Ndio,hakuna namna nyingine.
Ukijifanya kumshauri vinginevyo atajiona kuwa wa kumjali mpo.
Mdogo wangu mtoto wa mama yangu mkubwa ni mlevi,sasa siku moja nimeenda likizo akawekewa kikao,ndugu zake wote wapo nami mgeni msikilizaji.
Ilipofika zamu yangu kutoa ushauri mimi nikaanza na maswali kwa yule jamaa yangu.
1; Kati yetu hapa kuna ambaye alisha kununulia pombe? Akajibu hapana.
2; Kati yetu hapa kuna ambaye aliwahi kukupatia fedha kwa ajili ya mambo mengine badala yake wewe ukanywea pombe? Akajibu hapana.
Hili la mwisho nikalielekeza kwa ndugu zetu.
3; Kati yetu ni nani amewahi kumnunulia pombe huyu jamaa au kumpatia fedha kwa ajili ya mambo mengine badala yake jamaa akanunulia pombe?
Hakuna aliyejitokeza.
Hitimisho langu liliibua ungomvi baina yangu na huyu dogo huku ndugu wengine wakiangua vicheko
Nilimuambia hivi;
WEWE KUNYWA POMBE,JIMWAGIE MPAKA WATENGENEZAJI WACHOKE.
KWANZA SAMAHANI KWA KUKUCHELEWESHA,WEWE NENDA HARAKA UKANYWE POMBEEEEE.
Jamaa aliniambia kuwa "kati ya watu niliokuwa ninawaona wana akili na wananipenda ni wewe,ila kwa ushauri huu HUNIPENDI HATA KIDOGO.
Ukweli ni kuwa alipunguza saaana na huwa simpatii hata ndala zilizo katika.