Utamu wa vyombo vya Dola kuonjeshwa ladha ya madaraka matamu ya kisiasa

Poa 2

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Posts
1,317
Reaction score
1,320
Wadau nawasalimu wote Kila mmoja kwa imani na itikadi yake.
Baada ya salamu napenda kujikita katika kufafanua mada Kama kichwa Cha uzi kinavyojieleza.

Wote Ni mashahidi katika awamu ya tano tuliona jinsi vyombo vya Dola hasa tiss na polisi vilivyotumika kumlinda RAISI magufuli hasa chama Cha ccm ili kibaki madarakani kwa nguvu kubwa mno.

Tulishuhudia wakuu wa mikoa na wilaya wengi wakiteuliwa kutokea upande huo yaani teeth, na wanajeshi Jambo hili si baya ila nia na malengo ya Mamlaka pengine ndiyo iliyoleta maswali mengi.

Tulishuhudia wanajeshi wakisombeshwa korosho kusini na matokeo yake tumeyaona wote, tulishuhudia jinsi ccm ikiongozwa na katibu mkuu wa kipindi hicho bwana BASHIRU alivyovitumia vyombo hivyo vya Dola hasa polisi na teeth kujibakisha madarakani na mengine Kama hayo.

Ni ukweli kwamba kiongozi au Chama chochote Cha siasa kinapokosa uhalali na ushawishi kwa wananchi hujigeuza chama Dola ili angalau kisalie kwa kitambo kidogo TU
Ni ukweli kwamba ccm kwa Sasa Ni chama Dola na raisi yeyote atakayekuwa Ni kivuli TU. Chama na viongozi wake hufikiri kwamba kujiunganisha na Dola ndio salama yao kumbe hali hii huwa tofauti kabisa, historia inayoonyesha hivyo.

Ni ukweli kwamba viongozi wengi wa kuchaguliwa wanatambua wapo Hapo si kwa jeuri,uwezo, ushawishi,uhalali au nguvu zao Basi Ni vyombo vya Dola hasa polisi na hayati magufuli.

Ni ukweli kwamba viongozi wakuu vya Hivi vyombo vya Dola, serikali, ccm na wanaccm wenye kutafakari wanatambua kwamba ccm haikubaliki Tena na HAKUNA njia mbadala zaidi ya kutumia Dola
Ni ukweli kwa jeshi la polisi linatambua viongozi wengi hasa wabunge na madawani wapo kwenye nafasi hizo si kwa jasho lao Bali kwa jasho la jeshi la polisi na polisi mmoja mmoja, na hii ndio point mbaya kuliko zote kwani ukitazama mwenendo wa jeshi la polisi kwa Sasa Ni Kama umejaa kiburi jeuri na ukatili kwani wanajua viongozi wengi wapo pale kwa jasho lao polisi.

Ni ukweli kwamba huu muungano wa jeshi la polisi na ccm unakwenda kuzaa kitu kipya kwa nchi yetu Tanzania, utamu na tamaa ya madaraka inazidi kujengeka ndani ya dhamiri zao na matokeo ya tamaa hiyo wote hatukuwa salama.
Ni ukweli kwamba unapokaribia mwisho wa chama siasa hujigeuza dola na hatimaye hujigeuza watesaji kwa raia wote si upinzani TU na mwisho Hujigeuza magaidi wa kidola na mwisho kabisa makamanda wetu wananchi (JWTZ) huchukua dola kwa mda ili kuandaa mazingira ya Taifa jipya ( naona hivyo😁😁)

NA UKWELI NI KWAMBA WOTE WANAOZUIA KATIBA MPYA KWA VIJISABABU VYA AJABU NDIO WENYE UCHU WA MADARAKA, MAADUI WA TAIFA LETU NA NDIO MAGAIDI, HAWALITAKII MEMA TAIFA N.K pointi Kila mwananchi asomaye na aelewe.

