mkubwa sana katika kipindi hicho na roho nyingi ilizo fia vitani au utumwani hazitaki kurudi tena duniani, ikapelekea hao watu waliofeli mitihani yao kuogopa kurudi duniani ili kurekebisha makosa yao hivyo wameamua kubaki 4d kama mizuka au nafsi za wafu na kutelekeza miili yao ambayo inazaliwa hapa duniani bila nafsi.

Baada ya kutelekeza miili yao watu wanazaliwa bila kujua wema au roho nzuri au kujali wengine.

Mtu ambaye hana nafsi atajijuaje mwenyewe au atajigundiaje? Hii ndio msingi wa mada yangu maelezo ya hapo juu ni kwa ajili ya kujenga hoja ili watu wangu waelewe nini chanzo.

Binadamu yoyote anakuwa na mwili na roho kwa kuwa na vitu hivo viwili anaweza kuonekana mkamilifu kwa kuwa anakula anakunywa na kuzungumza na anaweza hata kuzaa watoto lakini bado ndani ndani yake hajakamilika. Kwani kuna kitu kakosa ambacho ndio nakiweka bayana hapa.

Binadamu ambaye hana nafsi inamana kwenye akili au ufahamu wake hana ile internal dialog. Nikisema internal dialogue namaniaha kuwa kuna kile kisauti kipo kichwani kwako mfano ukiwa unatembea unafikiria uende wapi au ufanye nini au ukitaka kufanya kitu kibaya sauti hiyo inakupa onyo kwamba usifanye kitu hicho. Mfano ukiwa umelala au unataka kulala unaweza kuwa unawaza mawazo yako hata kama umewasha feni au redio unawaza japo kuwa kuna kelele mawazo yapo.

Mtu ambaye hana nafsi hawazi chochote isipokiwa kilichopo mbele yake wala hana utashi wa kutofautisha kati zuri na baya kwakuwa akili yake na mawazo yake yametulia muda wote huwa anakuwa na utashi wa kuwaza kitu kimoja tuu. Mfano kama anasoma hii mada atasoma tuu maandishi lakini hata waza kuwa ndani ya maandishi kuna nini au ujumbe gani. Mfano akiangalia sinema huwaza starehe ya kutazama bila kujua funzo la sinema hiyo ni nini.

Nafsi ndio operating system ya mwanadamu mtu ambaye hana nafsi anakuwa kama binadamu wa kawaida tofauti ni moja tuu hana hisia au sauti ya kumwonyesha kitu kizuri na kibaya. Anachoangalia ni jambo la kumfurahisha mwili wake na mahitaji ya kimwili tuu au kumridhisha yeye mwenyewe hawazi kuhusu wengine. Hana mahitaji ya kiroho kabisa.

Binadamu mwenye nafsi ni ngumu sana kufanya vitu kama meditation kwani mawazo yake hayapo tayari kusimamishwa ili kichwani kwake kubaki empty ili ufahamu wake uvamiwe na kiumbe kingine asicho kifahamu. Nilisha zungumzia mambo ya meditation kwenye mada ya New Age Religion.

Kwa wale wanaofanya meditation wanajua kuwa inabidi uweze kusimamisha mawazo yako yote usiweze kuwaza kitu chochote kitu ambacho ni kigumu sana kwa mtu mwenye nafsi hawezi kabisa kufanya meditation hata akijaribu ataishia kuwaza mambo yake au kupitiwa na usingizi. Mtu ambaye hana nafsi ni rahisi kufanya mesitation.

Vitu kama meditation ni hatari sana kwa mtu mwenye nafsi inaweza kusababusha ukawa kichaa kwakuruhusu ufahamu wako kuvamiwa na kiumbe usichokijua baada ya wewe ku shut down mawazo yako kichwani ukawa empty head. Ni sawa na kuingiza Virus katika mfumo wako.

Anyway kwa mtu ambaye amezaliwa hana nafsi ataishia kuwa mfuasi wa dark lord na mtu mwenye nafsi ataishia kuwa mfuasi wa Light. Mtu ambaye alikuwa na nafsi kisha akauza nafsi anaweza kuirudisha nafsi yake ila sio kwa maombi bali kwa nia yake ya dhati. Kiumbe aliyeuza nafsi anatawaliwa na asili ya hofu inabidi apambane nae as he walked in the valley of shadow of death and darkness he shall fear no evil.

