Utani wa watu ninaoupenda hapa JF pamoja na watu na mada utakazowakuta

Utani wa watu ninaoupenda hapa JF pamoja na watu na mada utakazowakuta

kaka Lucas Mwashambwa ephen_ nimeona anaanza kutumiwa vimemo vya kingereza. Unalizungumziaje hili?
Uje dasalama nikupeleke kwao chanika tukaongee na mama yake.
Achana na yule chizi anaandika viingereza vya kukopi utafikiri anamuandikia Barua Rihanna au Beyonce. Mimi naongea lugha na maneno yanayotoka moyoni na siyo yule chizi anakopi utafikiri imla.

Ukichanja Damu yangu unakuta imejaa Upendo na mawazo mazuri kwa ephen.
 
Achana na yule chizi anaandika viingereza vya kukopi utafikiri anamuandikia Barua Rihanna au Beyonce. Mimi naongea lugha na maneno yanayotoka moyoni na siyo yule chizi anakopi utafikiri imla.

Ukichanja Damu yangu unakuta imejaa Upendo na mawazo mazuri kwa ephen.
tutamshonea dela la CHADEMA😂😂😂😂
 
Mkuu,

Kuna watu walijitolea kupigania uhuru wa Afrika, wengine wamejitolea kupigania usawa wa watu, na kadhalika.

Mimi, kwa kadiri ya uwezo wangu, pale ambapo naona kunaweza kuwa na deserving case, najitolea kuweka mambo sawa na kunyoosha dhana kuhusu uwepo wa Mungu. Hususan hapa JF.

Hizi habari nyingi kwa wasomaji wa Kiingereza si kitu cha ajabu. You can pick up Bertrand Russell or Richard Dawkins and get most of my points, even more, in a week or two.

Tatizo jamii yetu kwa kiasi kikubwa haisomi, na zaidi, Kiingereza ni mzigo wa misumari unaotutesa sana. Na hata kwa wanaoelewa Kiingereza, logical and critical thinking ni janga la kitaifa.

Nilivyoanza, nilionekana mtu wa ajabu sana, almost kichaa. Lakini polepole, naona siku hizi, hizi dhana za kupinga uwepo wa Mungu, kifalsafa, kimantiki, zinaeleweka sana. Kuna watu wengi wanaelewa, ama wamejifunza na kukubali mantiki ya dhana ya kutokuwepo Mungu, ama walikuwa wanaijua mantiki hii tangu awali na wamepata urahisi wa kuungana na watu wanaoonekana kuhoji uwepo wa Mungu.

Siko mpweke kama awali tena, na kadiri siku zinavyoenda, watu wanavyozidi kupanuka mawazo, kusoma, kusafiri, kueleea mambo zaidi, tutaelewana tu.

Ingawa imani potofu huwa zina tabia ya kung'ang'ania sana kwenye vichwa vya watu hata kwa "cognitive dissonance" tu, mapambano yanaendelea, mafanikio makubwa katika kuupiga vita upotofu huu wa imani ya Mungu yapo mbele yetu.

Asante sana kwa tag.
Mwenyezi Mungu akuongoze katika njia sahihi.
 
wakuu Mambo ni vipi.

Mimi huwa napenda sana kusoma mada mbali mbali hapa Jf
Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu, Leo nitazungumizia utani wa watu hapa Jf na watu na mada ambazo utawakuta.

1 . Ni Accumen Mo na mgalatia Maghayo
Hawa ndugu zangu mimi huwa wananifurahisha sana. Nitakapoona komenti ya maghayo basi najua Accumen Mo lazima aweke wino wake hapo na lazima iwe ni kituko. Mwanzoni mgalatia huyu alikuwa ana battle sana na adriz nikaona utani umepungua umeamia kwa accumen mo. Sijui nyinyi mnauchukuliaje utani wenu ila kwangu ni burudani

2. Lucas Mwashambwa
CHIEF PRIEST
Tindo
Ma mmoja anaitwa Benjamin netanyhau

Sijui wao huenda wakawa wanaongea kwa kuchagua pande zao za siasa ila mimi kwangu huwa ni burudani. Hasa Kaka Lucas akiwa anamjibu Benjamin netanyhau huwa anamwambia hivi “ Punguza mibange unayovutia chooni “🤣🤣 binafsi kwangu ni burudani . Tindo na Lucas na ndugu chief priest hazijawahi kuiva ni paka na panya. Hili battle huwa ninalipenda.
Lakini kaka Lucas katokea kumuelewa Sana dada @ephen hata ukiangalia charts zao unaona kuna flow nzuri kabisa baina yao.

Kuna mtu mmoja sijui yeye kama yupo serious ila kwangu huwaga ni kucheka Etwege huyu jamaa yeye hata kama mada inahusu mboga za majani lazima neno Tundu Lissu liingie hapo na lazima atafute koneksheni ya mboga na Tundu lissu. Kwangu mm huwa ni kucheka tu na furaha tele. Nakukubali sana ndugu.

Ukitaka Infropreneur uone komenti yake wewe anzisha mada ya kusema Mungu yupo, kama si komenti ya kwanza mpaka ya tano tangu mada ianzishwe labda hayupo online😂😂 huwa nafurahi sana.

Ukitaka kuona uzi wa mpira unanoga wawepo Hawa watu sana sana kuhus SIMBA VS YANGA

Okwa BOBAN SUNZU mhasibu
Labani og
NALIA NGWENA
Scars
Hapo kuna wananchi na kuna simba watoto wa kariakoo, Mimi huwa majadiliano yao yananifurahisha sana. Ninawakubali sana.

Ngoja niishie hapa next time nitakuja na kitu kinachonifanya Niipende zaidi Jf .

Weka watu unaopenda aidha utani wao au chemistry waliyonayo.
Ehee! Sasa sijui ndiyo nimeandika nini!
 
😂😂😂😂huwa anafurahisha sana.
cocastic yeye huwa ni mtu ambaye hajali ukisema vyovyote vile yeye hajali.

Ukimchunguza zaidi pia mbali na masuala ya upinde utamkuta unapotaka kuisema simba😂😂

Kuna mdada anaitwa @Lamony yeue katika komenti zake tatu mbili lazima ziwe na emoji ya kucheka.

Kuna mdada anaitwa Aaliyyah yeue ukitaka kupata komenti yake ni mada za chakula, lazima utakumbana na komenti yake
😂😂😂Huu mwili ni WA muda mfupi mbinguni tutapewa mwingine mpya hebu tuwe tunakula vizuri ndugu zangu kwenda na mwili mzuri mbinguni hakuna maana 😀😀😀
 
The Stress Challenger nina wasiwasi wana undugu na Maghayo
Niliwahi kuleta Uzi Wenye ushahidi wa wazi unaofichua kuwa Maghayo ndio The Stress Challengerr mods wakapita nao .

Kuna siku nyingine sijui alivuta bange Kali ,mwamba alojichanganya ndani ya dakika mbili alipost Uzi mmoja ukiwa na heading , content mpaka maneno ya ndani ya Uzi sawa katika ID mbili za The Stress Challengerr na ya Maghayo , mimi nikamkumbusha na kumuwekea screenshot kuwa huo Uzi ushapost kwa ID ya The Stress Challengerr akastuka na kudai eti The Stress Challengerr anazingua...
 
Back
Top Bottom