Utani wa watu ninaoupenda hapa JF pamoja na watu na mada utakazowakuta

Utani wa watu ninaoupenda hapa JF pamoja na watu na mada utakazowakuta

Ukitaka Kiranga uone komenti yake wewe anzisha mada ya kusema Mungu yupo, kama si komenti ya kwanza mpaka ya tano tangu mada ianzishwe labda hayupo online😂😂 huwa nafurahi sana.
Mkuu,

Kuna watu walijitolea kupigania uhuru wa Afrika, wengine wamejitolea kupigania usawa wa watu, na kadhalika.

Mimi, kwa kadiri ya uwezo wangu, pale ambapo naona kunaweza kuwa na deserving case, najitolea kuweka mambo sawa na kunyoosha dhana kuhusu uwepo wa Mungu. Hususan hapa JF.

Hizi habari nyingi kwa wasomaji wa Kiingereza si kitu cha ajabu. You can pick up Bertrand Russell or Richard Dawkins and get most of my points, even more, in a week or two.

Tatizo jamii yetu kwa kiasi kikubwa haisomi, na zaidi, Kiingereza ni mzigo wa misumari unaotutesa sana. Na hata kwa wanaoelewa Kiingereza, logical and critical thinking ni janga la kitaifa.

Nilivyoanza, nilionekana mtu wa ajabu sana, almost kichaa. Lakini polepole, naona siku hizi, hizi dhana za kupinga uwepo wa Mungu, kifalsafa, kimantiki, zinaeleweka sana. Kuna watu wengi wanaelewa, ama wamejifunza na kukubali mantiki ya dhana ya kutokuwepo Mungu, ama walikuwa wanaijua mantiki hii tangu awali na wamepata urahisi wa kuungana na watu wanaoonekana kuhoji uwepo wa Mungu.

Siko mpweke kama awali tena, na kadiri siku zinavyoenda, watu wanavyozidi kupanuka mawazo, kusoma, kusafiri, kueleea mambo zaidi, tutaelewana tu.

Ingawa imani potofu huwa zina tabia ya kung'ang'ania sana kwenye vichwa vya watu hata kwa "cognitive dissonance" tu, mapambano yanaendelea, mafanikio makubwa katika kuupiga vita upotofu huu wa imani ya Mungu yapo mbele yetu.

Asante sana kwa tag.
 
Ukitaka Nyafwili uone komenti yake wewe anzisha mada ya TBC , kama si komenti ya kwanza mpaka ya tano tangu mada ianzishwe labda hayupo online😂😂 huwa nafurahi sana.
Nyafwili huwa pia unamkuta kwenye mada za dini😂😂😂 simuelewagi yupo opposer au proposer
Ila kuna jamaa yeye mkimya sana ukitaka kumuona anzisha mada ya kupinga ndoa hua anajiita someone passion_amo1 😂😂😂. Pia utamkuta kwenye mada za kupinga dini lakin kwenye mada za biashara.

Kuna mtu anaitwa Greatest Of All Time huyu ukimuongelea messi vbaya lazima uzi uchafuke😂😂🤣🤣
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mimi sijui watu huwa wanachukuliaje lakini yote kwa yote Lucas ana roho ngumu sana. Wengi hawapendi maandishi yake lakini akianzisha nyuzi yake watu wanajazana .
Huwa ninafurahi sana akianza kujibu watu.
Kaka Lucas Mwashambwa huwa anapokea sapoti kutoka kwa MamaSamia2025 Tlaatlaah Etwege [emoji23][emoji23]hilo ni chama lake.
Ila kuna upinzani akishafika Bams Rabbon Erythrocyte hapo mada lazima ichangamke[emoji23][emoji23][emoji23] aisee hawa watu ni burudani sana hapa JF.
Watu wanaongea vyenye masirahi kitaifa.
Wewe unachekacheka eti burudani.

Hili Taifa liko doomed.
 
Ukitaka cocastic uone komenti yake wewe anzisha mada ya kuwasema 🌈🌈, kama si komenti ya kwanza mpaka ya tano tangu mada ianzishwe labda hayupo online😂😂 huwa nafurahi sana.
😂😂😂😂huwa anafurahisha sana.
cocastic yeye huwa ni mtu ambaye hajali ukisema vyovyote vile yeye hajali.

Ukimchunguza zaidi pia mbali na masuala ya upinde utamkuta unapotaka kuisema simba😂😂

Kuna mdada anaitwa @Lamony yeue katika komenti zake tatu mbili lazima ziwe na emoji ya kucheka.