Ni vigumu kuandika kila kitu hapa.

Reincrnation and past life read the book [emoji1313]View attachment 2040553
Mimi nimekwelewa sana jinsi ya kuingia pm sijui ntakupa vip kuongea na wewe mengi zaidi au naomba pm
 
Mkuu hii mada ni ndefu ila nitakuelesha kwa ufupi tuu manake ili uweze kusoma alama za vidole vyako lazima ujue misingi mitano ya mistari iliyopo kwenye kiganja cha mkono.

Kuna mstari wa ndoa chini ya kidole kidogo , kuna mstari wa maisha au umri wa kuishi huu umepita karibu na gumba, kuna mstari waa kichwa ni ule wa katikati , kuna mstari wa moyo na mstari wa pesa. Kila mstari una maana yake kulingana na urefu au ufupi wake. Kuna alama nyingine kama X na Delta. Hii alama ya delta ni kama pembe tatu ni wachache ambao wanayo
Sawa sawa nakupata kabisa description hii ila hujaelezea hata kidogo kama ulivyoahidi.
1. Msitari wa ndoa ni mrefu unagusa ngozi nyeusi.
2. Mstari wa maisha upo kama unafika kwenye ungio la kiganja na mkono ila unafifia fulani ivi then unagawanyika vistari 3 kistari kimoja kinagusa na kukatiza moja ya mstari unaotengeneza x. Kistari kingine nafikiri tuki ignore. Alafu kinachobaki kinafika kwenye joint.
3. Mstari wa kichwa moyo na pesa apo sijajua which is which in this x.

Mi naona x.sio delta. Tell me about x and delta. Tell a bit kuhusu urefu au ufupi vinamaanisha nini
 
Tell me more kuhusu watu wenye M kiganjani. Please all to that...
E.g their life in general, wealth and prosperity, successes and failures im life, Relations and possible remedies to the bad energies associated
Sijawahi kuamini Mambo ya viganja,Kuna mtu niliwahi kutana nae akasema anaweza kujua destiny yangu,Mambo aliyotabiri hayajawahi kamilika na Mimi Nina M...Alichokuja niudhi akasema kitu Cha mwisho nakiona katika Maisha yako you will faint'"nikashangaa kufaint Tena ndio nini?Akajibu kwa sauti ya chinichini "UTAKUFA"nikamuuliza Sasa kifo changu nacho Ni utabiri?Hicho so ndio kitu pekee kwenye Maisha yangu nilicho na uhakika nacho?jifanye nifanyavyo nitakufa tu,,Aaaaah nikaona hizi Mambo za michoro ya mkono magumashi tu.
 
Sijawahi kuamini Mambo ya viganja,Kuna mtu niliwahi kutana nae akasema anaweza kujua destiny yangu,Mambo aliyotabiri hayajawahi kamilika na Mimi Nina M...Alichokuja niudhi akasema kitu Cha mwisho nakiona katika Maisha yako you will faint'"nikashangaa kufaint Tena ndio nini?Akajibu kwa sauti ya chinichini "UTAKUFA"nikamuuliza Sasa kifo changu nacho Ni utabiri?Hicho so ndio kitu pekee kwenye Maisha yangu nilicho na uhakika nacho?jifanye nifanyavyo nitakufa tu,,Aaaaah nikaona hizi Mambo za michoro ya mkono magumashi tu.

Tunasikiliza tu, then we wont give a damn😊🤩
 
Sijawahi kuamini Mambo ya viganja,Kuna mtu niliwahi kutana nae akasema anaweza kujua destiny yangu,Mambo aliyotabiri hayajawahi kamilika na Mimi Nina M...Alichokuja niudhi akasema kitu Cha mwisho nakiona katika Maisha yako you will faint'"nikashangaa kufaint Tena ndio nini?Akajibu kwa sauti ya chinichini "UTAKUFA"nikamuuliza Sasa kifo changu nacho Ni utabiri?Hicho so ndio kitu pekee kwenye Maisha yangu nilicho na uhakika nacho?jifanye nifanyavyo nitakufa tu,,Aaaaah nikaona hizi Mambo za michoro ya mkono magumashi tu.

