Utamu wa pesa, kwako ni upi?

Umenikumbusha Ile stori ya kweli kabisa ya Masai aliyechimbia Mamilioni pale Kwa mworomboo Chuga halafu akayasahau,Hadi waliokuwa wanachimba Barbara walivyozikuta huku nusu zikiwa zimeliwa na mchwa.Watu wengi hawajui Bata au Bata haliwajui.
Wengi huwa tunafikiria kesho, bila kujua na leo pia ni siku tunatakiwa kuiishi.
 
Kuvaa vizuri kukoje, kula vizuri kukoje, pisi kali zikoje? Hayo yote uliyoorodhesha ni definition ya mtu. Pisi kali kwako kwa mwingine mbovu.
Mkuu kwa mantiki hiyo hata hela yangu nikiiona ndogo kuna mwingine anaiona kubwa. Kila mtu anamahitaji yake kulingana na nafsi yake. Kuna mtu ataenda Zanzibar au Manyara na kuna mtu ataenda Santorini, Mykonos na Bali hao wote wametimiza yale mahitaji yao kulingana na vile nafsi yao inavyotaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…