DOKEZO Utapeli biashara mtandaoni: Shuhuda za watu waliowahi kupigwa na kujuta sana

DOKEZO Utapeli biashara mtandaoni: Shuhuda za watu waliowahi kupigwa na kujuta sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Mimi ni mmojawapo😂

Na nadhani nilipigwa kama mara tatu hivi kabla sijajifunza na kuelimika

Miaka ile ya 2010 nikaagiza kupitia Ebay radio touch screen.. Wakati huo bongo ilikuwa ni kuanzia lako 5 kwenda juu.. Mimi nikaipata kwa elfu 50 tuu free delivery😂

Baada ya miezi miwili kupiga bila mzigo kupata nika file complaint! Nikajibiwa kwa ushahidi kwamba nilitumiwa kwenye email😂 kumbe ilikuwa programme ya radio ya touch na sio radio yenyewe..


Nikachoka kabisa
Nikajaribu tena safari nyingine kununua kisu na teaser .! Kisu hakikuzidi urefu wa kidole kidogo! Teaser ilikuwa ni kiplastic kidogo Mfano wa teaser ambacho hata ukiambiwa utoe jero hununui.. Huo ukawa mwisho wanga kafanya biashara na Ebay

Watu wengi sana wamepigwa kwenye hizi biashara..ni wazi hata hapa wapo! Unachokiona kwenye picha na kuagiza sicho unacholetewa!

Unakuja kupata asili ukishaelimika kwamba
1. Zingatia sana vipimo vya bidhaa unayotaka kununua
2. Zingatia sana bei.. Kitu cha bei unayojua ni ya kawaida kukipata kwa roho ya bei unaweza ukawa hujapata bali umepatikana😂
3. Vitu vya bei rahisi sana sana na free delivery pia makinika navyo
Zifuatazo ni picha mbalimbali za watu waliowahi kupigwa kwenye hii online shopping
FB_IMG_1735439174060.jpg
FB_IMG_1735439170363.jpg
 
Back
Top Bottom