Cause you know, everything is F*cked up anyway... mimi nimepitia uzi huu kuna stuffs zipo alarming... apo alipotaja M nimestuka na kuwa curious aniambie stuffs zaidi anazojua nirelate. Na mimi ni msomaji mzuri wa vitabu na motivations but huwa nina add my common sense to what i read. Ninajua khs meditation toka kitambo na nimefuatilia sana about it and each time and reason they give i definitely dont buy it sijawahi na stowahi kushawishika kufanya meditation. Nimekisoma hicho kitabu alichotaja THE SECRET CHA RHONDA BRYNE kilikua kinaniletea ukakasi sana yani ni magic tupu... its all cheap coffee... i just cant be that much insane nimeisha mdiscredit aliyekirecommend eti ni life changing book
 
Labda kwa kukujibu tu ni kwamba huo mstari ni kwaajili ya kutengenezea watu wenye nafsi hofu. Kufa lazima kila mtu afe lakini sio mauti. Kuna tofauti kati ya kufa na kuonja mauti.

Watu wenye nafsi pindi wakifa wana option ya reincarnation kurekebisha makosa yao na watu ambao hawana nafsi hawawezi kuwa na nafasi ya reincarnation wanapokufa na story yao inaisha.. Nita ku tag
Mi ningeomba kuuliza japo si kwa umuhimu, najua wewe sio muumini wa dini wala vitabu vya dini ila kwanini unatumia sana mifano yako kutoka kwenye biblia kuliko kwenye vitabu vyengine?
 
Tuna tishika kishenzi kuusu kifo naawa ma shekh nama pastor kumbe Ni kutoa ofu [emoji120][emoji120][emoji120] kinacho takiwa nikufwata sheria tu[emoji120][emoji120]
Akili za kuambiwa changanya na za kwako, ila utegee kuambiwa kuhusu kifo na watu wengine hali ya kuwa hata hao watu hawajawahi kufa na kurudi kama wewe tu hivyo wote hamna experience kuhusu kifo? Masheikh wanaokutisha kuhusu kifo hawajawahi kufa na huyo anayekwambia kifo hakitishi pia hajawahi kufa sasa hapo utawezaje yupi mkweli?

Cha msingi na wewe fikiria kivyako kwa akili yako kuhusiana na kifo na jibu utakalo lipata ndio lishike hilo hilo kwanini utegemee watu kukwambia?
 
#JAMES WEB TELESCOPE NA DINI

wanasubiri chombo ifanye yake utukufu wapeleke kwenye dini zao, utawasikia "Quran ilishagaandika" au "bibilia ilishagaandika" are you serious?

Binafsi naamini Mungu Ila siamini dini, dini ni mfumo tu ulioanzishwa na wadamu usikae kwenye dini yako kisha ukaanza kusema dini zingine za uongo

Hii ndo imefanya kuwe na mtafaruku na uvunjifu Wa amani duniani

Nilikutana na mtu mmoja mm nilikuwa nakula ice cream asubuhi akaniambia "imani yangu ni kutokula ice cream wakati Wa asubuhi" nikamjibu it is fine usile, akaniambia "hujanielewa, namaanisha kutokana na imani yangu ya kutokula ice cream wakati Wa asubuhi wewe pia huruhusiwi kula ice cream wakati Wa asubuhi, nikamuangalia usoniiii nikaangalia na viatu alivyovyaa nikaamua kuachana naye"

Hivyo ndivyo dini zinavyofundishwa
Tunalazimishana kuamini kitu Fulani

Mnakaririsha hadi watoto wadogo wawaite wasioamini makafiri, au wanaokula nguruwe waitwe makafiri wakati huo huo hujui ukiupungukiwa damu unaenda hospitalini kujazwa damu ya nani? Ni ya hao hao makafiri wala nguruwe ambao damu yao Ina chembe chembe za kitimoto

Leo mkristo anaamini yesu ni Mungu wakati akisilimu anaamini yesu sio Mungu vise versa kwa msilamu anaamini yesu sio Mungu lakini akibadili dini na kuwa mkristo anaamini yesu ni Mungu

Dini ni Kama kuandika namba 6 chini

Tukikaa pande mbili tofauti mm nitaiona 6 wewe utaiona 9 kwahiyo wewe kuwa sahihi haimaanishi Mimi Niko wrong, you have not seen the life by my side, ukija upande wangu utaiona ni 6 na utakubaliana na Mimi

Kibaya zaidi tunatishana eti usipoamini dini Fulani unaenda motoni[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wrong huo ni uvivu Wa kufikiri

Ebu fikiria kuhusu Eskimo walioko Greenland ambao hawajui uislam wala ukristo je akifa anaenda motoni sababu hakuwa muislam au mkristo? Kama jibu ni ndiyo hamuoni Kama anaonewa kwa kuhukumiwa kwa kitu ambacho hakijui?

