Utapeli unaendelea mafundi kuweni makini hii imetokea leo

Hawa matapeli nafurahigi sana wakinopigia maana me najua kucheza nao nawachora mbaka wanajua kabisa hapa tumepata wakupiga kumbe laa hasha nawapotezea tu mda mwishoe tunakuja kutukanana na hapo wapo hoi hasa Hawa wanaojidai ni wahudumu wavoda

Me ni Mzee wa kutumia Salio zao vyema
 

Matapeli sasa hivi wamewageukia mafundi kutaka kuwatapeli. Kosa wanalofanya ni kuomba fundi atume hela ili pikipiki ijazwe mafuta ije imchukue impeleke saiti hela atarudishiwa hukohuko saiti. Mbaya zaidi fundi na huyo tapeli hawajuani
Afu sauti ya kibaba kabisa.. Makamu ya miaka 50 Hiv Daah aisee
 
Aina hii ya wizi, bodaboda nao wamepigwa sana. Anabebeshwa vitu vya kununua kwenye maduka, halafu mwisho wa siku anaambiwa atume na hela! Na biashara inaishia hapo.
 
Manina washenzi wanaroho ngumu.
Mama lishe wa watu kashaua mtaji , na hii kitaji ya kuunga unga.
 
Kuna kipindi hata bodaboda walikuwa wanatapeliwa kwa mtindo huu:
Tapeli anampigia cm boda anamwambia samahan nimepewa namba yako naomba nikuagize vitu,maana hapa kwangu nina wageni siwezi kutoka.

Hapo tapeli atafanya kama anamuagiza labda mchele nyama na mazaga mengine.


Kabla boda hajapeleka vitu,tapeli atampigia simu tena samahani naomba uniwekee na pesa kwenye namba yangu naona umeme umeisha hela utaikuta huku ukileta vitu.

Huyo boda akishaweka iyo ela kwenye simu ataenda location aliyoambiwa jamaa(tapeli)anaishi atapiga simu weee haipatikani

NDO ANAKUWA ASHALIZWA HIVYO
 
Ukiona mtu anaanza kupiga Dana dana mara hiki mara kile, na si kama mlivyozungumza mwanzo jua kabisa hapo Kuna uwalakini na jambo hilo.
 
Mi niliambiwa niende kasanga( Morogoro)kupima kazi ya tiles, kabla ya kwenda boss akanambia anaingia ofisin kwahiyo akanipa namba ya mtu alieko site.

Namchek mshkaj anasema ayaaa nimetoka niko mikese afu gar haina mafuta kwahiyo nimtumie hela ya mafuta afu boss akitoka kwenye kikao ofisin atanilipa.

Akaanza oooh unajua fundi piga hesaab vizur afu uweke cha juu apo tugawane boss hana shida namjua sana kwenye ile site mafundi walijenga wamepiga hela kinoma yan.

Kumbe matapeli bwana nashukuru sikuwatumiaga iyo hela.
Angesema elfu 5 ivi ningetuma mana ningejua nauli, asa mi fundi nkutumie hela ya mafuta lita 7 kwan unaenda dar
 
Ahaaa
 
Afu sijui wanapeana mbinu hii Mimi alisema eti mafuta ya Piki Piki 25000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…