Utalii wa ndani kwa watoto hasa hawa wa shule za Msingi na Sekondari

Utalii wa ndani kwa watoto hasa hawa wa shule za Msingi na Sekondari

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,446
Reaction score
1,645
Habari Tanzania !

Naomba kuuliza kwa kukaribisha hoja ya Utalii hapa nchini. Je, hatuwezi kuwa na Utalii wa ndani (Domestic Tourism) kwa kuwapatia watoto wa Shule za Msingi na Sekondari (Serikali na Binafsi) haki ya kuona vivutio vya nchi yao na hii kitu iwekwe kwenye mitaala ya Elimu yao.

Yaani Utalii wa ndani ujengwe kama jambo la lazima na tupandikize shauku kwa hawa watoto watambue Vivutio vya nchi yao, tuwajengee morari nzuri ya kuwazia taifa lao vizuri kuliko ilivyo sasa. Kwa wachache sana hasa wale watoto wa daraja la juu kiuchumi ndio unufaika na hii huduma ukilinganisha na watoto wa tabaka la kati na chini.

Ombi kwa Wizara ya Mali asili na Utalii ongeeni vizuri na wenzenu wa Wizara ya Elimu waweke hii kitu kwa watoto walau kwa mwaka wawe wanatembelea vivutio visiopungua 4 na kukiambatana na maswali ya utashi ili tuwapandikizie nia njema.

Asante.
 
Back
Top Bottom