Utapeli unaendelea mafundi kuweni makini hii imetokea leo

Utapeli unaendelea mafundi kuweni makini hii imetokea leo

Hawa matapeli nafurahigi sana wakinopigia maana me najua kucheza nao nawachora mbaka wanajua kabisa hapa tumepata wakupiga kumbe laa hasha nawapotezea tu mda mwishoe tunakuja kutukanana na hapo wapo hoi hasa Hawa wanaojidai ni wahudumu wavoda

Me ni Mzee wa kutumia Salio zao vyema
 
huyo tapeli bado hajaiva, alitakiwa akuite mpaka saiti, ukifika ajidai yupo bize na simu muda wooote.

Ikikata hii inaingia nyingine, halafu ghafra anakuomba simu yako, anataka kumpigia mtu, akitoka hapo anaenda kwa fundi umeme napo anaachukua simu kwa maelezo yale yale kisha anamalizia kwa fundi bomba.

Akimaliza huyoooo anatokomea

Matapeli sasa hivi wamewageukia mafundi kutaka kuwatapeli. Kosa wanalofanya ni kuomba fundi atume hela ili pikipiki ijazwe mafuta ije imchukue impeleke saiti hela atarudishiwa hukohuko saiti. Mbaya zaidi fundi na huyo tapeli hawajuani
Afu sauti ya kibaba kabisa.. Makamu ya miaka 50 Hiv Daah aisee
 
Mama lishe hawajaachwa nyuma nimeona mama lishe wawili wamepikishwa chakula lundo sahani kama 50 hivi Kisha wakaambiwa kuleta shule
Wahusika huangalia kama shule Kuna ka shughuli flani known basi wanawaambie leta chakula shule
Mda mfupi akiwa anakaribia kuja wanamwambia tuma kiasi kadhaa tununue umeme hapa ukija tunakupa hela Yako
Wa kwanza alituma 100000 wa pili 15000 na wote wakaja wakaganda na sahani zao hadi tulipotoka na kuwashangaa nao wakatushangaa
Aina hii ya wizi, bodaboda nao wamepigwa sana. Anabebeshwa vitu vya kununua kwenye maduka, halafu mwisho wa siku anaambiwa atume na hela! Na biashara inaishia hapo.
 
Mama lishe hawajaachwa nyuma nimeona mama lishe wawili wamepikishwa chakula lundo sahani kama 50 hivi Kisha wakaambiwa kuleta shule
Wahusika huangalia kama shule Kuna ka shughuli flani known basi wanawaambie leta chakula shule
Mda mfupi akiwa anakaribia kuja wanamwambia tuma kiasi kadhaa tununue umeme hapa ukija tunakupa hela Yako
Wa kwanza alituma 100000 wa pili 15000 na wote wakaja wakaganda na sahani zao hadi tulipotoka na kuwashangaa nao wakatushangaa
Manina washenzi wanaroho ngumu.
Mama lishe wa watu kashaua mtaji , na hii kitaji ya kuunga unga.
 
Kuna kipindi hata bodaboda walikuwa wanatapeliwa kwa mtindo huu:
Tapeli anampigia cm boda anamwambia samahan nimepewa namba yako naomba nikuagize vitu,maana hapa kwangu nina wageni siwezi kutoka.

Hapo tapeli atafanya kama anamuagiza labda mchele nyama na mazaga mengine.

Kabla boda hajapeleka vitu,tapeli atampigia simu tena samahani naomba uniwekee na pesa kwenye namba yangu naona umeme umeisha hela utaikuta huku ukileta vitu.

Huyo boda akishaweka iyo ela kwenye simu ataenda location aliyoambiwa jamaa(tapeli)anaishi atapiga simu weee haipatikani

NDO ANAKUWA ASHALIZWA HIVYO
 
Ukiona mtu anaanza kupiga Dana dana mara hiki mara kile, na si kama mlivyozungumza mwanzo jua kabisa hapo Kuna uwalakini na jambo hilo.
 
Mi niliambiwa niende kasanga( Morogoro)kupima kazi ya tiles, kabla ya kwenda boss akanambia anaingia ofisin kwahiyo akanipa namba ya mtu alieko site.

Namchek mshkaj anasema ayaaa nimetoka niko mikese afu gar haina mafuta kwahiyo nimtumie hela ya mafuta afu boss akitoka kwenye kikao ofisin atanilipa.

Akaanza oooh unajua fundi piga hesaab vizur afu uweke cha juu apo tugawane boss hana shida namjua sana kwenye ile site mafundi walijenga wamepiga hela kinoma yan.

Kumbe matapeli bwana nashukuru sikuwatumiaga iyo hela.
Angesema elfu 5 ivi ningetuma mana ningejua nauli, asa mi fundi nkutumie hela ya mafuta lita 7 kwan unaenda dar
 
huyo tapeli bado hajaiva, alitakiwa akuite mpaka saiti, ukifika ajidai yupo bize na simu muda wooote.

Ikikata hii inaingia nyingine, halafu ghafra anakuomba simu yako, anataka kumpigia mtu ya kwake salio limekata

akitoka hapo anaenda kwa fundi umeme napo anachukua simu kwa maelezo yale yale kisha anamalizia kwa fundi bomba.

Akimaliza huyoooo anatokomea
Ahaaa
 
Mi niliambiwa niende kasanga( Morogoro)kupima kazi ya tiles, kabla ya kwenda boss akanambia anaingia ofisin kwahiyo akanipa namba ya mtu alieko site.

Namchek mshkaj anasema ayaaa nimetoka niko mikese afu gar haina mafuta kwahiyo nimtumie hela ya mafuta afu boss akitoka kwenye kikao ofisin atanilipa.

Akaanza oooh unajua fundi piga hesaab vizur afu uweke cha juu apo tugawane boss hana shida namjua sana kwenye ile site mafundi walijenga wamepiga hela kinoma yan.

Kumbe matapeli bwana nashukuru sikuwatumiaga iyo hela.
Angesema elfu 5 ivi ningetuma mana ningejua nauli, asa mi fundi nkutumie hela ya mafuta lita 7 kwan unaenda dar
Afu sijui wanapeana mbinu hii Mimi alisema eti mafuta ya Piki Piki 25000
 
Back
Top Bottom