Nyie mnawazaga kukomolewa tu. Lakini sio.
Huenda mngewabeba hawa viumbe kwa miezi 9 mngeelewa kidogo ile attachment ya mtoto na Mama yake.
Sasa mfano mumeachana sababu mwanaume ni mhuni. Mtoto atakuwa exposed kwa mambo mangapi?
Our kids are our everything. Our happiness, our comfort when lonely, and they keep us sensible and sane.
Kwann unazaa na wahuni?!
Mabinti wa siku hizi sijui mlikosa nini kwenye lishe za utotoni maana mnakuwa na akili nzito kuliko mtoto wa kindergarten.
Mnapokuwa katika umri sahihi wa kuchagua mwanaume wa maisha yenu huwa mnawengeka kweli kweli akili zenu.
Mnachaguwa watu kwa criteria za kipuuzi sana ambazo baadae hazitawasaidia lolote.
Hivi umeshawahi kuwasikiliza mabinti wanapokuwa wanamshauri mwenzao kupata mwenza?!
Utasikia mambo kama , "we toka nao wote wawili halafu utajua nani yupo serious na wewe"
"Mapenzi ya kweli ndio yatalipa kodi na ada za watoto, we mwanaume ni hela, tazama pochi mapenzi ya kweli waachie njiwa"
"Mchukue RayVan, kwanza ni handsome anajua kupendeza hata picha zake zinadamshi shost, mkipost tutakoma"
"Mume wa mtu ndio nini kwani, wa kwakwe akiwa kwake akiwa nje huku ni wetu sote, kwanza wanaume ni wachache sana kushare ni lazima aache kukutisha toka nae vizuri tu"
" Sasa kwann nimuache kwani kuolewa lazima, me sasa hivi mapema mno kuolewa, nahitaji kujifurahisha nile ujana ntaolewa nikifika 27 au 28"
Hizi ni baadhi tu ya kauli kati ya kauli bilioni kadhaa ambazo hutolewa na mabinti wa kisasa ambao huonyesha ishara ya wazi kuwa wanapoelekea sipo.
Kama jamii inabidi tujifunze kuwakalia kimya ili kama ni majanga wadili na familia zao wajifinze kwa vitendo bila msaada watanyooka sisi wanajamii tuwe watazamaji tu.
Maana jamii inajitolea kuwatetea kila uchao na kuwawekea mikakati ya kuwalinda ila ninyi mnatumia vibaya hiyo fursa kucheza na akili za watu kwa kufanya maamuzi ya kipumbavu mkijua jamii itawatakasa na kuwapa msaada na hisani na yakiwakuta ghafla mnaanza kujifanya m'mekuwa malaika ghafla huwa hamkosei ila mnakosewaga tu na kusababishiwa matatizo na kuwalaumu wanaume ambao mliwachagua ninyi wenyewe na viherehere vyenu na mashosti wanaopatikana katika kamati za uchaguzi wa boyfriend.
Sasa kabla ya kusema baba mtu ni muhuni, wewe umewahi kujiuliza wahuni toka lini wakawa baba wazuri hadi ukaamua kuwavulia na kuingia nao kwenye mahusiano ukijua ni wahuni.
Wewe unaenda jitongozesha kwa mume wa mtu, au kwa kijana bishoo msuka marasta,mvaa mlegezo,mlamba lips ambaye nina uhakika ukiambiwa usimame nae mbele ya jukwaa umtambulishe wewe mwenyewe binafsi utaona aibu tupu sababu utajua huyo si mwanaume wa kuanza nae familia , ila bado unajiachia anakupa mimba na kukutelekeza unasema muhuni, wakati unalala nae ulidhani wahuni huwa wakipata watoto wanaacha uhuni au kama ni mume wa mtu ulidhania mkewe anajiskiaje na ataamuacha mkewe awe na wewe. Sifuri kabisa.
Maisha ya laana huleta laana tu. Pambaneni. Malipo ni hapa hapa duniani.