Uchaguzi 2020 Utapeli: Mgombea Ubunge atia nia kugombea majimbo tofauti , ni Rorya na Tarime Mjini , kila jimbo na Chama chake

Uchaguzi 2020 Utapeli: Mgombea Ubunge atia nia kugombea majimbo tofauti , ni Rorya na Tarime Mjini , kila jimbo na Chama chake

Anaweza kuwa mwanachama wa vyama vyote kule alikotia nia. Hivi kuna sheria inayomzuia mtu kuwa mwanachama wa vyama zaidi ya kimoja? Tuanzie hapo. Ni muhimu kuanzia hapo kwa sababu huyu mtia nia ni mwanasheria labda amejihami kwenye eneo hilo!
[emoji1787][emoji1787] duuh hatari
 
Ana nia ya dhati ya kuwawakilisha wananchi wa pande zote, achaguliwe tu na pande zote akawawakilishe.
 
Ha haha! Kwa hiyo utetezi wa Kabudi ndio ukauamini? Ndio maana nawaambia CCM ni waongo by nature! Mie niliweka ushahidi, Kabudi aliweka bla bla ambazo hata Kenya waliishia kucheka tuu!
Lakini kwa vile yeye Waziri ukamuamini mie ukaona nadanganya.
Narudia kwa msisitizo, CCM ni waongo sana kuanzia mwenye kigoda hadi mtu wa chini.
BTW hivi issue ya #2 kuwekewa sumu na Mambosasa kumsaka muhusika duniani pote hadi chini ya bahari iliishia wapi?


Kuna nchi zilikuwepo kwenye ile list yako na sio member wa UN.Sasa zilipigaje kura? Kumbe wewe tatizo kubwa sio uwongo bali ni ignorance. Inaonekana ulitoka from nowhere ukazama kwenye siasa.Haya mambo yanahitaji elimu na uelewa mkubwa pia.Leta tena hako kalist uchwara nikuonyeshe Nchi ambazo sio member wa UN ili siku ukikutana na experts usiaibike.
Kuhusu hayo mambo mengine kawaulize CCM.
 
Ili ionekane ni ujanja ujanga naomba mleta mada anithibitishie haya

a) Huyu ni mtu mmoja na mwanachama wa vyama viwili vya siasa.
b) Hawa sio mapacha na jina “Dea” kwa Chadema halioneshi kuwa watu hawa ni mmoja.

Kufanana sura si uthibitisho watu hao wawili ni mtu mmoja.
 
Mimi ni mwanaccm toka 2010, nilivoona wapinzani wanabaguliwa nimeamua kukata kadi za chadema, cuf na act wazaendo.

Mojawapo ya chama hicho kitashika awamu ya saba au nane.... Lazima. Wakichunguza watakuta nina kadi yao kitambo hivo sitabaguliwa.


Baada ya watanzania m60 kuwa na mahaba ya ccm Mimi nimepunguza kimbelembele cha mahaba ya live kusikilizia upepo kwanza.
 
Sasa yeye ni mwanachama wa chama gani?
Tangu Ndugai ainajisi Katiba tulisema hili wenye nongwa waluozoea kunyonga wakatetea. Lakini madhara yake ndo haya. Mbunge wa CHADEMA mwanachama wa CCM,!!!
 
Hii wengi wameifanya mwaka huu. Sema tatizo la huyu bwana katia nia kwenye majimbo yaliyo karibiana Sana. Lkn kuna wajanja wawili nawafahsmu wamevuta fomu katika majimbo yaliopo kanda tofauti.
Uko sahihi mkuu, kuna mmoja kapiga Kyela na Sumbawanga mjini.
 
View attachment 1504183

Ikiwa kama nimemsingizia basi nisamehewe , bali rada za wapekuzi wetu waliotapakaa nchi nzima wanaoangalia kwa karibu sana uadilifu wa wagombea wamenasa mmoja wa watia nia akiendesha siasa za kishamba zisizoeleweka

Ingekuwa ni kwenye soka basi bila shaka TFF ingemfungia bila huruma , lakini huku kwingine sifahamu adhabu anayopaswa kuipata .
Duh kabeti timu zote mbili
 
Uko sahihi mkuu, kuna mmoja kapiga Kyela na Sumbawanga mjini.
Mmoja kavuta fomu Jimbo mojawapo ktk mkoa wa Pwani halafu kaenda kuvuta mkoa wa Katavi. Wenyewe wanasema rais anateua watia nia wa ccm ama wapinzani wenye mvuto. Ndiyo maana wanategesha majina yao pande zote
 
View attachment 1504183

Ikiwa kama nimemsingizia basi nisamehewe , bali rada za wapekuzi wetu waliotapakaa nchi nzima wanaoangalia kwa karibu sana uadilifu wa wagombea wamenasa mmoja wa watia nia akiendesha siasa za kishamba zisizoeleweka

Ingekuwa ni kwenye soka basi bila shaka TFF ingemfungia bila huruma , lakini huku kwingine sifahamu adhabu anayopaswa kuipata .
Nipatie majina yako na picha yako moja nikutengenezee bango kama hilo hapa hapa kwenye simu..
 
Back
Top Bottom