Kipindi nasoma nilipata demu mmoja kitaa mrembo haswa, nikasafiri kwenda mkoani kusoma tukawa tunawasiliana kwa simu tu
Likizo ilivyofika nikam alert kua nakuja, nikastukizwa hapo hapo na habari mpya kua ye mgonjwa anaumwa asthma na muda wowote ataenda njombe kutibiwa
Nikawa najiuliza kama ugonjwa umefikia mpak hatua hiyo ya wewe kuhitaji matibabu ya kwenda mkoani maana yake upo critical, lakini mbona siku za nyuma hukuwahi kuniambia au kuonesha dalili zozote za ugonjwa?
Halafu mbona ghafla hivi yani kwanini iwe siku ambayo nakuja mimi na wewe ndio iwe siku hiyo hiyo ya kondoka?
Nikamwambia basi nabadilisha ratiba nakuja siku kabla ya wewe kuondoka na ikiwezekana nakusindikiza hadi huko
Akakubali kinyonge
Nikamwambia kesho naanza safari akasema poa, nilivyofika usiku nikiwa stend nikampigia aje akasema ametingwa sana hajiskii vizuri, nikamuacha
Asubuhi yake majira ya saa 10 alfajiri nikatumiwa meseji kua kulingana na hali ilivyo nibadilikia hapo jana, wazazi wamenambia niende hospitalini leo
Pale pale nikamjibu kuwa sawa basi ngoja nije hapo stend uzuri nina usafiri sito chukua muda, akajibu akasema "yani hivi ndo napanda gari na limeanza kuondoka lala tu baby usijisumbue tutaonana nikirudi"
Siku moja nikapita mitaa yao nikiwa na mshkaji wangu kucheki hivi nikaona demy ana bonge ya litumbo, nikamwambia msela ebu simamisha kwanza nijionee vizuri
Kushuka hivi nikagongana naye macho akashtuka akiwa haamini kama nimemsanukia na mimba yake, nikarudi zangu huyo tukaamsha.
She asked for forgiveness I said No, I'm not a God so I'm not a forgiver