Utapeli miamala ya simu: Usikubali malipo kwa simu toka kwa usiyemjua

Nimepapitia pote mkuu pamoja na vikorombwezo vyake.

Ikumbukwe tunatofautiana kielimu, cognition power, instincts nk. Vyote vyote kwa pamoja vikikamilisha vinavyoitwa ubinadamu. Hatuwezi kuwa sawa.

Wajomba wa tuma kwa namba hii, na hii ya kuhamishiwa muamala baada ya huduma au manunuzi (ndani ya changamoto kadhaa) ni tofauti.

Angalia posts #86 na #89 kujiridhisha.

Jamaa yangu yalipompata ilikuwa yapata 22:00 baada ya kuwa wamemsingizia na tapeli mbobezi huyo kutafuta vibanda vya mpesa bila mafanikio ili atoe cash bila ya mafanikio.

Kuhamisha muamala kwa simu kiungwana ikawa ni compromise ukizingatia ustaarabu na kauli za mteja yule.

Ama kwa hakika umdhaniaye siye, ndiye.

Hivi sasa keshaumwa na nyoka. He learnt it the hard way.

Kwamba ma operator wanatoa elimu kwa SMS? Nikiri sijawahi kuona moja iliyo katika msingi wa mada hii.

Binafsi nikiri pia, haya hayajanikuta thanks ni kwa instincts tu na kwa hakika ashukuriwe bwana wa majeshi!

Nayasema haya tokea mjini, sembuse pande za dongo beshi, nanjilinji na mwalusembe huko?!

Ninakazia: Jamaa yangu katapeliwa kwa kutowajibika ipasavyo kwa wabeba dhamana. Kwao Tozo ni muhimu zaidi wala si usalama wetu.
 
Mie tukifanya malipo kwa simu baada ya kumaliza jmtu lazima niamishe salio hata kidogo kwenda mtandao mwingine au hata kununua LUKU.UKISHAUFANYIA MATUMIZI HATA YA ELF 1 HAWEZI TENA KUURUDISHA.
 
Mtoa mada pengine huelewi vizuri hizi mambo zinafanya vipi kazi.

Kutuma pesa kwenda kwa mtu mwingine kwa Mpesa na kulipa huduma kwa mpesa ni mambo mawili tofauti kabisa.

Ukituma pesa kwa mtu, unaweza kuomba pesa irudishwe bila hata mpokeaji kutoa ruhusa, maana mtumaji ndio mwenye hela.

Ukilipa huduma kwa Lipa namba au namba ya biashara, kabla pesa haijarudishwa; biashara iliyopokea lazima itoe ruhusa ili pesa irudishwe.

Makosa ya huyo jamaa kutojua tofauti ya hivi vitu viwili, visipeleke lawama kwa watu wa Mpesa; maana tayari wametengeneza mifumo inayofanya kazi. Labda elimu ndio muhimu ila mtu kurudisha pesa aliyotuma "kimakosa" sio utapeli.
 
Mie tukifanya malipo kwa simu baada ya kumaliza jmtu lazima niamishe salio hata kidogo kwenda mtandao mwingine au hata kununua LUKU.UKISHAUFANYIA MATUMIZI HATA YA ELF 1 HAWEZI TENA KUURUDISHA.

Hata miye nimekuwa nikihamisha kwenye line yangu nyingine - sheer instincts.

Ninakazia: Kwamba hayakunikuta, ashukuriwe bwana wa majeshi.
 
Umeandika haya:

"Mtoa mada pengine huelewi vizuri hizi mambo zinafanya vipi kazi."

Ni wazi kuwa ungekuwa mada umeielewa usingeandika pia haya:

"Labda elimu ndio muhimu .."

Kwamba:

"ila mtu kurudisha pesa aliyotuma "kimakosa" sio utapeli."

Karudisha pesa aliyotuma kimakosa au katapeli kuwa analipa kumbe - jongo?

Rejea kamusi ya kiswahili kuhusiana na neno utapeli.
 
Kwamba unaita uongo bila ya kuwa na ufahamu wowote wa kadhia hii?

Vodacom amekiri tatizo hili ni rampant?

No wonder kuna Tanzania ya viwanda ikijengwa katika awamu fulani.

Bure kabisa!
Naona umekariri sana neno rampant😅😅
 
Naona umekariri sana neno rampant😅😅
Unaona kwa macho matupu au umetupia na miwani ya mbao pia?

"Eti huyu naye ni mdau mahiri kwenye kudai katiba mpya iliyo muafaka zaidi. Tutasubiri miaka mingi sana."

Kwa hakika wewe ni mfano mzuri sana wa wale watanzania walio wajinga mno.

Hiiiiii bagosha - hii nayo nimekariri. Kwani unasemaje basi?
 
Labda nikuulize swali jepesi, huyo aliyepokea pesa alikuwa ni mtumiaji wa aina gani wa Mpesa

1. Mtumiaji wa kawaida
2. Namba ya biashara
3. Lipa namba
 
Mie tukifanya malipo kwa simu baada ya kumaliza jmtu lazima niamishe salio hata kidogo kwenda mtandao mwingine au hata kununua LUKU.UKISHAUFANYIA MATUMIZI HATA YA ELF 1 HAWEZI TENA KUURUDISHA.
Usipate shida ivo...ukiwa na lipa kwa simu ata joe biden hawezi rudisha muamala
 
huuu ni mtihani kwelii.. kuna jamaa yangu ana mitindo hiyooo sana.
 
Labda nikuulize swali jepesi, huyo aliyepokea pesa alikuwa ni mtumiaji wa aina gani wa Mpesa

1. Mtumiaji wa kawaida
2. Namba ya biashara
3. Lipa namba

Labda nikuulize wewe unaonaje? Nikuongeze na hili - unadhani elimu ya kutosha kuhusu haya imetolewa kwa wateja mijini hadi dongo beshi? Au wajisemea tu?

Au kwa vile haijakukuta wewe basi inatosha?
 
Labda nikuulize wewe unaonaje? Nikuongeze na hili - unadhani elimu ya kutosha kuhusu haya imetolewa kwa wateja mijini hadi dongo beshi? Au wajisemea tu?

Au kwa vile haijakukuta wewe basi inatosha?
Tatizo hauleweki, nimekuuliza simple question, account yake ni ya aina gani? Bila kujua hilo, tunapoteza muda hapa
 
Tatizo hauleweki, nimekuuliza simple question, account yake ni ya aina gani? Bila kujua hilo, tunapoteza muda hapa
Kumbe niliyokuuliza ni magumu? Ama kweli nyani kuona ku*dule hadi anunue kioo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…