Naona comment ya 2013 ndio inaingia tena kwa mara nyingine, nadhani nilishakujibu mkuuJodoki Kalimilo;
Ndugu Jodoki, majibu yako yamenifurahisha sana, inaonyesha unaupeo mzuri katika mambo haya. Mimi niimestushwa sana na kupandishwa kwa gharama ya kodi ya kiwanja changu, maeneo ya Dar. Nimeanziasha thread huku about that. Katika thread hii swali langu kuu lilikuwa ni hili;
Je, hivi inawezekana kweli kodi ya kiwanja chenye ukubwa wa acre moja ikapande kutoka 90,500 (2011/12) mpaka 340,000 (2012/13) tshs? Hivi kodi za viwanja zimepanda au unataharifa zozote za mabadiliko haya?
Tafadhali naomba unisaidie kwa ufahamu wako. Ni matumaini yangu kwamba mchango wako unaweza kuwasaidia na watu wengine.
Asante sana
Nenda kwenye halmashauri uliyopo kitengo cha ardhi watakupa mwongozo wa namna ya kufanya na kama una hela wanakupimia kisha watakupa letter of offer ambapo baadae utatakiwa kwenda ofisi wa kamishina wa ardhi ili kuweza kupata hati yako, ni zoezi linaweza kuchukua kama mwaka hivi kupata hati ila kikubwa ni eneo kupimwa kisha upate letter of offer (hii inakupa uhalali wa kiwanja chako) then baada watu wa halmashauri/manispaa wataipeleka kwa kamishina wa ardhi ili aweze kufanya taratibu zingineHabarini wadau...naomba kufahamisha ni hatua gani za kufwata ili kupata hati ya kiwanja ambacho hakina hati kabisa lakini mmiliki halali ni mimi.Thanx in advance
Mkuu sio hawana kipaji, huu uzi una miaka kadhaa na wengine wameshazeeka (jokes), kwa uzito wa issue ya ardhi nina uhakika ukisoma comments kwenye hizo page utapata jibu though kwa haraka haraka suala lako linaangukia sehemu mbili kwanza mambo ya mirathi kisha ukishakamilisha huko ndio unakuja kuangalia kuhusu umilki wa hicho kiwanja kwa jina lako then hatua za kukatia hati milki kwa kufuata taratibu sawa na watu wengine wanaomilki visivyo vya urithiKuna watu hawana vipaji vya ualimu,hata wakuelekezeje huwezi kuelewa.Mimi nina kiwanja cha urithi nyumbani kijijini kabisa nataka NIKIKATIE HATIMILIKI Naanzaje WADAU.............
Ada zinakuwaje mwaka huu?
Sio mwaka huu hata miaka mingine yaani ukiezeka tu unaletewa bill sema sehemu nyingi unakuta mpaka uweke mlinzi ndo unapewa billmwaka huu site ambazo zimewekwa paa tu bila kuhamia unalipia property tax na ya mwaka jana hata unsurveyed areas
Kwanza kuna aina mbili za hati..
1.hati ya kawaida
2.hati ya kimila
Hati ya kawaida inatolewa katika eneo ambalo lina mchoro Wa mipangomiji..na limepimwa na kupatiwa namba za viwanja....
Kwa mujibu Wa sheria za ardhi mwenye mamlaka ya umilikishaji ni afisa ardhi Mteule.....
Utaratibu ni kuwa muombaji Wa eneo lililopimwa anawasilisha barua kwa afisa ardhi Mteule Wa halmashauri husika....afisa ardhi Mteule kama Katibu Wa kamati anaratibu maombi ya umilikishaji Wa viwanja na kuingiza maombi husika katika kamati ya ugawaji Wa viwanja na mashamba ambayo mwenyekiti wake ni Mkurugenzi Wa halmashauri husika....maombi yanajadiliwa na waombaji wanabarikiwa au wanakataliwa kupewa viwanja kama viwanja ni vya serikali....
Baada ya maombi kukubalika ofisi ya ardhi inamuandalia gharama ambazo muombaji anatakiwa kulipia ili apate hati na anapewa muda Wa siku 30, ili kufanya malipo ya hati miliki ambayo ni
1.malipo ya mbele ambayo ni asilimia 7.5 ya thamani ya kiwanja
2. Ada ya maombi Tshs 20000/-
3.ada ya usajili Wa hati ambayo ni asilimia ishirini ya kodi ya ardhi
4.ada ya maandalizi ya hati tshs 50000/-
5...ada ya ramani ndogo Tshs 20000/
6.ushuru Wa serikali ambao ni asilimia moja ya kodi ya ardhi kwa Mwaka...
7.kodi ya ardhi ambayo ni bei ya mita ya mraba zidisha na ukubwa Wa kiwanja....
Akishalipia anawasilisha cheti cha kuzaliwa,kiapo au passport ..na picha sita passport size kwa ajili ya kupatiwa hati mmiliki....
Hati inaandaliwa na kufungashwa tayari kwa kwenda kwa kamishna Wa ardhi na baadae kwa Msajili Wa hati Wa kanda husika kwa ajili ya kusajiliwa
Naomba kuwasilisha
Akhsante