Utamkumbuka Edward Lowassa kwa mambo gani?

Yaani leo amefariki ndio mnasema yote haya,Kwanini hamkusema alipokuwa bado hai?.Anyway sawa.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Mtangazaji Mwandamizi wa Clouds media ndugu Mwijaku amesema yeye binafsi amshukuru sana mzee Lowasa kwa kubuni na kujenga shule za Kata

Mwijaku amesema yeye mwenyewe amesoma shule za Kata na sasa amekuwa Mtu Maarufu sana nchini na Duniani

Source: Clouds Radio
 
kwamba CCM mlimuibia kura zake za urais
 
Mbona wanasema jamaa hajawahi kuiba chochote huko serikalini..
 
Ufisadi wa Richmond amekufa pasipo kutoa siri ya Richmond ilikuwa niyanani kati ya Yeye na Mkwere.Lowassa nikati ya wanasiasa waliochangia umasikini kwa watanganyika kwa ufisadi wao na Mkwere,by Dk Slaa voice.
Hizo ni siasa za majitaka, Dr Lowassa hajawahi kuiba hata pen ya mtu sembuse kuwa fisadi. Achen kumchafua bwana.
 
Namkumbuka kwa ufisadi
kingine nachomkumbuka zaidi ni utapeli aliowafanyia UKAWA.
akawa anajisahaulisha badala ya peoples power! akawa anasema CCM hoyee!
 
Kuna wakati bwawa la mtera lilikauka kupita kiasi.akiwa waziri wa maji alifuatilia jambo hili kwa umakini mkubwa ikagundulika kuwa kuna watu wamechepusha mkondo wa mto Ruaha kwa kuelekeza maji kwenye mashamba ya mpunga
baada ya kufunga hiyo mifereji kuelekea hayo mashamba na maji kurudi kwenye mkondo wake wa kawaida bwawa la mtera lilirudi kwenye ujazo mzuri wa maji.alikuwa akisimamia jambo alikuwa makini na mfuatiliaji
zaidi sana alikuwa na hofu ya Mungu
Na jambo kubwa ninalojifunza kwake ni kukaa kimya hata kama watu wanakusema vibaya katika jamii.
bila kupunguza ukali wa maneno au kuficha mambo, kuna baadhi ya viongozi walifikia hatua ya kumdhihaki Ndugu yetu Lowassa kuwa anajinyea.na kuwa atafia Ikulu.mwingine akafikia kupiga jaramba jukwaani japo sina uhakika kama alikuwa miongoni mwa waliodhihaki.nasema sina uhakika kwa kuwa sikumsikia kwa kauli yake akimtaja ndugu yetu Lowassa kuwa ni mgonjwa.lakini wapo waliofikia kusema kuwa hawapo tayari kufanya uchaguzi wa marudio kwa kumchagua mgombea mgonjwa
Tuwe makini katika kusema
 
Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere itakuwa alikuwa Team Jakaya maana alishinikiza Lowassa ajitoe kwny mbio za Urais 1995 otherwise anarudisha kadi ya Chama
Unaonekana wa juzi,1995 alishinda kikwete dhidi ya Mkapa pale Dom.Mwal akaforce kurudisha kadi mgombea akiwa Kikwete
 
Kipindi nakaa monduli miaka ya 2010 to 2012 alikuwa anatupa mahindi Bure Kila nyumba
 
Nakumbuka aliwahi kusema haya yafuatayo:-

1. Kabla hajafa lazima awe Rais wa nchi hii

2. Aliahidi kutuletea mvua ya kutengeneza toka Thailand baada ya kufanya ziara huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…