Na Ni ukweli kwamba matokeo ya chama kujiungamanisha na Dolana kuwaacha wananchi upande wa pili huwa ni mapinduzi ya kijeshi au Vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Watanzania na viongozi wenye hekima wa Taifa letu pendwa tunakoipeleka tz wote tutaumia, vyama vingi tulikubali wenyewe na Kama tumeshindwa mbona mna Mamlaka kwani Nini msivifute? Kuliko kufungana, kuuana,kutesana na kumbakiana kesi, kumbukeni chama tawala vyama Hivi vimezalisha ajira nyingi Sana kwa watanzania yaani Ni sifa kwa chama Cha ccm kutengeneza hizo ajira mnataka kuvivuruga ili hata hizo ajira zipotee? Kwa wimbi la vijana wengi wasio na ajira Ni hatari kwa usalama wa Taifa.
Pole Sana mh. Rais mama yetu Samia suluhu ninajua kwa huu muungano wa chama chako na dola kunakupa wakati mgumu Sana kutimiza malengo yako najua unajua kula na vipofu bila kuwashika mikono
Nb: CHAMA+ DOLA= MAPINDUZI note that.
 
Kuna mazwazwa hawatakuelewa lakini umeongea jambo lenye uhalisia sana, kuna watu wanafikiri kujifungamanisha na viongozi wa kijeshi ndo watakaa salama, majeshi yafanye kazi zake kwa mujibu wa sheria na viongozi wa kiraia watimize majukumu yao kwa wananchi, bila kutegemea mbeleko ya chuma ya vyombo vya dola.
 
Viongozi dhaifu na waoga hufikiri hivyo lakini mwisho wake huanzia Hapo Hapo alipo
 
Tiba inakuja hiyo ndoa yao itavunjika
Hata hivyo vyombo vya dola vinaongozwa na binadamu Tena wenye ndugu haitodumu milele tabia ya kuwaumiza ndugu au jamii au kabila au dini za maaskari polisi, wanajeshi na tiss kwa sababu za kisiasa za kiongozi mmoja mwenye uchu wa madaraka kitaumana TU Kama kwa konde
 
Hivi watanzania walioona adha ya kukosekana kwa nishati ya uhakika ya umeme awamu ya 3 na ya 4 na jinsi maisha yao na future zao zilivyoparanganyika kwa ajili hiyo. Leo hii wanapona kuna kila dalili za kurudishwa kulekule unafikiri watafurahia? Hata kama hawana la kufanya lakini nyoyo zao zitakuwa hazina amani na watalia kimoyo moyo na machozi yao hayakuwa bure.

Ukishaona kunatokea kamanda wa cheo cha juu wa polisi anawachana viongozi wa kisiasa kwamba ifike mahali sasa wanasiasa wachaguliwe kwa sifa stahiki si vigezo vya Mzee au mjomba maarufu. Ukae ukijua kwa uhakika humo majeshini wako walio kinaishwa na matendo ya baadhi ya wanasiasa ambao ndio viongozi wetu.
 
Wadau nawasalimu wote Kila mmoja kwa imani na itikadi yake.
Baada ya salamu napenda kujikita katika kufafanua mada Kama kichwa Cha uzi kinavyojieleza.

Wote Ni mashahidi katika awamu ya tano tuliona jinsi vyombo vya Dola hasa tiss na polisi vilivyotumika kumlinda RAISI magufuli hasa chama Cha ccm ili kibaki madarakani kwa nguvu kubwa mno.

Tulishuhudia wakuu wa mikoa na wilaya wengi wakiteuliwa kutokea upande huo yaani teeth, na wanajeshi Jambo hili si baya ila nia na malengo ya Mamlaka pengine ndiyo iliyoleta maswali mengi.

Tulishuhudia wanajeshi wakisombeshwa korosho kusini na matokeo yake tumeyaona wote, tulishuhudia jinsi ccm ikiongozwa na katibu mkuu wa kipindi hicho bwana BASHIRU alivyovitumia vyombo hivyo vya Dola hasa polisi na teeth kujibakisha madarakani na mengine Kama hayo.

