Utapeli wa “Chumvi na Mafuta ya Upako” Wafichuliwa

Manabii wauza chumvi, Paulo anawaambia katika Wafilipi 3:19:
"Mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, na utukufu wao ni aibu yao; wanafikiri mambo ya dunia."
 
Nilienda mahali nikakuta mtu anawaonyesha kwa furaha wenzake, kichupa kidogo alichonunua kwa bei mbaya. Nafikiri kilichomvuta kukinunua kichupa kile ni kwamba aliambiwa kina mafuta ya mizeituni. Sasa kwakuwa alisoma kwenye Biblia kwamba Yesu alikuwa akienda kusali katika mlima wa mizeituni aliamini mafuta hayo lazima yana upako. Lakini si ajabu kilichokuwemo kwenye hicho kichupa sio mafuta, bali ni maji yaliyotiwa rangi😀

Kwani wanaoenda kwenye mikutano ya manabii wa uongo, wakiambiwa wanunue mafuta ya mizeituni, nani anahangaika kwenda kuyapima maabara ili ahakikishe kuwa ni mafuta au ni maji. Hivi ndivyo watu wanavyopigwa mchana kweupe.
 
Kuna nabii fulani alivyojua watu wameishtukia chumvi ya kununua, akawa anagawa bure chumvi. Lakini saa ya maombezi anawaambia watu watoe sadaka ya kujimaliza. Mtu anayetoa pesa ndefu ndo anaombewa kwa kuwekewa mikono.

Soma Biblia yote hautaona Mitume wakitoza pesa kabla ya kuwaombea wagonjwa. Tushtuke jamani
 
Paulo ni nani bwana wewe,mhuni mmoja tu hivi!!..yesu anahubiri hamtaki,anaondoka eti kamtokea akienda damascus,akampa utume
 
Paulo ni nani? je amemzidi YESU
 
Maisha magumu na watu wanataka kutakata kwa namna yoyote ile. Sasa huku kwenye imani wameona watu weusi wengi hawana uwezo wa kuchambua mambo na kuhoji. Wanapigwa wengi sana.
 
Paulo ni nani bwana wewe,mhuni mmoja tu hivi!!..yesu anahubiri hamtaki,anaondoka eti kamtokea akienda damascus,akampa utume
Kabla Paulo hajaokoka alikuwa akiitwa Sauli. Ni kweli Sauli alikuwa zaidi ya mhuni. Lakini Yesu alimbadilisha na kumtumia kuhubiri Injili na kutenda miujiza ya kupita kawaida, lakini HAKUUZA CHUMVI WALA MAFUTA kabla ya kuwaombea wagonjwa na wenye shida.
 
Dini ni UTAPELI.
Dini sio utapeli. Utapeli ni kuwaambia wagonjwa kwamba wakitaka kupona wanunue kwanza chumvi na mafuta ya upako. Yesu aliponya watu bure (free of charge).

Mathayo 9:35 (NEN)​

Yesu akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri Habari Njema za ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi.
 
Paulo ni nani? je amemzidi YESU
Jibu hili hapa:
Warumi 1:1-17 BHN
Kutoka kwangu mimi Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, na mtume niliyeteuliwa na kuitwa kwa ajili ya kuhubiri Habari Njema ya Mungu. Hapo kale, Mungu aliwaahidi watu hii Habari Njema kwa njia ya manabii wake katika Maandiko Matakatifu. Hii Habari Njema inamhusu Mwana wa Mungu, Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kuhusu ubinadamu wake, alikuwa mzawa wa Daudi; kuhusu utakatifu wake wa kimungu, alithibitishwa kwa uwezo mkuu kwamba ni Mwana wa Mungu kwa kufufuliwa kutoka kwa wafu. Kwa njia yake, mimi nimepewa neema ya kuwa mtume, ili kwa ajili yake niwaongoze watu wa mataifa yote wapate kuamini na kutii...
 
Ukristo sio dini.
Dini ni biashara ,ukiona Ukristo umefanywa dini basi Kuna biashara ndani yake

Ukristo ni wokovu wa MUNGU kumtafuta mwanadamu aliyepotea dhambini

Dini ni njia , mishemishe, mbilingembilinge,harakati ,utapeli wa mwanadamu kutafuta pesa na ku manipulate watu kupitia jina la Mungu
 
Duh! Umechanganya masomo... lakini
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.(Yakobo 1:27 BHN)
 
Duh! Umechanganya masomo... lakini
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.(Yakobo 1:27 BHN)
Dini iliyotajwa hapa sio hizi dini zenu mnazoita Leo

Kasome tafsiri mbalimbali utajua sio hizi dini zenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…