Uchaguzi 2020 Utapeli: Mgombea Ubunge atia nia kugombea majimbo tofauti , ni Rorya na Tarime Mjini , kila jimbo na Chama chake

Uchaguzi 2020 Utapeli: Mgombea Ubunge atia nia kugombea majimbo tofauti , ni Rorya na Tarime Mjini , kila jimbo na Chama chake

Tunampa poleeeee......
Moyo wake upo kwa maslahi ya wananchi ambako ni chadema lkn ana hofu ya udharimu wa ccm......

Mtaka yote kwa pupa atakosa yoteee..
 
Mwanaccm agombee Chadema? Hivi hujui kuwa mtu muongo asili yake ni CCM? Huko ndio kwenye asili ya uongo, sio Mwenyekiti, KM, Chakubanga, Mangula, wasanii hadi vuvuzela nyie wote waongo tuu!
Kwahiyo mchungaji Msigwa aliyekiri kuwa muongo na kumzushia Kinana naye ni wa CCM?
 
Katiba ya CCM inasema wazi mwanachama atakoma uanachama kwa "Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa". Katiba ya Chadema pia nayo inasema wazi "Asiwe mwanachama wa Chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na CHADEMA."
===
Ninadhani muhusika anajua maelezo ya katiba za vyama hivi, vinginevyo, mleta mada awe ameamua kumchafua.
 
Kwahiyo mchungaji Msigwa aliyekiri kuwa muongo na kumzushia Kinana naye ni wa CCM?
Umewahi kuwa na kesi ya madai mahakamani? Kama hujawahi huwezi kuelewa kwa nini Msigwa katamka yale maneno
 
Hiyo ni ishara kuonesha namna ambavyo siasa nchini kwetu zimefiliska kufikia kiwango hiki.

Style ya uongozi wa Magufuli imefuta ideological identity/positions za vyama vya siasa vyote na kubakiza party legal framework operations similar to an industrial line of product manufacturing.

Hata CCM hali iko hivyo ndio maana tunashuhudia wajasiria siasa wengi (kibao) wanaomba kugombea udiwani au ubunge kupitia chama hicho.

Pengine utakuwa ulimsikia Augustino Lyatonga Mrema jana ndani ya Mkutano Mkuu wa CCM akiomba chama chake kipewe wagombea ubunge/udiwani kutoka miongoni wa watakaokuwa hawakupitishwa na CCM.

Aidha, ukisikiliza nyimbo walizokuwa wakiimba wasanii kwenye mkutano mkuu wa CCM na kisha kushangiliwa na wajumbe hao pasipo nyimbo kuwa na ideological substance inaonesha kiwango kilichofikiwa cha ideological paucity ndani ya CCM.

Ukiona mwenyekiti na mgombea kiti cha urais wa chama anateuliwa, lakini badala ya hotuba yake ya kukubali uteuzi kusheheni mipango kiitikadi au tathmini ya utendaji miaka mitano iliyopita (hapa kikwete alipaweza sana), kwa mfano namna ambavyo chama kinaungwa mkono na wananchi (wanachama wapya), uwezo wa kubuni na kutekeleza miradi yake ya kisiasa, uwezo wa kuhamasisha na kutumia rasmilimali za chama, uwezo wa kuimarika kwa institutuinal machinery ya chama, uwezo wa chama (siyo serikali) kuchagiza (influence) public opinion, na kadhaika - mgombea pekee wa nafasi ya urais na mteule wa Chama Cha Mapinduzi ana-reduce mkutano mkuu wa chama chake kuwa tukio la kupiga kura za kumteua mgombea tu, na ndani ya masaa manne, badala ya kuendelea na ratiba ya siku mbili zilizopangwa, anakatiza na kutangaza kuisha kwa mkutano mkuu, ujue kuwa kwa sasa Tanzania inaelekea shimoni kisiasa, and the first victim is CCM!
Na nchi imepoteza mwelekeo inajiendea tu kama jongoo.

Ukifikiria bunge lilivyokuwa unapata mashaka sana juu ya kesho ya taifa hili.
 
Katiba ya CCM inasema wazi mwanachama atakoma uanachama kwa "Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa". Katiba ya Chadema pia nayo inasema wazi "Asiwe mwanachama wa Chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na CHADEMA."
===
Ninadhani muhusika anajua maelezo ya katiba za vyama hivi, vinginevyo, mleta mada awe ameamua kumchafua.
Simjui wala sina ugomvi naye wowote
 
Siasa za kuchafuana tu zimeanza mgombea mwenye nia hawezi Fanya huo upuuzi watu wanamtengenezea mazingira ya kutokuaminiwa
 
Back
Top Bottom