Ni ukweli kwamba kiongozi au Chama chochote Cha siasa kinapokosa uhalali na ushawishi kwa wananchi hujigeuza chama Dola ili angalau kisalie kwa kitambo kidogo TU
Ni ukweli kwamba ccm kwa Sasa Ni chama Dola na raisi yeyote atakayekuwa Ni kivuli TU. Chama na viongozi wake hufikiri kwamba kujiunganisha na Dola ndio salama yao kumbe hali hii huwa tofauti kabisa, historia inayoonyesha hivyo.

Ni ukweli kwamba viongozi wengi wa kuchaguliwa wanatambua wapo Hapo si kwa jeuri,uwezo, ushawishi,uhalali au nguvu zao Basi Ni vyombo vya Dola hasa polisi na hayati magufuli.

Ni ukweli kwamba viongozi wakuu vya Hivi vyombo vya Dola, serikali, ccm na wanaccm wenye kutafakari wanatambua kwamba ccm haikubaliki Tena na HAKUNA njia mbadala zaidi ya kutumia Dola
Ni ukweli kwa jeshi la polisi linatambua viongozi wengi hasa wabunge na madawani wapo kwenye nafasi hizo si kwa jasho lao Bali kwa jasho la jeshi la polisi na polisi mmoja mmoja, na hii ndio point mbaya kuliko zote kwani ukitazama mwenendo wa jeshi la polisi kwa Sasa Ni Kama umejaa kiburi jeuri na ukatili kwani wanajua viongozi wengi wapo pale kwa jasho lao polisi.

Ni ukweli kwamba huu muungano wa jeshi la polisi na ccm unakwenda kuzaa kitu kipya kwa nchi yetu Tanzania, utamu na tamaa ya madaraka inazidi kujengeka ndani ya dhamiri zao na matokeo ya tamaa hiyo wote hatukuwa salama.
Ni ukweli kwamba unapokaribia mwisho wa chama siasa hujigeuza dola na hatimaye hujigeuza watesaji kwa raia wote si upinzani TU na mwisho Hujigeuza magaidi wa kidola na mwisho kabisa makamanda wetu wananchi (JWTZ) huchukua dola kwa mda ili kuandaa mazingira ya Taifa jipya ( naona hivyo😁😁)

NA UKWELI NI KWAMBA WOTE WANAOZUIA KATIBA MPYA KWA VIJISABABU VYA AJABU NDIO WENYE UCHU WA MADARAKA, MAADUI WA TAIFA LETU NA NDIO MAGAIDI, HAWALITAKII MEMA TAIFA N.K pointi Kila mwananchi asomaye na aelewe.

Na Ni ukweli kwamba matokeo ya chama kujiungamanisha na Dolana kuwaacha wananchi upande wa pili huwa ni mapinduzi ya kijeshi au Vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Watanzania na viongozi wenye hekima wa Taifa letu pendwa tunakoipeleka tz wote tutaumia, vyama vingi tulikubali wenyewe na Kama tumeshindwa mbona mna Mamlaka kwani Nini msivifute? Kuliko kufungana, kuuana,kutesana na kumbakiana kesi, kumbukeni chama tawala vyama Hivi vimezalisha ajira nyingi Sana kwa watanzania yaani Ni sifa kwa chama Cha ccm kutengeneza hizo ajira mnataka kuvivuruga ili hata hizo ajira zipotee? Kwa wimbi la vijana wengi wasio na ajira Ni hatari kwa usalama wa Taifa.
Pole Sana mh. Rais mama yetu Samia suluhu ninajua kwa huu muungano wa chama chako na dola kunakupa wakati mgumu Sana kutimiza malengo yako najua unajua kula na vipofu bila kuwashika mikono
Nb: CHAMA+ DOLA= MAPINDUZI note that.
Watavuna walichopanda soon
 
Back
Top Bottom