Utakaa barabarani mpaka ufikishe miaka 90?

Hii ninaiona hata kwangu inavyonitafuna kidogokidogo. Hatuna ubunifu kabisa. Tazama siku hizi nyumba zote zikijengwa eti zinawekwa fremu. Mtaa mzima ni fremu tupu. Yani kuchungulia fursa tofauti imekuwa changamoto sana.

Lakini, pamoja na juhudi binafsi kuhitajika, serikali pia ina nafasi katika hili,kuanzia "elimu hai" mpaka kujenga mifumo mizuri ya kiutawala na uchumi.
 
Kwahiyo solution ni kupoteza nguvu za ujana wako pembezoni mwa barabara? Hahaha
Kwao ni solution maana hawana haja na career kwa kazi wanazofanya, wametoka maisha ya jamii yao ya Bora liende hivyo vilimo vya kisasa na biashara rasimi nizawatu wanaojiweka kwenye mfumo wa kuwa na career zinazotambulika na nini wanafanya Ili kujiingizia kipato ila hao wakukaa barabarani wao walichagua kuishi nje ya mfumo wa rasimi na career mpaka kufa.
 
Uchoyo pia unatunyima nafasi, Wazungu wanakaribisha vijana wenye mawazo mapya na pesa ya mitaji kuanzia €250,000 wanapewa visa katika nchi zao.

Pia wanaomaliza na first class wanalengwa kuwa mameneja wa makampuni.
 
Uchoyo pia unatunyima nafasi, Wazungu wanakaribisha vijana wenye mawazo mapya na pesa ya mitaji kuanzia €250,000 wanapewa visa katika nchi zao.

Pia wanaomaliza na first class wanalengwa kuwa mameneja wa makampuni.
Hhaha! Sisi mpaka tubadilike kifikra aisee. Tuwaoga kishenzi.Na uoga unaletwa na huu ujinga tulionao.
 
Maamuzi yao yanafanya miundombinu iliyojengwa kwa kodi zetu kuharibika, na watu kushindwa kutumia hiyo miundombinu ipasavyo. Sehemu zile ni za watembea kwa miguu ila hawaruhusiwi kupita kwenye maeneo yao waliopangiwa kwasababu ya watu ambao ni wavivu.
 
We acha tu watu hawataki kufikiri zaidi na kupanua mawazo.
Eti kuna watu kwenye huu uzi wananiomba fursa ili watoke barabarani. Mhmm ukisikia maajabu ya dunia utayakuta Tanzania.
 
Kwa maelezo yako inaonekana umekulia mjini dada,tuliokulia kijijini tunaelewa urahisi na ugumu wa maisha ya kijijini.
Yes,kula kijijini kama unajituma utakula maana unalima mwenyewe.kasheshe inakuja pale unapotakiwa kuvaa,kupelekea watoto shule.unajikuta mazao ya kuuza unayo ila bei mgogoro,ref.gunia la mahindi elfu 30-50

Kwenda hospitali endapo utaumwa,hakuna anayekubali kupokea mazao akupe dawa,ukienda kuuza unakutana na mkono wa walanguziref.bkb mkungu mkubwa wa ndizi ijulikanayo kama mtwishe sh.elfu tano na wanunuzi hakuna na bado zinaiva na kuozaTukitaka vijana wake vijijini tuboreshe masoko na kujenga viwanda vya kuyaongezea mazao thamani hapo tutavuka
 
awajaamua kua serious na kuchakata ubongo..wengi hawapendi kujichosha wanapenda mteremko kitu ambacho hakiwezi wafikisha popote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…