Kuna utapeli wa aina nyingi sana kwenye miamala ya kifedha na mtandaoni, kila siku wezi wanabuni mbinu mpya.
Umakini unahitajika sana, hesabu pesa na kucheki balance kila unapofanya muamala wa kupokea kwani hata mawakala nao wanatapeli wateja, kutuliza akili ni jambo la muhimu sana.
Usikubali watu wakupanikishe, wakija wengi wawekee utaratibu kila mmoja umuhudumie akili ikiwa imetulia la sivyo unaweza kulia.