Kuna mdada anaitwa Aaliyyah yeue ukitaka kupata komenti yake ni mada za chakula, lazima utakumbana na komenti yake
 
Ukitaka Nyafwili uone komenti yake wewe anzisha mada ya TBC , kama si komenti ya kwanza mpaka ya tano tangu mada ianzishwe labda hayupo online😂😂 huwa nafurahi sana.
Kwa kweli TBC wanisamehe tu, Nilijitahidi kuwafuatilia, nikanunua na TV kubwa nikadhani labda muonekano wa picha ni mdogo kwenye screen lakini nilishindwa... 😀😀
 
😂😂😂😂😂😂sema basi tu. Ephen na Lucas wanapendana sana. Ila Lucas ninahisi yupo anakimbila 45+ ila ephen akizidi sana ni 25 hata yeye hawez bisha

Mnyiha Lucas Mwashambwa ni kijana mdogo tu hata 35 hajafika, ila kwa namna watani zangu hawa walivyo wabishi unaweza ukadhani ana miaka ya kukaribia kuchukua pensheni yake...

Hapo kwa ephen hebu tupause kwanza...
 
wakuu Mambo ni vipi.

Mimi huwa napenda sana kusoma mada mbali mbali hapa Jf
Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu, Leo nitazungumizia utani wa watu hapa Jf na watu na mada ambazo utawakuta.

1 . Ni Accumen Mo na mgalatia Maghayo
Hawa ndugu zangu mimi huwa wananifurahisha sana. Nitakapoona komenti ya maghayo basi najua Accumen Mo lazima aweke wino wake hapo na lazima iwe ni kituko. Mwanzoni mgalatia huyu alikuwa ana battle sana na adriz nikaona utani umepungua umeamia kwa accumen mo. Sijui nyinyi mnauchukuliaje utani wenu ila kwangu ni burudani

2. Lucas Mwashambwa
CHIEF PRIEST
Tindo
Ma mmoja anaitwa Benjamin netanyhau

Sijui wao huenda wakawa wanaongea kwa kuchagua pande zao za siasa ila mimi kwangu huwa ni burudani. Hasa Kaka Lucas akiwa anamjibu Benjamin netanyhau huwa anamwambia hivi “ Punguza mibange unayovutia chooni “🤣🤣 binafsi kwangu ni burudani . Tindo na Lucas na ndugu chief priest hazijawahi kuiva ni paka na panya. Hili battle huwa ninalipenda.
Lakini kaka Lucas katokea kumuelewa Sana dada @ephen hata ukiangalia charts zao unaona kuna flow nzuri kabisa baina yao.

Kuna mtu mmoja sijui yeye kama yupo serious ila kwangu huwaga ni kucheka Etwege huyu jamaa yeye hata kama mada inahusu mboga za majani lazima neno Tundu Lissu liingie hapo na lazima atafute koneksheni ya mboga na Tundu lissu. Kwangu mm huwa ni kucheka tu na furaha tele. Nakukubali sana ndugu.

Ukitaka Infropreneur uone komenti yake wewe anzisha mada ya kusema Mungu yupo, kama si komenti ya kwanza mpaka ya tano tangu mada ianzishwe labda hayupo online😂😂 huwa nafurahi sana.

Ukitaka kuona uzi wa mpira unanoga wawepo Hawa watu sana sana kuhus SIMBA VS YANGA

Okwa BOBAN SUNZU mhasibu
Labani og
NALIA NGWENA
Scars
Hapo kuna wananchi na kuna simba watoto wa kariakoo, Mimi huwa majadiliano yao yananifurahisha sana. Ninawakubali sana.

Ngoja niishie hapa next time nitakuja na kitu kinachonifanya Niipende zaidi Jf .

Weka watu unaopenda aidha utani wao au chemistry waliyonayo.
Kwenye mada za mpira bila kumtaja popoma Jenta huu uzi ni takataka japo kuwa ni maono yako.
 
Mnyiha Lucas Mwashambwa ni kijana mdogo tu hata 35 hajafika, ila kwa namna watani zangu hawa walivyo wabishi unaweza ukadhani ana miaka ya kukaribia kuchua pensheni yake...

Hapo kwa ephen hebu tupause kwanza...
🤣🤣🤣🤣 ila ephen ana 23 kama unadai lucas hajafika 35 ina maana yupo 28-31 si mbaya ngo’mbe hazeeki maini😂😂
 
Back
Top Bottom