Utamkumbuka Edward Lowassa kwa mambo gani?

Nakumbuka jinsi Msukuma alivyomsema eti anapupu wakati anatembea.

Wanasiasa ni watu wa hovyo sana.
 
Tushawahi cheza mpira wa miguu team magu vs team lowasa 2015 nilikua team lowasa
 
Kusambaza Mtandao wa Maji Mikoa Ya shinyanga Tabora na Mwanza sasa hivi hawana shida ya maji..
Kuanzisha shule za kata Nchi nzima kwa sasa 85-89% ya Vijana wote wamefika Form four..
NA MENGI MAZURI KAFANYA SANA..
 
Very interesting. Lini ulihamia kwa Magufuli?
 
Kampeni zake 2015 zilikua zinachekesha sana eti mara masheikh wamfuate mara maaskofu na wachungaji eti wanamtaka awe rais, kuna siku alipanda daladala la kwenda buguruni kaka kiti cha dirishanu.
 
 
Tunakumbushana tu maneno ya mwendazake Lowasa alipotangaza Kujiuzulu na Bunge zima kushikwa na Mfadhaiko

Mlale Unono 😀😀🔥
 
Kiukweli Lowassa alikuwa kiongozi aliyeandaliwa kama alivyosema Ryoba
 
Aliacha kwasababu hakuna anachopoteza wadhifa wa waziri mkuu mstaafu kuhudumiwa hadi mwisho uko palepale na pesa kapiga
 
Lowasa alikuwa ni kati ya viongozi waliopata bahati ya kuzaliwa kizazi ambacho wale wachache walioweza kupata elimu kipindi hicho na kuichagua siasa kama sehemu yao ya maisha, wana maisha mazuri sana.
Kwenye siasa kuna kuanguka, kuna kusalitiana kwenye makubaliano, kuna kuogopana katika upana wa maendeleo binafsi, ambapo nashuhudia viongozi wengi wana muelezea Lowasa alivyoanguka kwenye mbio za urais 2015, alivyojiuzulu Uwaziri Mkuu, kama anguko la kisiasa la asha.....matukio hayo mawili ni matukio makubwa katika siasa za Afrika ambapo ni mfano wa kuigwa......bara letu la Afrika kwa ubinafsi na uroho wa viongozi wafia tumbo ni ngumu kiongozi mwenye madaraka ya Uwaziri Mkuu kuandika barua kwa Rais kuomba kujiuzulu ni ishara ya uwajibikaji hili, Mh. Lowasa katufundisha kwa vitendo, inaweza isitokee, lakini kubaki tu kwenye kumbukumbu tu, inatosha.

Misingi ya kusalitiana kwenye makubaliano ya kisiasa, naamini uwoga wa baadhi ya wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi kwenye dhana ile ile ya uwajibikaji, ule ushujaa uliogopesha wengi kwasababu wanasiasa wengi wanaogopa kuwajibika, lakini namshukuru Mwenyezi Mungu, kwenye ule msemo mchagua nazi sana mwishowe anachagua koroma ndivyo ilivyotokea alikatwa Mh. Lowasa akaingia Chuma (R.I.P) Dk. magufuli, moto uliwaka na kikubwa ambacho nakumbuka ajenda ya Lowasa ya Elimu bure, Chuma aliiendeleza, Rais wetu Mama wa Taifa naye anaiendeleza hii ni heshima ya kipekee sana, ingawa hawakumchagua Urais kwasababu ya uwoga wa baadhi ya watu.

Mimi binafsi nakushukuru sana uliingia mgogoro na serikali ya Misri kwasababu ya watanzania wao wakitetea mto Nile, na wewe ukitetea ziwa Victoria watanzania wafaidike na maji hayo.....leo hii sio kama kipindi chetu darasa moja la watoto 100 wanachaguliwa 3 kuendelea na masomo ya sekondari, siku hizi darasa zima linaendelea adui ujinga anakaribia kwisha ndani ya nchi hii, naamini tuliokuwepo tupambane kwenye kubadili mitaala ya elimu ili iwe msaada kwa watoto....Mh. Lowasa kaacha alama yake.....tuliobaki tuache ya kwetu.
Pumzika kwa Amani Baba yetu......ni kweli bendera zinapaswa kupepea nusu mlingoti, Taifa Linakulilia..[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…