UTALII WA KILIMO: Hiki ni kitu nilichokishuhudia wakati natafuta fursa za Kilimo Mkoa wa Iringa

UTALII WA KILIMO: Hiki ni kitu nilichokishuhudia wakati natafuta fursa za Kilimo Mkoa wa Iringa

Na hii je?
IMG-20250217-WA0045.jpg
 
Video ni shamba ya marekani/ulaya, mbona unatutoa mchezoni?
Nashukuru wale jamaa wamepiga niadd kwenye group lao la wakulima wa Parachichi baada ya kuonesha interest kwenye kuwekeza kwenye kilimo cha zao hilo.

Hii video nimeitoa kwenye group lao la Parachichi. Je hii nayo sio Tanzania huko Iringa ndanindani?
 
Safi Sana Kwa moyo wa kipekee mkuu,naomba kufahamu Nyanzwa yalipo hayo mashamba ya 50000 vipi mvua zipo Kwa wingi kiasi gani na zao gani linasitawi huko.?
Kwa maelezo yao mkuu. Kuna changamoto ya unyeshaji wa mvua ila kuna faida kwani kuna skimu ya umwagiliaji ambayo wakulima wanalima kwa kumwagilia.

Pia kuna mpango wa kujenga bwawa kubwa la kuhifadhi maji ya mvua ambayo yatatumika kumwagilia kwenye mashamba ya wakulima.

Bro kilimo cha Mbegu za vitunguu kinalipa sana. Jamaa wanauza tsh 20,000 hadi 30,000 kwa kilo moja ya mbegu za vitunguu.
 
Kwa maelezo yao mkuu. Kuna changamoto ya unyeshaji wa mvua ila kuna faida kwani kuna skimu ya umwagiliaji ambayo wakulima wanalima kwa kumwagilia.

Pia kuna mpango wa kujenga bwawa kubwa la kuhifadhi maji ya mvua ambayo yatatumika kumwagilia kwenye mashamba ya wakulima.

Bro kilimo cha Mbegu za vitunguu kinalipa sana. Jamaa wanauza tsh 20,000 hadi 30,000 kwa kilo moja ya mbegu za vitunguu.
Nikiwa natokeaMwanza nishukie wapi mkuu ili kwenda Nyanzwa
 
Hayo maeneo yote nayajua,hapo ruaha mbuyuni kuna wasagara sio poa,utalima ila utavuna guniamoja tu,kunachangamoto sana hapo,kwanza mto lukosi una tabia ya kuhama,wadudu waharibifu,kikubwa uchawi hatari,wanalimia dawa hapo.

Mtandika A and B pako powa,
Ilula sokoni ilula mtuwa kote huko nimevuruga japo sikumbuki kuona mto Kama ruaha mbuyuni ambako kuna mito miwili
Wasagara wakoje ebu fungua code unavuna gunia moja inakuawaje hio?
 
Malinyi ni wilaya,na Mahenge ni makao makuu ya wilaya ya Ulanga.
Kijiji cha Ruaha upatikani baada ya kupita Mahenge kama unataka kuelekea milima ya Sali hadi hifadhi ya mbuga ya Ruaha ipakanayo na mbuga ya selous Morogoro kusini kuelekea Liwale Lindi.
Pana bonde kama heka mia Tano au mia 700 nusu linamilikiwa na kanisa katoliki waasisi ni wajerumani enzi za utawala wa Wajerumani Bonde linalimwa mpunga mwka mzima maji yapo mtoni mwka mzima masika pekee mto unageuka bahari.
Hilo bonde ukichimba mita sita usawa wa shimo la choo unaanza kutana na dhahabu.
Dhahabu ilitoka kwenye safu za milima ikamwagika bondeni miaka.
Mazao unayoweza lima pale ni vitunguu, viazi mviringo vitamu, mahindi,nk.
Hali ya hewa ni joto kama la Dar but pembeni mwa bonde ni baridi kidogo usiku ni baridi sababu ya milima.
Habari njema sana hii
 
Wachawi sana na wana roho mbaya,wanaiba mazao kimazingaombwe shambani
Duuh hatari sana, kwahio umenyoosha mikono kwa wasagara? Watu wa Ruaha mbuyuni wanakula Bata sio mchezo vigoma kila siku hasa nyakati za mavuno ya nyanya na vitunguu ni nyoko
 
Inaendelea:
Pale farm for the Future pia wanaprogarm ya Young Mothers. Katika program hiyo, husapoti mabinti waliozalishwa na kutelekezwa na wenza wao au kukatishwa masomo tokana na kupata ujauzito.

Mabinti hao husapotiwa kwa kupewa elimu ya Kilimo, Ufugaji na ujasiliamali kisha hupewa mitaji kama ya mbuzi au mashamba au vifaa vya ujasiliamali na kusimamiwa ili waweze kujisimamia wenyewe kiuchumi.

Shamba hilo lililo chini ya taasisi fulani ya kidini toka nje ya nchi wana mradi wa shamba ambapo hulima mbegu za mahindi kwa ajili ya SEEDCO lakini pia wamepanda karanga mwitu, viazi na Alizeti. Jamaa wana Advance technology nami niliona mengi wa mara ya kwanza kwenye maisha yangu.

HOLISTIC FARMING.
Nimechoka nitaendelea kesho.
View attachment 3236560
Nimeipenda hii ......malizia tafadhali
 
Back
Top Bottom