Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,355
- 14,408
Yaani leo amefariki ndio mnasema yote haya,Kwanini hamkusema alipokuwa bado hai?.Anyway sawa.Lowasa alikuwa ni kati ya viongozi waliopata bahati ya kuzaliwa kizazi ambacho wale wachache walioweza kupata elimu kipindi hicho na kuichagua siasa kama sehemu yao ya maisha, wana maisha mazuri sana.
Kwenye siasa kuna kuanguka, kuna kusalitiana kwenye makubaliano, kuna kuogopana katika upana wa maendeleo binafsi, ambapo nashuhudia viongozi wengi wana muelezea Lowasa alivyoanguka kwenye mbio za urais 2015, alivyojiuzulu Uwaziri Mkuu, kama anguko la kisiasa la asha.....matukio hayo mawili ni matukio makubwa katika siasa za Afrika ambapo ni mfano wa kuigwa......bara letu la Afrika kwa ubinafsi na uroho wa viongozi wafia tumbo ni ngumu kiongozi mwenye madaraka ya Uwaziri Mkuu kuandika barua kwa Rais kuomba kujiuzulu ni ishara ya uwajibikaji hili, Mh. Lowasa katufundisha kwa vitendo, inaweza isitokee, lakini kubaki tu kwenye kumbukumbu tu, inatosha.
Misingi ya kusalitiana kwenye makubaliano ya kisiasa, naamini uwoga wa baadhi ya wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi kwenye dhana ile ile ya uwajibikaji, ule ushujaa uliogopesha wengi kwasababu wanasiasa wengi wanaogopa kuwajibika, lakini namshukuru Mwenyezi Mungu, kwenye ule msemo mchagua nazi sana mwishowe anachagua koroma ndivyo ilivyotokea alikatwa Mh. Lowasa akaingia Chuma (R.I.P) Dk. magufuli, moto uliwaka na kikubwa ambacho nakumbuka ajenda ya Lowasa ya Elimu bure, Chuma aliiendeleza, Rais wetu Mama wa Taifa naye anaiendeleza hii ni heshima ya kipekee sana, ingawa hawakumoa Urais kwasababu ya uwoga wa baadhi ya watu.
Mimi binafsi nakushukuru sana uliingia mgogoro na serikali ya Misri kwasababu ya watanzania wao wakitetea mto Nile, na wewe ukitetea ziwa Victoria watanzania wafaidike na maji hayo.....leo hii sio kama kipindi chetu darasa moja la watoto 100 wanachaguliwa 3 kuendelea na masomo ya sekondari, siku hizi darasa zima linaendelea adui ujinga anakaribia kwisha ndani ya nchi hii, naamini tuliokuwepo tupambane kwenye kubadili mitaala ya elimu ili iwe msaada kwa watoto....Mh. Lowasa kaacha alama yake.....tuliobaki tuache ya kwetu.
Pumzika kwa Amani Baba yetu......ni kweli bendera zinapaswa kupepea nusu mlingoti, Taifa Lunakulilia..[emoji24][emoji24][emoji24]
Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app