Yani hii nchi ccm itaendelea kutawala miaka 60,000 ijayo... Yaani mpaka mwaka 2019 mtu anasema Forex ni utapeli. Bad enough mtu huyu ukute kamaliza chuo na ana degree yake ... Oohhh Lord
Mtu anakwambia kilimo hakina hasara !!! .. Mungu wangu...
Mtu analinganisha Forex na michezo ya kubeti !!! Mungu wangu ... Sasa mbona haiendi kusajiliwa kwenye ile bodi ya michezo ya kubashiri ya wakina Abas Tarimba ???
Mtu anakuja na hoja eti hakuna hela bila kufanya kazi ... Unamuuliza wale wanaonunua hisa za za DSE (Soko la hisa Dar) katika vodacom , faida wanapataje??? .. Na Mimi nikinunua Hisa za mmarekani au makampuni 30 ya mjerumani (ger30) Nina tofauti gani na huyo wa DSE??
Sasa kwa nini wa DSE asisemwe asemwe yule wa ger30 kwenye forex ??..
Ila Mimi siwalaumu watanzania maana haya ni matokeo ya Sera mbovu za nchi kufuga raia kama Kuku bandani. . RAIA hawana exposure hata ya kutembelea nchi jirani walau hata Burundi muone wengine wanaishi vipi ... Kuna vitu vingi RAIA inabidi tupate exposure ili tuweze kufanya ...
Leo Serikali ya Tanzania huwa inauza T.Bills na Tresuary Bonds zake, na huwa zinatangazwa na mawakala wa soko la hisa la Dar Es Salam... Kwa akili hizi ninazoziona humu ndio maana sishangai kuona wanunuzi wakubwa wa hizi amana za serikali huwa ni waarabu na wahindi waishio Tanzania.. Wenzenu wanaamka na misuli ni mwendo wa kusali tu kutwa nzima. Kumbe wamenunua zao amana za serikali..
Nyie endeleeni kukopana vikoba .. Nchi inaliwa na wachache kwa kuamini hakuna kazi bila kutoka jasho .. Ila sishangai sisi tulikuwa watumwa ...
NB: ifike muda kila MTU afanye aonacho kinafaa. Tumejitahidi sana kuelimisha Ndugu zetu ila matokeo yake ni kuitwa matapeli ...