Kwann unazaa na wahuni?!
Mabinti wa siku hizi sijui mlikosa nini kwenye lishe za utotoni maana mnakuwa na akili nzito kuliko mtoto wa kindergarten.
Mnapokuwa katika umri sahihi wa kuchagua mwanaume wa maisha yenu huwa mnawengeka kweli kweli akili zenu.
Mnachaguwa watu kwa criteria za kipuuzi sana ambazo baadae hazitawasaidia lolote.
Hivi umeshawahi kuwasikiliza mabinti wanapokuwa wanamshauri mwenzao kupata mwenza?!
Utasikia mambo kama , "we toka nao wote wawili halafu utajua nani yupo serious na wewe"
"Mapenzi ya kweli ndio yatalipa kodi na ada za watoto, we mwanaume ni hela, tazama pochi mapenzi ya kweli waachie njiwa"
"Mchukue RayVan, kwanza ni handsome anajua kupendeza hata picha zake zinadamshi shost, mkipost tutakoma"
"Mume wa mtu ndio nini kwani, wa kwakwe akiwa kwake akiwa nje huku ni wetu sote, kwanza wanaume ni wachache sana kushare ni lazima aache kukutisha toka nae vizuri tu"
" Sasa kwann nimuache kwani kuolewa lazima, me sasa hivi mapema mno kuolewa, nahitaji kujifurahisha nile ujana ntaolewa nikifika 27 au 28"
Hizi ni baadhi tu ya kauli kati ya kauli bilioni kadhaa ambazo hutolewa na mabinti wa kisasa ambao huonyesha ishara ya wazi kuwa wanapoelekea sipo.
Kama jamii inabidi tujifunze kuwakalia kimya ili kama ni majanga wadili na familia zao. Sisi tuwe watazamaji tu. Maana jamii inajitolea kuwatetea na ninyi mnatumia vibaya hiyo fursa kucheza na akili za watu kwa kufanya maamuzi ya kipumbavu halafu yakiwakuta ghafla mnaanza kujifanya m'mekuwa malaika na kuwalaumu wale ambao mliwachagua ninyi.
Sasa kabla ya kusema baba mtu ni muhini wewe umewahi kujiuliza wahuni toka lini wakawa baba wazuri. Wewe unaenda jitongozesha kwa mume wa mtu, anakupa mimba na kukutelekeza unasema muhuni, wakati unalala nae kama mume wa mtu ulidhania mkewe anajiskiaje.
Maisha ya laana huleta laana tu. Pambaneni. Malipo ni hapa hapa duniani.