Kama ataenda mbinguni kwanini nyinyi mnajitia kihelehele kuwasambazia watu dini zenu worldwide badala muwaache wafe wakiwa hawajui lolote ili waende mbinguni? Maana nyinyi hamuwapendi wasioamini mnataka muwaingize mkenge kisa nyinyi mshaingia mkenge

Lakini je babu Wa babu Wa babu Wa babu Wa babu Wa babu Wa babu Wa babu yako yuko mbinguni au motoni anababuka tu[emoji23][emoji23] maana alikufa ilihali sio msilamu au mkristo

Tusikaririshane kwamba uislam au ukristo ndo dini sahihi na kupeleka utukufu kwenye dini zenu

India tu pekee kuna dini zaidi ya 1000, je umefatilia hizo dini zote ukaona Kama ni za kweli au uongo?
Na je ukweli ni upi na uongo ni upi?
Unatumia vigezo gani kusema huu ndo ukweli na huu ndo uongo?

Alafu Kama kweli dini zenu ndo kila kitu je Mungu Wa wakristo ndo huyo huyo Wa waislam? Kama jibu ni ndiyo je mbona ahadi zake zinatofautiana?

Ninavyojua Mimi kila mtu ananamna yake ya kutafsiri mungu/Mungu whatever utakavyoita mwingine anaamini ni Energy mwingine anaamini ni laws of nature(kanuni za asili) na mwingine anaamini ni "personal being" kila mmoja yuko sahihi kwa tafsiri yake sababu hakuna common standard ya measurement ya tafsiri

Dini ibaki Kama dini na kila mtu abaki na imani yake na sayansi ibaki mam sayansi na mambo yake

James web telescope itatuambia vingi kuhusu universe tunatumaini itatusaidia kukomboa maswali mengi zaidi ambayo zamani yalikuwa chini ya mwamvuli Wa dini Ila sayansi imekuwa ikiyakomboa na imeendelea kuyakomboa na itafanya hivyo sikuzote

Usichanganye sayansi na dini hutakawia kusema "jamaa wanakufuru wanataka wamchunguze mungu/Mungu" kitu ambacho si kweli
Umeelezea kuhusu dini ila vp kuhusu imani ya kuwepo Mungu? Hivi binaadamu anazaliwa akijua uwepo wa Mungu au ni jambo analolijua kupitia kwa wazazi wake au jamii aliyopo?
 
Kwa muda mrefu sana nimepitia sana hali uliyoieleza,
Pmj na kusoma lkn niliishi kwa hofu kubw sana,
Wasiwasi, hasira, kutojiamin, mambo kuharibik sna,
Ulevi, uzinzi nk.
Ni maisha ambayo yalinitesa sn huku nikiwa kama mtu aliyetekw mateka lkn anajitahid sn kujinusuru,
Mungu si athumAn,
Lkn baad ya kuanza Tiba ya chumvi na kuanza tiba mbadala/asili.
Kw sasa nimepona, na nikikumbuk namna nilivyotumikishw, nahic Kulia.
mambo ni mengi kuweza kuyaandik yote.

SWALI

Sijaelew lbd nilichezew tang utoton au ndio hii ya kuzaliw bila nafsi hlf ??
Uliposhiriki uzinzi ndipo uliruhusu roho chafu zikuharibie
 
Mimi sio muumini wa theory ya creation kutoka kwenye bible au quran soma mada zangu. Wala sina cha kitu cha kunishawishi kuna kitu kinaitwa creator. Ila nachojua nipo, nilikwepo na nitaendelea kuwepo. Ukisoma
Mada zangu nilisha zungumzia chimbuko la binadamu na nikaweka wazi msimamo wangu kuwa adamu na hawa ndio creation na walikuwa wamefungiwa mahali wasichamgqnyikane na binadamu wengine wenye nafsi. Chimbuko la adamu na eva ndio hawa watu ambao hawana nafsi.
Naomba link ya mada uliyozungumzia creation mkuu
 
Back
Top Bottom